WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Friday, 21 August 2009

ZANZIBAR U-17 "KARUME BOYS" 3-1 KENYA. "SERENGETI BOYS" 0-3 SUDAN

Nossor Ali (kushoto) akisherekea wakati alipopachika bao la tatu dhidi ya Kenya.


Timu ya Taifa ya vijana ya Zanzibar "Karume Boys" U-17 imeweza kushinda kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya timu ya Taifa ya vijana ya kenya katika michuano ya challenge cup U-17 iliyoanza wiki hii mjini khartoum-Sudan,bao la kwanza la Zanzibar "karume Boys ilipatikana katika dakika ya 21 lilofungwa na Mohammed Abdulahi,vijana hao kutoka Visiwani waliweza kupachika bao la pili dakika 29 mfungaji akiwa ni Juma Ali,ambapo hadi mapumziko Zanzibar ilikuwa inaongoza kwa bao 2-0.
Katika kipindi cha pili Kenya ilionekana kuongeza nguvu za mchezo ambazo zilipelekea kupata bao kwenye dakika ya 69 lililofungwa na Daniel Mwaura kwa njia ya Penalti,
baada ya bao hilo Kenya wakiwania kusawazisha walijikuta wakitundikwa bao la tatu na vijana hao wa Zanzibar kwa bao lilowekwa kimiani na Nassor Ali.
Zanzibar U-17 "karume Boys wanatarajiwa kuingia tena kiwanjani jioni hii kwa kupambana na Ethiopia ambayo tayri imepoteza mechi yake ya mwanzo dhidi ya Uganda kwa kuchapwa
bao 4-0.

katika mechi nyingine timu ya Taifa ya Tanzania U-17 "Serengeti Boys" imefungwa na wenyeji wa mashindano hayo Sudan 3-0, hata hivyo "Serengeti boys wamepewa ushindi katika mechi hiyo na kamati inayosimamia mashindano hayo ya vijana baada ya kugundulika wenyeji hao wa sudan walichezesha vijana wenye umri mkubwa kati yao wapo wenye umri wa miaka 18 na mmoja kati ya vijana hao wa sudan alikuwa na umri wa miaka 20,hivyo Serengeti Boys wamepata ushindi katika mechi hiyo moja kwa moja kutokana na kanuni za Cecafa.
-------------------------------------------------------------------------------------------------