WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday 9 September 2009

ORANJE FOOTBALL ACADEMY YAMPA PASI RIVALDO YA KWENDA NOTHERN IRELAND KUCHEZA SOKA YA KULIPWA

Rivaldo (wa kwanza kulia nyuma)akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Taifa ya Mozambique kabla ya kupambana na Bafana Bafana mjini Durban-South Africa.
----------------------------------




Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini ORANJE FOOTBALL ACADEMY leo imekamisha safari ya mchezaji wa timu ya Taifa ya Mozambaique "Mambas" ya kwenda kucheza soka ya kulipwa nchini Nother Ireland,

Rivaldo ambae ni mwenye asili ya Kitanzania ambae amezaliwa katika mji wa Nampula mji mkubwa wa 3 nchini Mozambique amekamisha safari hio leo na ataondoka mjini Maputo siku ya tarehe 17 sep 2009 mchana kuelekea Johannesburg ambapo ataunganisha ndege kwenda London siku hio na baadae London hadi Belfast-Nother Ireland ambapo atajiunga na timu yake mpya inayoshiriki ligi ya Championship(First Div) iitwayo BANGOR F.C.

Rivaldo jana alichukua Visa kutoka katika ubalozi wa England uliopo Maputo Mozambique na leo amekamilisha safari,ambapo alitakiwa kuripoti wiki hii katika timu yake hio mpya lakini kutokana na ndege kujaa ataondoka siku ya tarehe 17 sep mchana kuelekea huko,

mchezaji huyo ambae amemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu uliopita na klabu ya Sporting Lisbon ya Portugal ambao walimkodisha kwa timu ya Real Masáma ya Lisbon(Real masáma ni klabu ambayo Sporting Lisbon ya Portugal inaitumia kuweza kupandisha viwango vya soka kwa vijana wake ambapo Naní wa Manchester United pia alipelekwa hapo wakati akiwa katika klabu hio ya Lisbon kabla ya kumchukua tena na baadae kwenda Manchester United).

kabla ya Rivaldo kuchukuliwa a Sporting Lisbon alikuwa katika timu pinzani ya Benfica ya Portugal ambao wao walimchukua akiwa na umri wa miaka 15 akitokea Manchester United ya England ambapo alikuwepo huko kwa miezi sita, na kushindwa kubakia hapo kutokana na kukosa work permit na hivyo kuamua kwenda Benfica ya Portugal,

akiwa katika timu ya Manchester United Academy Rivaldo alikuwa pamoja na wachezaji nyota katika academy hio ya Manchester ambapo alikuwa na Rossi mchezaji chipukizi wa timu ya Taifa ya Italy pamoja na Pique mlinzi wa kati wa timu ya F.c Barcelana ya Spain ambao wao walikuwa na umri mkubwa kidogo kulikoni Rivaldo wakiwa katika Manchester United Academy.

Akiongea kwa njia ya simu dakika chache zilizopita Rivaldo alimwambia kiongozi wetu anaeishi Holland kuwa yupo fiti na ataweza kuitumikia vizuri timu yake hio mpya kuweza kuonyesha uwezo wake mkubwa ambao unamfanya kuwemo katika timu za taifa za U-18, U-20, na timu ya taifa ya Senior ya Mozambique kutokana na kiwango chake.

kituo cha kukuza soka kwa vijana cha Oranje Football Academy kwa kushirikiana na C.E.O wake mr Jacky Mahood ambae ni raia wa Nother Ireland,vice president wao anaeishi mji wa Belfast Nothern Ireland Mudathir ambae tokea leo yupo hapa nchini,pamoja kiongozi mwingine wa O.F.A ambae anaishi Holland ambae ni kiungo kikubwa cha kufanikisha safari hio wameweza kutoa nafasi hio kwa mchezaji huyo wa Kimataifa mwenye umri wa miaka 18 ili kuweza kuwa mchezaji wa kwanza kwenda kufungua milango ya soka kwa vijana hao kimataifa.

Kutokana na kuwa Rivaldo amekulia katika soka ya europer kituo hicho cha O.F.A kimetoa nafasi hio kwake kwani ataweza kuonyesha soka ambayo inahitajika katika timu yake hio mpya ambapo hivi karibuni pia itaweza kuchukua wachezaji wengine 2 washambuliji wa timu ya Taifa ya Tanzania ambao majina yao yatatolewa katika mtandao huu unaomilikiwa na kituo cha kukuza soka kwa vijana cha ORANJE FOOTBALL ACADEMY mara baada ya mipango yote kukamilika.

Rivaldo ni mchezaji ambae ataweza kuijengea sifa Academy yetu kwa kuaminika huko Nothern Ireland kwani kutokana na uzoefu mkubwa alionao ataweza kujenga uaminifu kwetu na timu yake hio na kufanya kuweza kutoa nafasi kwa vijana wetu hapo baadae.

Mwezi uliopita Rivaldo alikuwepo Portugal na timu ya taifa ya U-20 walioshiriki mashindano yanayofanyika kila mwaka yanayoshirikisha nchi zote zilizotawaliwa na zinazozungumza lugha ya kireno. na wiki iliyopita alikuwa katika timu ya Taifa ya "Mambas"ambao walicheza na Kenya katika mshindano ya kuwania ticket ya kombe la dunia na Orange Africa cup(ambapo Rivaldo hakuwemo katika kikosi cha mwisho siku ya mechi na kenya)

KWA NIABA YA VIONGOZI, WACHEZAJI, WANACHAMA, NA WAPENZI WOTE WA SOKA WA ORANJE FOOTBALL ACADEMY WANAMTAKIA KIJANA MWENZAO RIVALDO KILA LA KHERI WAKATI AKIWA HUKO,NA KUMATAKIO MAFANIKIO MEMA KWANI NDIO ITAKUWA NI MWANZA WA KUFUNGUA MILANGO KWA SOKA YA TANZANIA KWA UJUMLA.

KILA LA KHERI RIVALDO.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Rivaldo akiwa katika mechi na timu ya Taifa ya Mozambique.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Rivaldo (wa kwanza kulia)akiwa katika mazoezi na timu ya Taifa ya "Mambas"
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Rivaldo akiwa katika mazoezini na timu ya Taifa ya Mozambique
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Rivaldo akishangilia mara baada ya filimbi ya mwisho
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Rivaldo akiwa katika moja ya magazeti ya sports la Portugal ambapo wamemfanansha ushambuliaji wake wa kasi kwa wapinzani ni sawa na Joáo Couto aliekuwa mshambuliaji hatari wa Benfica miaka ya nyuma.
------------------------------------------------------------------------------------------------
Rivaldo akimiliki mpira katika mechi yake na Taifa Stars katika uwanja wa taifa ambapo Mozambiaque ilishinda kwa bao 1-0
-------------------------------------------------------------------------------------------------