WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 19 September 2009

RIVALDO KUONA MECHI YA TIMU YAKE LEO KABLA KUANZA MAZOEZI JUMATATU

Chipukizi wa kimataifa RIVALDO ambae jana aliwasili mjini belfast tayari kuonyesha uwezo wake katika timu ya daraja la kwanza Championship nchini NOTHERN IRELAND, jana jioni alikutana na manager wa timu yake ya BANGOR F.C ya mji wa BELFAST na kutambulishana kwa mara ya kwanza tokea nyota huyo Rivaldo kuwasili mjini hapo mapema asubuhi jana.

Leo manager huyo COLLIN McCURDY atafatana na nyota huyo kwenda kuona mechi ya ligi ya Champioship ambapo BANGOR F.C watacheza nyumbani na timu ya COAGH UNITED ambapo itakuwa ni mechi ya nne tokea kuanza kwa ligi hiyo ambapo BANGOR f.c imeshinda mechi 2 na kupoteza mechi moja ugenini wiki iliyopita hivyo kuwa na point 6 kutoka katika mechi 3,


timu 4 za kwanza zinafatana kwa kushika uongozi wa ligi hio kwa kuwa na point sawa kila moja ikiwa na point 7 lakini zikiwa zimetofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa, huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na DONEGAL CELTIC yenye point 7 ikiwa mbele kwa mabao ya kufunga,


nafasi ya 5 na ya 6 kuna timu 2 ambapo ipo nafasi ya sita BANGOR F.C wapo hivi sasa kabla ya mechi ya leo timu zote mbili zina point 6 kila moja,


akiongea kwa njia ya simu na web blog hii ya ORANJE FOOTBALL ACADEMY kutoka Belfast RIVALDO alisema leo atafatana na manager wake COLLIN McCURDY kuangalia mechi ambapo ataweza kupata nafasi ya kuona uwezo wa timu pamoja na kufatilia kwa makini nafasi yake anayochozea ili aweze kuipima akilinganisha na uwezo wake na hio itampa uwezo mzuri wa kuweza kujua ni jinsi gani anaweza kutoa mchango wake kwa klabu yake hio, alisema imekuwa ni vizuri kuiona klabu ikicheza mechi kabla ya kuanza mazoezi,kwavile wanacheza nyumbani naamini kila mchezaji ataweza kuonyesha uwezo wake mkubwa ili washinde mechi hio ambapo ikisaidiwa na washabiki ni dhahiri ataweza kubahatika kuona uwezo wa timu kabla ya kuanza mazoezi mapema jumatatu ijayo.


KWA NIABA YA ORANJE FOOTBALL ACADEMY INAMTAKIA RIVALDO KILA LA KHERI NA MAFANIKIO MEMA.

-------------------------------------------------------------------------------------------------