WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Friday, 26 March 2010

O.F.A U/14 KIWANJANI TENA KATIKA MECHI YA LIGI

Vijana Wadogo wa O.F.A U/14 kesho wataingia tena kiwanjani kupambana na Simba Kids katika mechi ya ligi ambayo itafanyika katika kiwanja cha Mao Tse Tung B.
Vijana hao wanatarajia kuendelea na kasi yao ya ushindi na kutandaza soka ambayo inalingana na wakubwa zao kutokana na kutumia mbinu moja ambazo wanapewa na walimu wao mahiri wa O.F.A katika mechi iliyopita iliweza kuirarua African Kids jumla ya bamao 4-1.
.................................

O.F.A kubwa itajimwaga tena kiwanjani siku ya Ijumaa tarehe 02-04-2010 kupambana na Ivory Coast mechi ambayo itakuwa ni ya mwisho ya hatua ya makundi ambapo O.F.A inajitupa kiwanjani ikiwa tayari na ticket ya kuingia katika hatua ya mwisho ya kumpata Bingwa wa msimu huu 2010.
O.F.A imejihakikishia kuingia katika hatua hio ya mwisho ambayo washindi 3 wa kila kundi watasonga mbele,baada ya kuwa na uhakika wa nafasi moja kati ya 3 O.F.A itaendelea na ubabe wake katika ligi hio na kutaka kuhakikisha kuwa inashinda kila mechi ambayo itakuwa mbele.
katika mechi ya msimu uliopita Ivory Coast iliweza kuifunga O.F.A mechi ambayo ilipelekea O.F.A kupoteza nafasi ya kutwaa Ubingwa kwahio mechi hio ya ijumaa vijana wa O.F.A itaichukulia umuhimu na kumaliza deni la kufungwa na vijana hao Ivory Coast msimu uliopita.
katika moja ya mikakati ya O.F.A ni kuhakikisha kuwa hakuna timu inawazunguka kuwafunga kwa mara nyingine kwahio vijana wanatarajia kuonyesha kiwango cha hali ya juu na kuibuka na ushindi mnono katika mechi hio ya ijumaa.

Mpaka sasa katika msimo wa makundi Oranje Football Academy inaongoza kundi lake baada ya kucheza mechi 7,kupoteza mechi 1,sare mechi 1 , na kushinda mechi 5 huku ikijikusanyia point 16 ambazo tayari imejihakikishia kuwa timu ya kwanza katika makundi kuingia katika hatua ya fainali ya kumpata bingwa wa msimu huu 2010.
Vijana wa O.F.A watataka kuhakikisha wanamaliza mechi ya kundi lake bila ya kupoteza mechi nyingine hivyo kujihakikishia kuongoza katika kundi lake.

wakati wanaoshika nafasi ya pili na ya tatu katika kundi hilo watakutana wenyewe kwa wenyewe katika mechi ya kukamilisha mzunguko huo ambapo nafasi ya pili akiwa na point 14 na watatu imejikusanyia jumla ya point 13 wakati kwenye nafasi ya 4 inashikiliwa na timu yenye point 12 kati ya timu zote 3 chini ya O.F.A zina nafasi ya kujipatia nafasi moja kati ya 2 zilizobakia hivyo kuzifanya mechi za mwisho kutoa washindi wawili waliobakia ambapo mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa kwa kuanza wakati mmoja katika viwanja tofauti.
..........................................................................................................................................