WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday, 5 April 2010

"DERBY" ORANJE FOOTBALL ACADEMY 1-0 SHANGANI F.C


Vijana wadogo wanaochipukia kwa kasi kubwa katika soka Oranje Football Academy U/14 leo wametoa kichapo kwa wapinzani wao wakubwa Shangani F.c baada ya kuitungua bao 1-0 katika pambano safi la kuvutia lililomalizika hivi punde katika kiwanja cha Mao Tse Tung B.


katika pambano hilo la kuvutia lilowavutia washabiki wengi waliokuwepo kushuhudia mechi hio ambayo ilikuwa na upinzani mkubwa nje ya kiwanja karibu wiki nzima kwa wapenzi wa pande zote mbili.


Timu zote mbili zilicheza soka safi yenye upinzani mkubwa ambao uliwaacha washabiki kuwa na wakati mgumu wa kutabiri ni nani ataweza kuibuka mshindi katika mechi hio ambayo ilikuwa ni sawa na fainali kwa pande zote mbili ambapo walishambuliana kwa nguvu kutafuta ushindi katika mechi hio ya leo.


Alikuwa ni yule yule muuaji mshambuliaji hatari wa vijana wa Oranje Football Academy Moh'd Omar alieweza kuwazima Shangani F.C baada ya kupachika bao safi na kumfanya kuwa "Match Winner"na kuipeleka Oranje Football Academy U/14 moja kwa moja katika ya fainal ya Play-Off pia kuifanya O.F.A kuendelea kuongoza katika kundi A


Moh'd Omar mshambuliaji ambaye atakuwa ni mmoja kati ya wafungaji bora wa hapa nchini miaka ya karibuni kama ataendelezwa na kubakia na kasi yake aliyokuwa nayo sasa ili kuweza kufikia lengo hilo,

kama wataalamu wa soka wataweza kufatilia viwango vya wafungaji wote wa soka nchini wenye umri wake hakuna shaka wataweza kugundua kiwango cha Nyota huyu anaechipukia ana uwezo mkubwa katika safu ya ufungaji.


Katika mechi ya mwishoni mwa wiki iliyopita mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa kumiliki mpira na skills nzuri mbinu za kuwachomoka mabeki pamoja na kipaji kikubwa cha kuwasoma makipa na kupachika mabao kwa staili anayotaka aliweza kuipatia O.F.A ushindi baada ya kupachika mabao yote 2 ambayo yalipelekea vijana wa O.F.A kuichapa Black Lion 2-0.


Kwa ushindi huo wa leo Unazifanya timu zote mbili za O.F.A ya wakubwa na wadogo kuingia katika hatua ya Fainali pamoja na kuongoza katika makundi yao


Uongozi wa Oranje Football Academy kwa pamoja unatoa pongezi kwa vijana wake wadogo U/14 pamoja na wakubwa zao kwa kazi nzuri ya kuweza kuvuka hatua ya awali na kutinga hatua ya final.
.........................................................................................................................................................................