WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday 3 May 2010

"DERBY" ORANJE FOOTBALL ACADEMY YAICHAPA NA KUIFUNZA SOKA MKUNAZINI F.C BAADA YA DAKIKA 120 ZA MCHEZO

Kikosi cha Oranje Football Academy (kilicho waua Mkunazini f.c )kikiwa katika picha ya pamoja na kocha Bo Nilson kutoka Sweden hapo ni katika moja ya mechi ambapo Kocha Nilson (watatu kulia) alibahatika kuwaona vijana wa Oranje Football Academy wakitandanza soka baada ya kocha huyo kutoka Sweden kuwa na vijana hao O.F.A katika mazoezi
.........................................................................................................................................................................
O.F.A wakiwa katika mazoezi
.........................................................................................................................................................................
Kocha Nilson akisimamia mazoezi ya O.F.a
.........................................................................................................................................................................
(Kocha Bo Nilson akiwa na vijana wa Oranje Football Academy mazoezini)

.........................................................................

Mabingwa wa soka wa knock-out U/17 Oranje Football Academy jana waliwatupa nje ya michuano hio wapinzani wao wakubwa Mkunazini F.c baada ya pambano kali lililoamuliwa kwa sheria ya penalti 5 kwa kila upande kutumika kutokana na kumaliza dakika 90 za mchezo matokeo yakiwa 3-3 na dakika 30 za nyongeza zikimalizika matokeo yakiwa baada ya dakika 120 za mchezo 3-3.

Pambano hilo ambalo lilihudhuriwa na mashabiki wengi ambalo lilikuwa linawakutanisha mabingwa wa knock-out msimu ulipita U/20 na mabingwa wa U/17 msimu uliopita 2009.


Mkunazini F.c ambao ni mabingwa wa msimu uliopita U/20 Huku wakidhamiria kutimiza ahadi yao ya kuiangamiza Oranje Football Academy ambao pia ni mabingwa U/17 msimu uliopita waliweza kuandika mabao mawili hadi kufikia dakika ya 30 za mchezo kipindi cha kwanza.


Baada ya kuingia kwa mabao hayo 2 vijana wa Oranje Football Academy walianza kutulia na kujipanga vizuri katika nafasi ya ulinzi huku safu ya kiungo na ushambuliaji wakianza kuelewana kama kawaida yao ambapo waliweza kuandika bao 1 kabla ya mapumziko hivyo kufanya pambano hilo kwenda mapumziko mabao yakiwa Mkunazini f.c 2-1 O.F.A


Kipindi cha pili kilianza kwa vijana wa Oranje Football Academy wakitumia pasi za haraka haraka zenye uelewano mkubwa waliweza kupachika bao la kusawazisha na kulifanya pambano hilo kuwa kali na la kusisimua ambapo O.F.A waliweza kusawazisha nakufanya mabao kuwa 2-2.

Ilikuwa ni Mkunazini F.c katika dakika ya 75 wakiandika bao la 3 na kuwafanya washabiki wao kuanza kushangilia ushindi katika pambano hilo.


zikiwa zimesalia dakika 5 pambano hilo kumalizika Oranje Football Academy walisawazisha bao hilo na kufanya matokeo kuwa 3-3 hadi mwisho wa dakika 90 za kawaida.



pambano hilo liliendelea kwa dakika 30 za nyongeza kuweza kumpata mshindi lakini hadi mwisho wa dakika 120 mabao yalikuwa ni 3-3.



mabao ya Oranje Football Academy yalipachikwa kimiani na Yussuf Miraji 2 na Seif Abadalla 1 ambae pia alitoa pasi kwa mabao 2 yaliyopachikwa wavuni na Yussuf Miraji.


kutokana na mechi hio kumalizika dakika 120 bila kupatikana mshindi Sheria ya Penalti 5 ilitumika ambapo Oranje Football Academy ilipachika kimiani penalti 4 kati ya 5 na Mkunazini F.c pia walifunga 4 na kupoteza 1. huku Beki wa O.F.A Muhene Majid akimpa kipa penalti ya 5 Mkunazini f.c walipaisha juu.


wafungaji wa penalti kwa upande wa O.F.A ni (1) Nassir Ali, (2)Yussuf Abdalla, (3) Mudathir Yahya, (4) Kibwana Khamis, penalti ya 5 Muhene Majid(alipoteza)


Penalti moja kwa kila upande iliongezwa kutokana na matokeo kuwa 4-4 katika penalti hizo.
Seif Abdalla aliipachikia Oranje Football Academy penalti ya 6 ambapo Mkunazini F.c waliweza kufunga pia na kufanya kuwa 5-5.


Alikuwa ni mshambuliaji nyota wa Oranje Football Academy Mzee Kheri " Match Winner" aliepachika penalti safi ya 7 na Mkunazini kupaisha juu na kuifanya Oranje Football Academy kuiondoa Mkunazini f.c katika michuano hio ya msimu huu 2010.


Kutakana na Mkuanzini kuahidi kuikomoa O.F.A katika pambano hilo walishindwa kutimia ahadi zao ambapo waliweza kupata funzo la soka kutoka kwa chipukizi hao wa kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini ambao wanazidi kuwiva kisoka siku hadi siku, pamoja na kuwa Mkunazini F.c kuongoza mara tatu katika dakika 90 za pambano hilo vijana wa O.F.A waliweza kutuliza soka na kushinda pambano hilo kwa jumla ya mabao 9-8.


hadi mwisho wa pambano hilo ilikuwa ni vijana wa O.F.A waliotoka kiwanjani na furaha na kupeleka majonzi makubwa katika kambi ya Mkunazini f.c
.........................................................................................................................................................................