WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 2 May 2010

"DERBY" ORANJE FOOTBALL ACADEMY YAIFUNZA SOKA MKUNAZINI F.C MECHI ILIYOMALIZIKA KWA DAKIKA 120

Mabingwa wa soka wa Knock-out U/17 Oranje Football Academy leo wamewafunza soka na kukata midomo ya wapinzani wao wakubwa Mkunazini F.C U/20 baada ya kuitupa nje ya michuano ya Knock-out ya msimu huu 2010 katika mechi kali iliyokuwa na upinzani mkubwa ambayo ilikuwa ya kiwango cha hali ya juu kwa pande zote mbili.

Mkunazini F.C ambao ni mabingwa wa Knoc-out U/20 msimu uliopita 2009 waliweza kuanza kwa hasira mechi hio kwa kutaka kutimiza ahadi yao ya kuikomoa na kuingamiza Oranje Football Academy waliweza kuanza kufurahia azma yao hio kwa kuanza kushangilia ushindi baada ya kuweza kuweka kimiana mabao 2 ya haraka haraka ndani ya dakika 30 za kipindi cha kwanza na kuifanya Mkunazini F.c iongoze kwa mabao 2-0,

Baada ya kuingia kwa mabao hayo 2 vijana wa Oranje Football Academy walianza kutulia na kujirekebisha katika safu ya ulinzi kutoruhusu tena magoli zaidi na safu ya kiungo na ushambuliaji kuanza kazi ya kucheza soka kama kawaida yao ambapo vijana hao wa Oranje Football Academy waliweza kupachika bao moja dakika za mwisho za kipindi cha kwanza hio kuifanya mechi hio hadi mapumziko O.F.A 1-2 Mkunazini.

Kipindi cha pili vijana wa Oranje Footbal Academy walizidisha kusukuma mashambulizi makali wakitumia pasi za haraka haraka kwa uelewano mkubwa waliweza kupachika bao la pili na kuifanya mechi hio kuwa 2-2.

Zikiwa zimesalia dakika 15 kumalizika pambano hilo Mkunazini F.C waliweza kupachika bao la 3 na kuifanya tena Oranje Football Academy kuwa nyuma kwa mara nyingine tena 2-3.

katika dakika ya 85 zikiwa zimesalia dakika 5 kumalizika kwa pambano hilo huku Mkunazini F.C wakishangilia ushindi walikuwa ni vijana wa Oranje Football Academy tena kudhihirisha uwezo wao wa soka kwa kuweza kupachika bao safi la kusawazisha ambapo hadi mwisho wa dakika 90 mabao yalikuwa ni 3-3.

katika mechi hio ambayo ni lazima kupatikana mshindi iliendelea kwa dakika za nyogeza 30 ambapo mashambulizi yalikuwa makali kwa pande zote mbili ambapo hadi mwisho wa dakika 120 matokeo yalikuwa O.F.A 3-3 MKUNAZINI F.C

Mabao ya Oranje Football Academy yalipachikwa kimiani na Yussuf Miraji mabao 2 na Seif Abdalla 1.

Kutokana na matokeo hayo ya 3-3 sheria za penalti zilitumika ambapo Oranje Football haikufanya makosa baada ya kupachika mabao 5 bila ya kukosa penalti yoyote katika penalti zote 5 ambapo pia Mkunazini walijibu kwa kufunga penalti 5.

Penalti ya 6 OF.A walipoteza kwa kumpa kipa na Mkunazini Kupaisha.

Oranje Football Academy waliweza kupachika bao safi penalti ya 7 na MkunaziniF.C wakapaisha tena juu ya Goli penalti hio na kuifanya Oranje Football Academy kushinda ushindi wa jumla ya mabao 9-8 hadi mwisho wa matokeo ya mechi hio.


Oranje Football Academy ni kituo cha kukuza Soka kwa Vijana nchini hilo ilikuwa ni funzo kwa Mkunazini F.c kutoka kwa vijana O.F.A.

Kesho mazoezi yataendelea kama kawaida kwa chipukizi wa U/14 na wakubwa zao kutokana na mikikimikiki ya leo kesho atakuwa na mapumziko.
.........................................................................................................................................................................
Kikosi Cha Oranje Football Academy kikiwa katika picha ya pamoja na Kocha Bo Nilson(watatu kulia waliosimama) kutoka Sweden katika moja ya mechi ambazo Kocha huyo alibahatika kuwaona vijana hao baada ya kuwapatia mazoezi hapo kabla .........................................................................................................................................................................