WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 2 May 2010

(kikosi cha Oranje Football Academy kikiwa katika picha ya pamoja na kocha Bo Nilson kutoka Sweden watatu kulia katika moja ya mechi ambayo kocha Nilson alibahatika kuwaona nyota hao wa O.F.A baada ya kuwa na vijana hao katika mazoz



Mabingwa wa soka wa Knock-out U/17 Oranje Football Academy leo wameweza kutoa kichapo kwa kuwafunza soka wapinzani wao wakubwa Mkunazini F.C U/20 baada ya kuitupa nje ya michuano hio katika pambano kali la soka lililomalizika kwa mikwaju ya penalti baada ya kwenda sare ya mabao 3-3 katika muda wa kawaida wa dakika 90 ambapo muda wa nyongeza wa dakika 30 za kumpata mshindi hazikuweza kubadilisha matokeo hayo ambapo hadi mwisho wa dakika 120 matokeo yalikuwa Mkunazini F.C 3-3 O.F.A




Mkunazini F.C ambao ni mabingwa wa Knock-out U/20 msimu uliopita waliuanza mchezo kwa hasira kwa kutaka kutimiza ahadi yao ya kuikomoa na kuingamiza Oranje Football Academy ambapo walianza kusherehekea ushindi wa mabao 2-0 ndani ya dakika 30 za kipindi cha kwanza.




kutokana na kuingia kwa mabao hayo mawili kuliwafanya vijana wa Oranje Football Academy kuanza kutulia na kujipanga vizuri katika safu ya ulinzi kuhakikisha hakuna makosa tena yatakayosababisha kufungwa goli jingine huku upande wa viungo na washambuliaji wakianza kuelewana kama kawaida yao waliweza kupachika bao na kabla ya kwenda mapumziko na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa Mkunazini f.c 2-1 O.F.A




Kipindi cha pili vijana hao wa Oranje Football Academy waliweza kutulia na kupeleka mashambulizi ya nguvu ya mfululizo kwa kutumia pasi za haraka haraka waliweza kupachika bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 2-2.




Ilikuwa ni Mkunazini F.c tena katika dakika ya 75 walipopachika bao la 3 na kuonekana kama mechi hio ingelimalizika kwa mabao 3-2 lakini ili kuwa ni uelewano mkubwa kwa vijana hao wa Oranje Football Academy ambao walipachika bao safi katika dakika ya 85 dakika 5 kabla ya kumalizika mchezo na kuifanya mechi hio hadi dakika 90 Mkunazini F.c 3-3 O.F.A




Katika mechi hio ambayo ilikuwa ni lazima kupatikana mshindi iliendelea katika muda wa nyongeza wa dakika 30 ambapo mashambulizi makali kwa pando zote mbili hayakuweza kutoa bao la ushindi kwa timu zote mbili na hio kuifanya mechi hio kumalizika kwa 3-3




mabao ya O.F.A yalipachikwa kimiani na Yussuf Miraji 2 na Seif Abdalla 1.




Kutokana na matokeo hayo ya dakika 120 kuwa 3-3 Sheria ya penalti ya kumpata mshindi wa mechi hio ilitumika ambapo O.F.A ilipachika mabao yote 5 na Mkunazini F.c 5.




O.F.A ilipoteza Penalti ya 6 kwa kumpa kipa ambapo Mkunazini F.c walipaisha penalti hio na kuamuriwa kuendelea tena na penalti moja kwa kila upande ambapo O.F.A ilipachika bao safi na Mkunazini f.c kupaisha juu ya goli na kuifanya waage michuno hio kwa jumla ya mikwaju ya mabao 9-8




Kesho mazoezi yataendelea kama kawaida kwa chipukizi wa U/14 na wakubwa zao U/17 watakuwa na mapumziko kutokana na machovu ya pambano la leo.


.........................................................................................................................................................................