WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday, 19 July 2010

ORANJE PASTOR ASIMAMISHWA KAZI

Pastor mwenye umaarufu mkubwa katika mji wa Harlem nchini Holland Pastor Paul Vlaar Van Obdam amefungiwa shughuli zote za kujishighulisha katika kanisa lake ambalo ni kanisa kubwa katika mji huo wa Harlem nje kidogo ya Amsterdam kutokana na kuweka uzalendo zaidi kuliko Kazi ya Bwana Mungu kanisani hapo.

Sababu ni kuwa Pastor Vlaar jumapili ya tarehe 11- 7 - 2010 wakati Holland ilipokuwa ikicheza na Spain alishangilia na kuendesha shughuli za soka kanisani hapo badala ya ibada ya kawaida ya kila jumapili.

Akitangaza kufungiwa kwake kutojishughulisha na kazi za kanisa Bishop wa mji wa Harlem alisema"amekwenda mbali sana na maadili ya Bwana Mungu hivyo suala hili sio la kuliwachia".

Pastor Vlaar siku hio ya fainali za kombe la dunia alivalia vazi la Orange pamoja na kuwaamuru pia waumini wa kanisa hilo wakiwemo waimbaji wa kwaya wakiwa wamevalia mavazi ya Orange huku wakiimba wimbo maarufu wa mashabiki wa soka au michezo yote inayoshirikisha holland kimataifa nyimbo ambazo pia zilitumika muda wote nchini afrika ya kusini kwa mashabiki wa soka wa holland "VIVA HOLLANDIA"ambapo nyimbo hizo hazikuwa hazileti maana yoyote katika shughuli zote za kawaida kanisani hapo.

kama hayo hayakutosha Pastor Vlaar alitundika ndani ya kanisa zima vipendera vya rangi ya orange pamoja na bendera za nchi huku kukiwa na mipira kadhaa bandia ikiwa imetundikwa kila sehemu kanisani hapo.

akizidisha uzalendo wake wa kushabikia soka kanisani hapo Pastor Vlaar alimuamuru mmoja wa waumini kanisani hapo kwa kumpa mpira wa aina ya "jabulani" na pastor Vlaar kupiga filimbi aliyokuwa nayo na kumuamuru ampigie shiti na baadae Pastor Vlaar kuudaka mpira huo na kuunyanyua juu kwa kushangilia akimaanisha ushindi kwa nchi ya holland siku hio ya fainali huku akishangiliwa na waumini wengi waliojaa katika kanisa hilo.

Wananchi wengi wa Holland wamelalamikia kitendo cha Bishop kumsimamisha kazi pastor Vlaar kwa kusema yeye pia ni bianadamu kama ambavyo wananchi wa nchi nzima walikuwa katika hali ya kuishangilia nchi yao tokea kuanza kwa mashindano hayo kiasi cha ofisi nyingi kufungwa au wafanyakazi kuchukua likizo siku ambazo holland walikuwa wakicheza mechi mchana kwahio pastor Vlaar aliona kuwa ni vizuri ili kuwapata waumini siku hio awakamatie katika soka na baadae aliendesha ibada ya kanisa kama kawaida ambapo kanisa lilijaa siku hio na hata watoto na vijana walijaa kanisani hapo wakiwa wamejichora usoni bendera ya nchi.

jee kwa upande wako unatoa mawazo gani kwa kusimamishwa kwa pastor Vlaar ambapo vyombo ya habari vya holland vimembatiza jina la " oranje pastor".?