WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 15 May 2011

AJAX AMSTERDAM MABINGWA WA HOLLAND







Timu ya Ajax Amsterdam ya Holland imetwaa ubingwa wa nchi hio baada ya kuwafunga mabingwa wa msimu uliopita F.C Twente jumla ya mabao 3-1katika pambano lililofanyika katika uwanja wa Amsterdam ArenA.


Hio inakuwa ni mara ya 30 kwa Ajax Amsterdam kutwaa ubingwa huo katika historia,kabla ya pambano la leo Ajax walikuwa nyuma kwa point moja dhidi ya F.C Twente ambapo pambano hilo lilichezewa katika uwanja wa nyumbani wa Ajax mbele ya mashabiki wake iliweza kuitumia vizuri nafasi ya kufungwa na timu hio ya f.C Twente katika pambano la KNVB Bekker(FA Cup)wiki iliyopita, huku ikijitayarisha kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfulululizo F.C Twente ilikuwa tayari wameandaa Helicopter kuwachukua wachezaji kutoka uwanjani na kuwarejesha nyumbani kutokana na marabara kuwa na msururu mkubwa wa mashabiki hivyo kungeliwafanya wachezaji wao kuchoka na safari ya kurejea nyumbani.


Ajax ilikuwa ya kwanza kupachika katika dakika ya 23' bao lililofungwa na Siem de Jong baada ya kupokea pasi kutoka kwa Gregory Van Der wiel, Danny Landzaat aliipatia Ajax bao la pili kwa bao la kujifunga mwenyewe huku ikiwa tena krosi kutoka kwa Van Der Wiel,


Theo Jansen alipiga shuti umbali wa mita 20 na kuiandikia F.C Twente bao la kwanza lakini alikuwa ni Sieam De Jong tena liieihakikishia Ajax Amsterdam Ubingwa huo baada ya kuipatia bao la 3 katika dakika ya 78'.


Huo ni ubingwa wa kwanza kwa Ajax Amsterdam tokea mwaka 2004 na kuifanya timu hio kutimiza idadi ya mara 3o za ubingwa huo wa Holland.