WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 14 May 2011

SIMBA S.C KUCHEZA CAF CHAMPIONS LEAGUE,TP MAZEMBE YAONDOLEWA

Simba s.c ya Tanzania imebahatika kupata nafasi ya kucheza katika mashindano ya Mwaka huu ya Caf Champions League baada ya Bodi ya Soka barani Afrika kutupa nje ya michuano hio timu ya Tp Mazembe ya Jamhuri ya Congo baada ya kugundua Tp Mazembe kumchezesha Mchezaji Janvier Besala Bokungu kinyume cha sheria.

katika uchunguzi waliokuwa wakiufanya bodi ya uchunguzi ya Caf ilibaini kuwa kutokana na kuchezeshwa mchezaji huyo kifungu cha Sheria chapter VIII kinachohusu (fraud)article 24,article 26 (qualification of players)na article 29 orange caf champions league regulation.


Sasa Simba itaendelea na michuano hio baada ya Tp Mazembe ambao ni mabingwa wa Afrika kwa miaka miwili mfululizo ambao habari hizi zitakuwa ni pigo kubwa kwao kutokana na tmu hio kusonga mbele katika hatua za makundi kutetea ubingwa wao ambapo tokea tarehe 11-05-2011 wapo nchini Brasil kwa mazoezi makali ya kujiandaa na kutetea ubingwa wao huo huku wakitakiwa na chama cha soka cha jamhuri ya congo kucheza pambano la ligi hapo kesho dhidi ya wapinzani wao wakubwa D.C Motema Pembe.


katika barua walioandikiwa uongozi wa chama cha soka cha jamhuri ya Congo ya kuwataka mabingwa hao kufika kiwanjani siku ya jumapili bila kukosa kupambana na mahasimu wao Motema Pembe ili kutoipangua ratiba ya michuano hio ya ligi na kuweza kumalizika kwa muda wake uliopangwa,ambapo mwaka jana Tp Mazembe pia ilichelewesha kwa kuahirishwa mechi kadhaa za ligi baada ya kwenda kushiriki michuano ya Cecafa.


hadi kufikia jana TpMazembe walikataa kukatisha ziara yao ya mazoezi ya wiki tatu nchini Brasil ambapo sasa pamoja na mazoezi hayo watajikuta wametupwa nje ya michuano hio mikubwa barani Afrika na pia kupoteza pambano lao muhimu la ligi ya jamhuri ya Congo na pengine kupewa adhabu ya kutotokea kiwanjani na kuvuruga ratiba ya ligi hio.


Kutokana na Tp Mazembe kutupwa nje ya michuano hio ya mwaka huu kamati ya Caf imeamua Simba ya Tanzania sasa itapambana na Wydad Casablanca wiki ijayo katika Play-off itakayochezwa kwa pambano moja tu nje ya nchi zao,ambapo nchi ya kuchezwa pambano hilo itatolewa wakati wowote kutoka sasa.


Mshindi wa pambano hilo moja atacheza katika hatua ya Mini League ya kumpata bingwa wa mwaka huu wa Afrika.

wakati huohuo timu ya E.S Setif imeifunga timu ya Coton Sport de Garoua jumla ya mabao 2-0 katika pambano la marejeano ya michuano hio ya Caf CL.


katika pambano la awali timu ya Coton Sport de Garoua iliifunga E.S Setif mabao 4-1 hivyo kutokana na matokeo hao timu ya Coton Spot De Garoua imesonga mbele katika michuano hio kucheza katika Mini-League.