WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday, 15 May 2011

U20 YAIFUNGA TIMU YA TAIFA YA MWERA 2-1

Oranje Football Academy U20 ikionyesha kandanda safi na la utaalamu wa hali ya juu leo imeweza kuifunga timu ngumu ya Taifa ya Mwera kwa jumla ya mabao 2-1.


katika pambano hilo safi ambalo vijana wa Oranje Football academy walionyeshe ilikuwa ni kutoridhishwa na kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika mechi iliyopita hivyo kupelekea vijana hao leo kuchea soka ya uhakika ili kuweza kuhakikisha inatoka na ushindi muhimu katika mechi hioya ligi inayoendelea.


katika pambano la leo mabao ya Oranje Football Academy U20 yalipachikwa wavuni na mshambuliaji wake nyota Seif Abdalla "karihe" ambae amerejea hivi karibuni kutoka katika mashindano ya Taifa Cup alipokuwa akiuwakilisha mkoa wa Pwani,


bao la Pili la O.F.A U20 lilipachikwa na kiungo nyota ambae ni "xavi" wa vijana hao wa O.F.A Mudathir Yahya.


Wakati huo huo kutokana na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa leo na vijana hao wa Oranje Football Academy aliekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania na Taifa ya Zanzibar kocha Abdulghani Msoma alivutiwa sana na kiwango kikubwa cha soka kilichoonyeshwa na nyota hao Oranje Football Academy na ameahidi kuwasaidia rasmi chipukizi hao kwa vifaa na mipango ya uendeshaji wa Academy hio.


Katika ahadi yake aliyoitoa muda mfupi tu tayari malimu huyo mwenye sifa na ubora katika kunyanyua vipaji vya soka kwa vijana ameanza rasmi leo kwa kutoa msaada wa Posho kwa timu nzima,viatu vya soka pea 10,bibz seti 1 na gloves za kipa pea 1.


Kocha Abdulghan Msoma ni mfano mkubwa wa kuingwa nchini katika kuendeleza soka kwa vijana nchini.


Kwa niaba ya Oranje Football Academy inapenda kuwaomba wafadhili mbalimbali nchini kujitokeza kuzisaidia academy kadhaa kwa lengo la kukuza soka na kunyanyua vipaji vya soka kwa vijana nchini ambao ndio hazina kubwa kwa taifa na ndio nyota wa kujivunia kwa Taifa letu hapo baadae.


Kituo cha kukuza soka kwa vijana cha Oranje Football Academy kinatoa shukurani za dhati kwa Coach Abdulghan Msoma kwa kuonyesha moyo mkubwa wa kuwasaidia vijana wetu.