WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday, 28 May 2009

KIPIMO KIZURI KWA STARS KUONEKANWA NJE

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’, Marcio Maximo amesema mchezo kati ya timu yake na New Zealand ‘Kiwis’ utakaofanyika Juni 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni kipimo kizuri kujua wapi Watanzania walipo. Maximo alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa ambayo itakuwa ya kwanza kwa Stars kucheza na timu ya Ulaya. Alisema mechi hiyo itakuwa ya kihistoria kwa Tanzania, kwani itacheza na timu bingwa ya bara la Oceania iliyoko daraja la juu kwenye viwango vya soka vya dunia na itashiriki michuano ya Kombe la Mabara itakayofanyika Afrika Kusini kuanzia Juni 14 mwaka huu. Pia alilitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuitafutia Stars mechi ngumu, ambazo zitaijenga timu na kutaka mechi ijayo ya kirafiki iwe nje ya Tanzania. Maximo alisema maandalizi yanaenda vizuri na kikosi chake kipo imara na kuwa katika wiki ya kwanza ya maandalizi waliweka msisitizo pamoja na kocha wa viungo Marcelo Guerreiro kuwajenga stamina wachezaji wake. Wakati huohuo, wadhamini wakuu wa Taifa Stars, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), inatarajia kuzindua promosheni maalumu za barabani kwa ajili ya kuwahamasisha mashabiki kujitokeza uwanjani kushuhudia mechi ya Stars na Kiwis, itakayochezwa usiku Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa SBL,Teddy Mapunda alisema promosheni hiyo itakayoongozwa na wenenguaji wa bendi ya Akudo Impact itaenda sambamba na utoaji wa tiketi za bure kwa ajili ya mechi hiyo.
-------------------------------------------------------------------------------------------------