WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday, 6 August 2015

KAMATI YA CENTRAL LEAGUE YAVUNJWA

Kamati inayosimamia mashindano yote ya soka ya vijana Wilaya ya Mjini imevunjwa. "Kamati tendaji ya zfa wilaya ya mjini leo imeivunja rasmi kamati hio kwa mujibu wa sheria baada ya kumalizika kwa muda wa kipindi cha uongozi wake "
Ni sehemu ya maelezo ambayo yamo kwenye barua kutoka Z F A Wilaya ya Mjini ambao ndio wenye mamlaka ya kuteuwa kamati hio ya vijana wilaya ya mjini barua hio imeandikwa kwa katibu wa central wilaya ya mjini anaemaliza muda wake pamoja na uongozi mzima wa kamati hio.

Uamuzi huo unaanza maramoja na uongozi mpya tunatarajia kujulikana hivi karibuni hasa kutokana na kuwa muda huu ni muda wa uhamisho na usajili wa wachezaji wa madaraja hayo,hivyo tunaamini Z.F.A itateua viongozi haraka iwezekanavyo ili kuweza kuendana sambamba na usajili pamoja kuanza ligi za madaraja hayo.

Sunday, 2 August 2015

ORANGE FOOTBALL ACADEMY YAIPONGEZA FC AZAM KWA KUTWAA UBINGWA WA CECAFA 2015
(Picha hizi mbili za juu ni kwaniaba ya Saleh Jembe)


Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini Orange Football Academy kinajumuika na Watanzania Wote nchini kuipongeza timu ya Fc Azam kwa kutwaa ubingwa wa Cecafa kwa vilabu bingwa za nchi za Afrika Mashariki na Kati huku mchezaji Mudathir Yahya alietokea katika kituo cha Orange Football Academy akiwa ni mmoja kati ya wachezaji waliochangia timu hio kuanzia mwanzo hadi kufikia hatua ya nusu fainali ya michuano hio.

Hii ni historia mpya inaandikwa na mabingwa hao wapya wa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati hivyo kuashiria mapinduzi makubwa ya soka katika ukanda huu.

Pamoja na mashindano hayo kuonyesha kuwa yanahitaji kuboreshwa ili kuondoa mtazamo wake wa sasa ambao ni mfumo wa miaka mingi na uliopitwa na wakati katika maendeleo ya soka la nchi hizo lakini Fc Azam imewezakuonyesha mabadiliko yake binafsi na kuviamsha vilabu vingine vya ukanda huu kuiga mfano huu.

Azam FC imeifunga Gor Mahia kwa mabao 2-0 na kubeba ubingwa wa Kagame wakiwa hawajafungwa hata bao moja katika dakika 90 za kawaida za mchezo, (ukiondoa mabao ya mikwaju ya penalti kati yake na Yanga katike mechi ya robo fainali.

Mwaka 2002, Tusker ya Kenya ilifanya hivyo, lakini Azam FC imefanya hivyo huku ikiwa haijafungwa hata bao moja, Simba na Yanga hazijawahi kufanya hivyo.

Bao la kwanza la Azam FC lilifungwa na John Bocco ambaye aliipangua beki ya Gor kabla ya kupiga krosi safi kabisa iliyomfikia Bocco akamaliza kazi.


Bao la pili, likafungwa Kipre ambaye alipiga mpira wa adhabu na kipa wa Gor akadhani unatoka.

Baada ya hapo, Gor iliendelea kupambana lakini ilishindwa kuukamata mziki wa Azam FC ambao walikuwa safi huku beki Serge Wawa akimtuliza mshambuliaji hatari Michael Olunga.

AZAM FC wametwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuifunga mabao 2-0 Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa fainali uliofanyia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.

Azam FC wanakuwa timu ya kwanza ya Tanzania nje ya Simba na Yanga SC kutwaa taji hilo- wakishiriki kwa mara ya tatu tu mashindano hayo baada ya mwaka 2012 walipofika fainali na kufungwa na Yanga SC 2-0 Dar es Salaam na mwaka jana kutolewa kwa penalti 4-3 mjini Kigali, Rwanda baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika ya 90 katika Robo Fainali na El Merreikh ya Sudan walioibuka mabingwa.
Timu hiyo yenye maskani yake Azam Complex, Chamazi, Mbade, Temeke mjini Dar es Salaam imeshinda mechi zake zote kuanzia Kundi C bila kuruhusu nyavu zake kuguswa hata mara moja- na ‘ilipata shida’ kidogo tu mbele ya Yanga SC katika Robo Fainali ilipolazimika kushinda kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0 dakika 90, wakati Nusu Fainali iliilaza KCCA 1-0.


Kwa ushindi huo, timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani 30,000 (Sh. Milioni 60), wakati Gor Mahia wanapozwa na dola 20,000 (Sh. Miliioni 40).

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Louis Hakizimana wa Rwanda aliyesaidiwa na Nagi Ahmed wa Sudan na Suleiman Bashir wa Somalia, hadi mapumziko tayari Azam FC walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0.
Bao hilo lilipatikana dakika ya 16, mfungaji Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyemalizia kwa kichwa krosi ya Kipre Herman Tchetche kutoka upande wa kulia.
Azam FC walitawala mchezo vizuri kwa dakika 20 za mwanzo, lakini baada ya hapo kasi yao ikapunguzwa na uchezaji wa rafu wa wachezaji wa Gor Mahia ambao hawakuchukuliwa hatua yoyote na refa Hakizimana. 

Wachezaji wa Gor walikuwa wakiwapiga viwiko na mateke wachezaji wa Azam FC na kuanguka chini wakitokwa hadi damu, lakini hiyo haikumfanya refa Hakizimana japo kutoa kadi ya njano.
Hali hiyo iliwafanya washambuliaji wa Azam waanze kucheza kwa woga na kupunguza kasi yao ya mashambulizi- huku Gor Mahia wakitumia mwanya huo nao kuanza kushambulia.
Medie Kagere alikaribia kuisawazishia Gor Mahia dakika ya 22 kama si beki muhimili wa ukuta wa Azam FC, Serge Wawa Pasacal kuokoa.
Kipindi cha pili, kocha Stewart Hall wa Azam FC alianza na mabadiliko akimtoa winga Farid Mussa Malik na kumuingiza beki David Mwantika.

Mabadiliko hayo yaliyolenga kuimarisha ulinzi yaliisaidia Azam FC kupunguza kasi ya Gor Mahia na kufanikiwa kuendelea kutawala mchezo. 
Mshambuliaji nyota kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche akaifungia bao la pili Azam FC dakika ya 64 kwa shuti la mpira wa adhabu lililompita kama mshale kipa wa Gor Mahia, Boniphace Olouch.
Mchezo huo uliotangulia mchana wa leo, KCCA ya Uganda iliifunga 2-1 Khartoum N ya Sudan na kumaliza katika nafasi ya tatu.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Aggrey Morris, Morald Said, Pascal Wawa, Farid Mussa/Erasto Nyoni dk46, Shomari Kapombe, Jean Mugiraneza, Himid Mao, Ame Ali/Frank Domayo dk69, John Bocco na Kipre Tchetche/dk88.


Gor Mahia; Boniphace Olouch, Mussa Mohammed, Sibomana Abouba, Harun Shakava, Karim Nzigiyimana, Innocent Wafula/Enock Agwanda dk83, Khakid Aucho, Godfrey Walusimbi, Medie Kagere/George Odhiambo dk83, Michael Olunga na Erick Ochieng/Ali Abondo dk74.


Hongera sana Fc Azam wachezaji,benchi la ufundi,Uongozi mzima wa klabu pamoja na Uongozi wa kampuni nzima ya Bakhresa Group kwa mchango wao mkubwa katika soka ambao umetoa ajira kwa vijana wengi ndani na nje  nchi pamoja na lengo lao la kuiletea hadhi Tanzania katika ramani ya soka barani Afrika.

Tunaamini hivi sasa nguvu zaidi zitaelekwezwa katika mashindano ya kombe la washindi wapili wa Afrika CAF. 

Tunatarajia matajiri wengine nchini watafata njayo za Azam Fc kwa maendeleo ya Taifa.AZAM GOUP COMPANIES: --->   http://bakhresa.com/

Saturday, 25 July 2015

ORANGE FOOTBALL ACADEMY CHACHU YA WATALII ZANZIBAR


Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini Oranje Football Academy " O.F.A " kupitia katika blog yake hii pamoja na plus.google.com ambayo inahifadhi picha za matukio mbalimbali ya picha yanayowekwa katika blog hii inayomilikiwa na kituo cha O.F.A hadi kufikia leo imeweza kufikisha idadi ya karibu nusu milioni ya watu duniani kote waliotembelea links hizo bila ya kujumisha idadi hio na official website ya kituo hicho www.ofaznz.net pamoja ya video ya YOTUBE ambavyo vyombo vyote hivyo kwa ujumla itafanya idadi kubwa ya kuzidi nusu millioni ya watu waliozitembelea na kuona mambo na habari mbalimbali zinazohusu Zanzibar.

Kati ya  watu hao duniani kote ambao kupitia katika links zetu hizo sio tu wameweza kufatilia soka la nchini bali wengi wao wameweza kufatilia ni nchi gani husika ambayo inazungumziwa na hivyo kuwafanya kati ya watu  hao zaidi ya nusu millioni miongoni mwao kuvutiwa zaidi ya utalii hivyo kuweza kuvumbua Zanzibar kuwa ni sehemu kubwa na tulivu duniani kwaajili ya mapumziko ya holidays kwa watalii hao.

Pamoja na kutokuwa na idadi kamili ya watu duniani kote ambao walioanza kuifatilia Zanzibar kwa  kuanzia safari yao kwa kutembelea katika links zetu hizo ni uwazi kwamba kati ya watu hao zaidi ya nusu milioni waliotembea kuna kundi kubwa sana la watalii ambao kituo chetu cha kukuza soka kwa vijana nchini ORANGE FOOTBALL ACADEMY kimekuwa ni " chachu " ya watalii hao kuja kutembelea visiwani pamoja na Tanzania kwa ujumla.

Pamoja na kwamba kituo chetu hakijanufaika hadi sasa na ujio huo wa watalii hapa nchini lakini kituo chetu kina kila sababu na  kinazidi kujivunia manufaa yanayopatikanwa nchini kwa njia hio ya utalii  zaidi ya kwa  kituo chetu ni moja ya " chachu " ya maendeleo hayo katika sekta hio ya utalii.


Katika link ya  plus.google.com idadi ya waliotembelea ni laki  444.467 wakati katika blog ya O.F.A idadi ikifikia 41,627 idadi hio kwa ujumla ni 486.094.
idadi hii haijumuishi ile ya official website ya ofaznz.net pamoja na youtube/oranje football academy zanziabr

Kituo chetu pia kinajivunia vijana wake wawili Mudathir Yahya ambae ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania pamoja na Seif Abdallah "karihe" ambae pia baadhi ya muda amekuwa ni mchezaji wa Taifa ya Tanzania wote wawili wakiwa ni wachezaji wa Azam Fc ya Dar Es Salaam pamoja na timu ya taifa ya Zanzibar, hivyo hayo ni moja ya maendeleo na malengo ya kituo chetu kutoa vijana zaidi watakaofata nyayo hizo za kaka zao siku zijazo.
Tunatarajia wadau wote  kutoa ushirikiano wa hali yoyote  na kituo chetu cha kukuza soka kwa vijana nchini ili kuweza kuendelea zaidi na kufikia malengo yake kwaajili ya Taifa letu.

BAADHI YA PICHA NA IDADI YA WALIOZIANGALIA DUNIANI KOTE 

Hizo ni baadhi ya picha zikiwa na idadi walioziangalia kupitia moja katika links zetu zinazomilikiwa na kituo chetu cha kukuza soka kwa vijana nchini cha Orange Football Academy.

idadi kamili kujumuisha na official website yetu pamoja na ile ya youtube itafuatia siku zijazo.