WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 14 January 2012

O.F.A YAISOMESHA TFF

Oranje Football Academy imeipa somo Chama cha soka nchini TFF ili iweze kulichukulia hatua zinazohitajika kuweza kuiwezesha Tanzania kujulikana kisoka Duniani na pia kuweza kushiriki michuano mbalimbali mikubwa inayosimamiwa na Caf pamoja na ile ya Fifa.

Katika somo hilo Kiongozi wa O.F.A anayeishi nchini Spain ndugu Pereira akizungumza na Blog hii inayomilikiwa na kituo cha kukuza soka kwa Vijana nchini O.F.A alisema
"ili Tanzania iweze kujulikana katika soka na kutoa upinzani kwa nchi nyingi za Africa ambazo hivi sasa zimekuwa zipo juu sana kisoka kulinganisha na Tanzania ni lazima Tanzania ibadilike iwe na wachezaji wengi wanaocheza soka ya kulipwa barani ulaya".

Aliendelea kwa kusema wachezaji wa nchi nyingi za Africa hivi sasa wanacheza katika timu kubwa miamba ya barani ulaya na ni tegemeo katika timu zao hizo ambazo huko wanapata mafunzo na mbinu za utaalamu wa hali ya juu kulinganisha na Tanzania ambao wachezaji wake wanaochezea nje hawajulikani hata ukilinganisha na jirani zao Kenya au Uganda,kama Tanzania wanataka maendeleo ya soka na wafikie katika malengo ya juu na kuwafanya wapenzi wa soka na Watanzania kwa jumla kuwa na furaha katika miaka ijayo inabidi wawe na mpango mkubwa sana wa kukuza vijana wao wa timu zao za taifa pamoja na kuwatafutia vijana hao timu za nje ili kuweza kuleta ushindani kwa nchi nyingine za Africa ambazo zimesheheni wachezaji waliozaliwa barani ulaya au kukulia huko au pia kuchukuliwa kutoka katika nchi zao kwenda kuchezea timu mbalimbali barani humo.

Katika Somo hilo kwa TFF alisema ni lazima chama cha soka cha Tanzania kwa makusudi ikishirikiana na Serikali kushirikiana ili kuweza kufikia malengo hayo ambapo yataleta mapinduzi makubwa katika soka na ajira ya vijana wengi nchini pamoja na kuliletea Taifa la Tanzania Kipato kikubwa kutoka na soka kama kitega uchumi kilichoko nje ya nchi.
Alitoa mfano kwa kusema nchi kama Brasil inaingiza billions za $ dollar kwa mwaka nchini humo kutokana na kuwa na wachezaji kila kona ya dunia ambapo fedha hizo hutumika kwa maendeleo mbalimbali nchini humo sio tu kwa wachezaji na familia zao bali banks mbalimbali na vitega uchumi ambao nyota hao hutoa ajira kwa mamilioni ya raia wa nchi hio kutokana na wachezaji hao wanaosakata soka nchi za nje kwa miaka mingi ambapo kila mwaka wanazidi kuzaliwa vijana wakiwa na skills zilezile au zaidi kuliko wale waliopita kutokana na mipango mizuri.

Kiongozi huyo wa O.F.A alisema kutokana na sheria za nchi ya Tanzania kutowaruhusu raia wake wanaoishi nje ya nchi wenye raia mbili kutotumika na kunufaika kama nchi nyingi za Africa na zile za South America zinavyofanya hakuna budi TFF kutumia mpango muafaka ili kuweza kuwatumia wachezaji vijana nchini kwenda nje kusakata soka ya kulipwa sambamba na nyota wa dunia ili kuwajengea misingi mzuri ya kiuchezaji na kuwaondoshea woga pale wanapokutana na wachezaji ambao wamezowea kuwaona katika TV tu katika timu wanazoshabikia wachezaji hao wa Tanzania za barani ulaya.

Alitoa mfano kwa kusema kwa sasa Tanzania ilitakiwa wawe mabingwa wa bara la Africa karibu mara zote kwa wachezaji wanaochezea nchini mwao CHAN michuano ambayo hata hivyo Tanzania inashindwa kufanya chochote cha maana ukilinganisha na nchi nyingine za Africa,
kama CHAN inashindikana,nadhani kusiwe na ndoto za kuzifunga nchi zenye nyota wanangára barani ulaya katika michuano mbalimbali.

Kama mchezaji amezowea kumuona Drogba,Eto'o,Essien,Yaya Touré katika Tv,leo ghafla anamkuta anatakiwa amkalie huku nyota huyo akiwa anashirikiana na wenzake kadhaa ambao wanatamba barani ulaya ,nadhani mchezaji wa Tanzania pamoja na uzuri wake atajaribu tu yeye na wenzake lakini nadhani mioyo itaaanza kuwadunda kabla ya kuanza pambano hadi mwisho wa dakika zote huku wapinzani wao wakicheza kwa kujiamini kuwa hawaogopi chochote kutoka kwa wapinzani wao wa Tanzania kitu ambacho kujiamini ni msingi mkubwa wa mafanikio na maendeleo ya soka kwa kila mchezaji,timu au nchi,bila ya kujiamini usitegemee matarajio yoyote ,alisema kiongozi huyo anayeishi mji wa Seville na mpenzi mkubwa wa F.c Barçelona.

Aliendelea kutoa mfano kwa kusema,kwa mara ya mwisho Tanzania iliingia katika fainali za kombe la Mataifa huru ya Africa Caf Nations Cup miaka ya 80 wakati huo walikuwepo Akina Tenga,Adolph Richard,Tino na wengineo hio ilikuwa ni bahati nzuri kwa Tanzania kwani kipindi hicho nchi za Africa wachezaji wao wote walikuwa wakichezea katika nchi zao kama Tanzania ilivyo sasa, aidha nchi hizo zilikuwa na mchezaji mmoja au wawili tu nje kinyume na soka la leo kikosi cha wachezaji 30 wote wanacheza soka barani ulaya na hawana matatizo ya malipo ya mishahara yao kwahio huleta utulivu kwa wachezaji hao na kuwafanya kujikita zaidi katika kazi yao ya soka.

Mbinu ambazo Pereira imeisomesha TFF ni kukitaka chama hicho cha soka nchini kuwa na mpango maalum wa kuweza kuiwezesha Tanzania kukuza soka na kuwa sawa sawa na nchi nyingine za Africa kutokana na nchi hio kuwa na vipaji vingi sawa na nchi nyingine yoyote ya Africa au Brasil, alisema kuwa na mpango mkubwa wa kutayarisha mechi za kirafiki za timu ya Taifa ya A na zile za vijana wa nchi hio, Mechi hizo za kirafiki zisiwe za kushitukizia tu kama ambavyo imezoeleka hadi dakika ya mwisho ndio TFF inakuwa inahangaika kutafuta kucheza mechi zao za kirafiki na mwisho kuangukia kucheza na Kenya au Uganda nchi ambazo kama utahesabu mechi walizocheza nazo za kirafiki na zile za challenge cup pengine zinafikia zaidi ya 50 katika historia zao, huwezi kucheza na Kenya au Uganda tu kila mara alisema kiongozi huyo,

Ukiangalia katika maendeleo ya soka katika bara la Africa ,nchi za Africa Mashariki na Kati ni nchi ambazo zipo nyuma sana kisoka kulingana na nchi za ukanda mwingine wowote wa bara hilo,kama unaagizia mechi ya kirafiki dakika za mwisho dhidi ya somalia ,hata ukishinda goli 10-0 nadhani hakutokuwa na maendeleo yoyote ambayo wachezaji watakuwa wamejiongezea kisoka na pengine ni bora kufanya mazoezi ye Taifa yanakuwa na pinzani zaidi ya kucheza mechi hio ya kirafiki kwa hio hupelekea matokeo ni sawa na kujirejesha nyuma kihatua baada ya kwenda mbele kisoka.

Katika mpango mkubwa wa kufuatilia mechi za kirafiki inabidi TFF iandike barua mapema kwa nchi wanazotaka kucheza nazo mapango huo wanaweza kuagiza mechi zao zote zilizokuwa katika kalenda ya fifa kwa muda wa miaka 2 na kuwa na uhakika ya tarehe zao na nchi ambazo watacheza nazo na sio kushitukizia tu au mara nyingi kukosa kucheza mechi hizo kwa vile inakuwa ni muda umepita.

Mpango huo wa kuagizia nchi za kucheza nazo utakwenda sambamba na kuuza wachezaji wa Tanzania nje kwa muda huo wa miaka 2 ambapo Tanzania itaweza kujivunia si chini ya nyota 10 hadi 15 watakaopata kucheza soka ya kulipwa barani ulaya kutokana na kuonekanwa na timu,makocha,maagents,na scouting mbalimbali wa bara hilo la ulaya ambapo vijana hao wa taifa ndio watakaoanza safari ya Tanzania kuelekea katika maendeleo ya soka duniani.

Alisema katika mpango huo TFF inahitajika iombe mechi za kirafiki kwa muda mrefu ujao ili kuweka uhakika mpango wa kuuza wachezaji wake unakwenda sambamba na huo muda wote wa miaka 2.kwa mfano:
1)Tanzania inatakiwa icheza mechi nyingi za kirafiki na timu za taifa za nchi zilizochoka kisoka barani ulaya ili kuwatangaza wachezaji hao katika nchi hizo na nyinginezo za bara hilo kama njia ya kwanza ya kuwatangaza vijana wake katika njia ya kuelekea kucheza soka barani ulaya,kuna nchi nyingi ambazo Tanzania inazo uwezo wa kucheza nazo na pia kuzifunga na kuwafanya vijana wake kuonekana ubora wao kisoka kabla ya kuanza kuagizia nchi zilizo katikati kisoka hapo baadae,
Nchi kama:
Faroe Islands,Moldova,Luxembourg,Liechtenstein,Kazakhstan,Tajikistan,Azerbaijan na nyinginezo ni nchi ambazo Tanzania inaweza kucheza nazo na kufanya vizuri na huku ikielekeza kuwatangaza wachezaji wake kuonekana katika timu za bara hilo la ulaya.

2)Baada ya mpango huo wa kwanza kuwe na mpango mwingine badala ya mpango huu wa sasa wa kucheza mechi nyingi za kirafiki katika kiwanja cha nyumbani cha Taifa,hivi sasa TFf inahitajika ibadilike kuomba mechi zake za kirafiki dhidi ya nchi za bara la Africa lakini mechi zao hizo zichezewa barani ulaya ujanja ambao hivi sasa unatumiwa na nchi zote za bara hilo zilizo juu kisoka,nchi kama Ghana wanacheza mechi nyingi nchini England,RD Congo wanawatangaza wachezaji wao wa nyumbani kwa kucheza mechi nyingi za kirafiki nchini Belgium,Senegal na nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa zinacheza mechi nyingi nchini france,hivyo ni rahisi kwa TFF kuagizia mechi kwa nchi za Africa na kutumia viwanja vya ulaya ambavyo nchi hizo ndio wanavyovitumia hivyo kutatoa nafasi kubwa kuwatangaza wachezaji wa Tanzania bara zima la Ulaya kwa kushirikia na mpango wa kucheza na timu zilizopo katika viwango vya chini vya bara hilo.

Mipango hio miwili itaweza ndani ya miaka 2 kuwatoa woga wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania pamoja na kuwapatia nafasi ya kuonekanwa na kuuzwa kirahisi kulikoni kusubiri kuwa kuna siku Tanzania itaweza kufanya vizuri kwani inaonekana kila siku inazidi kuporomoka huku nchi za Africa kila siku zikizidi kujiimarisha kisoka.
Aidha alisema ni lazima wachezaji Vijana nchini wapatiwe nafasi za kucheza mara kwa katika vikosi vya kwanza vya timu za Primier Leauge ili kuwajenga vijana hao kujiamini na sio kusubiri kucheza katika timu ya taifa ya vijana tu au kufanya mazoezi tu bila ya mashindano ya maana.
Ni lazima kuwe na mpango maalum wa mchezaji wa taifa ya vijana U23 waweze kucheza mechi nyingi za ligi kuu kitu kitakachowasaidia katika kujijenga kisoka.

Alimalizia kwa kusema TFF isimamie kuhakikisha timu zote za Primier League,First Div,na Sec div zinakuwa na timu ndogo za kudumu ambazo zinashiriki katika mashindano ya ligi ya madaraja mbambali nchini nchi kama nchi zote duniani zinavyofanya ili kuwajenga wachezaji hao na sio kucheza mechi za kirafiki tu mwaka mzima au kusubiri Uhai cup kwa timu za mprimier league mashindano yanayodumu wiki chache tu kitu ambacho kinaua viwango vya wachezaji hao.
Kama wachezaji hao watashiriki michuano ya soka ya madaraja mbali mbali nchini viwango vyao vitakuwa sana na pia vilabu vitanufaika na mfumo wa uchezaji wake kutokea chini hivyo kupelekea mchezaji kufundishika zaidi na mfumo wa klabu na kujua ni uchezaji wa aina gani amefundhiswa na anatakiwa kuutumia akiwa katika timu A ya klabu hio ,
itapelekea sio tu pamoja na nidhamu ya hali ya juu bali pia vilabu kujiokoa na kugharimu fedha nyingi za kusajili wachezaji kutoka nje na vilabu vingine vya nchini ambapo kiongozi huyo amepigia mfano wa mfumo huo wa vilabu vya kuwa na tamaa"labda"huyo mchezaji atakuwa na uwezo kama walivyomuona katika klabu aliyotoka ambapo mfumo wake na pengine nidhamu ni tofauti kabisa na atakaokutananao katika vilabu vyao vipya vya Primier Leuague ya Tanzania.
TFF inabidi tu kutoviruhusu vilabu hivyo B timu zao kupanda hadi Primier League kwani kaka zao A tayari wako huko lakini first div wanaweza kucheza kwani hapo mchezaji atawiva tayari kwa kuja kuchezea timu kubwa ya klabu hio pamoja na timu za Taifa za Vijana Tanzania,Huku akitoa mfano wa timu yake anayoipenda kwa kusema "unaona kwa mfano kama Barça B".