

















Katika michuano hio Oranje Football Academy yenye kikosi kinachoundwa na vijana wenye vipaji vya hali ya juu chini ya miaka 20 walinyakua ubingwa huo baada ya kushinda mechi zote tatu dhidi ya wapinzani wake katika fainali hizo.
Katika pambano la kwanza O.F.A iliweza kuifunga Children Soccer Stars ya Pemba jumla ya mabao 2-1 kabla ya kuichapa Fairmount ya Unguja bao 1-0 na kuitwanga Okapi ya Pemba mabao 7-0 katika pambano la mwisho lililofanyika katika uwanja wa Gombani na Kutwaa Ubingwa wa msimu wa 2011.