WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday 6 June 2012

Zanzibar yatoa adhabu Kombe la Dunia


TIMU ya Taifa Zanzibar (Zanzibar heroes)imeanza vizuri michuano ya Kombe la Dunia ya nchi zisizo wanachama wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni(Fifa) baada ya kuizabua timu ya Ratia mabao 6-0.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari Chama cha Soka Zanzibar(ZFA), Munir Zakaria mabao ya Zanzibar Heroes yalikwamishwa na winga Hamis Mcha aliyepiga 'hat trick' katika dakika za 33, 41 na 72.

Mabo mengine yalifungwa na kiungo Abdi Kasim 'Babi' katika dakika ya 51 na Amir Juma aliyekwamisha mawili katika dakika ya 88 na 90.

Zacharia alisema baada ya ushindi huo Zanzibar itashuka tena dimbani leo kwenye Uwanja wa Erbil kuvaana na Tamil Eelam likiwa ni pambano la kukamilisha hatua ya makundi.

Ushindi dhidi ya Ratia una maana kwamba, sare yoyote leo hii, itaivusha kucheza hatua ya nusu fainali.Katika hatua nyingine, Zacharia alisema Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Alu Mabrouk ameahidi kuizawadia timu Heroes Sh18 milioni iwapo watafanikiwa kutwaa ubingwa, na Sh9 milioni wakishika nafasi ya pili.