WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Tuesday, 1 November 2016

AZAM YOUTH ACADEMY KUSAKA VIPAJI ZANZIBAR WIKI HII


VIJANA 12 kutoka mikoa ya Morogoro na Dodoma wamechaguliwa kwenye mchujo wa kusaka wanasoka chipukizi wa umri chini ya miaka 17 (U-17) ulioratibiwa na klabu ya Azam FC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jana.

Zoezi hilo linalosimamiwa na Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Muingereza Tom Legg, lilihusisha vijana 528 huku 32 kati ya hao wakiingia fainali kabla ya kuchujwa na kupatikana waliobora zaidi 12.

Vijana hao 12 wanafanya idadi kamili ya vipaji vilivyochaguliwa kwenye mchujo wa awali kufikia 37 kati ya vipaji 2,073 vilivyofanyiwa usaili, wengine wakipatikana mikoa miwili ya awali ya Dar es Salaam na Tanga.

Wikiendi hii zoezi hilo la kusaka vipaji litaendelea tena kwa kufanyika Kisiwani Unguja, Zanzibar ndani ya Uwanja wa Amaan, Jumamosi ijayo Novemba 5 kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 9.00 Alasiri.

Kwa vijana waliozaliwa kati ya mwaka 2000, 2001 au 2002 waishio Zanzibar katika Visiwa vya Unguja na Pemba, wanaombwa kufika kwenye majaribio hayo ya sita kufanyika.

"Tafadhali unaombwa kufika na nakala ya cheti chako cha kuzaliwa kwa wale wote watakaokuja kwenye majaribio hayo,"imesema taarifa ya Azam na kuongeza; "Kwa majaribio mengine ya wazi kuhusu sehemu, tarehe na muda, tutawatangazia hivi karibuni,".