Kutokana na mambo ya kutojielewa Tanzania imekuwa ikipoteza nafasi zao hizo 4 na kujikuta ikibakiwa na nafasi ambazo zinawakilishwa na timu za Tanzania Bara huku ikisahau zile nafasi mbili za Zanzibar kuwa ni nafasi nyingine mbili za ziada za Tanzania.
Kutokana na ratiba za michuano hio nadhani unaweza kugundua kwamba timu za Tanzania Bara hupata wakati mgumu sana katika ratiba zao kwa kuangukia mara nyingi katika timu za nchi za Afrika kaskazini huku timu za upande wa Zanzibar zikianza mara nyingi na nchi tofauti za kusini mwa Afrika, kutokana na udhaifu au mfumo mbovu wa mashindano ya ligi ya Zanzibar inazifanya timu zake kuyaaga mara moja tu baada ya kucheza mechi zao za awali za nyumbani na ugenini hivyo Tanzania katika hali ya kutojitambua imekuwa ikipoteza timu mbili kila mwaka za Zanzibar katika hatua za mechi zao za kwanza kabisa hivyo kubakiwa na timu mbili za Bara ambazo kwa bahati mbaya nazo mara huangukia mikononi mwa Waarabu na kuanza tena stori hio miaka yote.
Kutokana na kutojitambua huko Tanzania inabakia kuwakilishwa kiakili na timu 2 yaani mbili kutoka Tanzania Bara, na pia timu mbili Tanzania Visiwani hapo nikimaanisha hakuna Muungano katika soka la umoja ambao unahusisha mikakati ya kuziboresha timu za pande mbili na kukomaa katika mshindano yaho makubwa barani Afrika kwa vilabu hivyo kubaki kila upande na timu mbili kivyake.
Muda umefika kwa viongozi wa pande mbili Bara na Visiwani kuanza mikakati mipya ili timu 4 ambazo ni nafasi nyingi kwa Tanzania kuweza kuzifanyia usahihi na kuwa na wawakilishi bora barani Afrika.
Kama nchi za Zambia zina wawakilishi 2 na kufika mbali katika mashindano ya Afrika ni wakati wa Tanzania yenye timu 4 kufika mbali zaidi kuliko timu hizo mfano waa kama Zambia.
Tunaomba viongozi wahusika wa pande zote mbili kukaa pamoja na KU-fix matatizo madogo madogo ili kuinua kiwango cha Soka nchini, Soka ni Ajira kubwa duniani kote hivyo Viongozi wahusika wasiendelee kuzorotesha Ajira za vijana na watu wengi nchini, huu ni muda muwafaka na kuanza teza hii kazi iliyozorota kwa miaka mingi.