WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 16 May 2009

MAXIMO AUNGA MKONO STARS KUCHEZA USIKU

Aunga mkono Stars kucheza usiku

Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo, ameunga mkono maoni ya baadhi ya wadau wa soka nchini wanaotaka mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya New Zealand kuchezwa usiku ili kuepuka kukosa mashabiki katika mchezo huo utakaochezwa Juni 3, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini, Dar es Salaam.

Maoni hayo yamekuja kufuatia Stars kupata mashabiki kiduchu kwenye mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Mabingwa wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (CHAN), uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa Stars kulala 2-0, ulishuhudiwa na jumla ya mashabiki 10,408.

Juzi baadhi ya wadau wa soka kama Sudi Tall, Juma Omari, George Msangi na Thomas Mdeka, waliishauri kuwa ili Stars kupata mashabiki wengi kwenye mchezo wake na New Zealand ni vema kama mchezo huo utachezwa usiku.

Akiunga mkono kauli hiyo, Maximo, alisema kuwa itakuwa ni vema kama mchezo huo utaanza kuchezwa saa 12 jioni kwani utatoa nafasi kwa watu wengi kujitokeza kushuhudia kutokana na siku hiyo kuwa siku ya kazi.

Alisema kuwa anaamini kila Mtanzania napenda kushuhudia timu yake ikicheza lakini kuna uwezekano mashabiki wakajitokeza kidogo kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kazi.
Maximo alisema kuwa yuko tayari hata kucheza muda wowote utakaopangwa, ambapo jukumu lake ni kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Kwa upande wake Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Frolian Kaijage, alisema kuwa mawazo ya mchezo huo kuchezwa usiku si mabaya, ambapo TFF itajaribu kuyafanyia kazi kwani utaratibu wa kufanikisha suala hilo uko mikononi mwa kamati inayoshughulika na uwanja huo.
-------------------------------------------------------------------------------------------------