WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday, 20 May 2009

NEW ZEALAND YATAKA MECHI NA STARS IRUSHWE MOJA KWA MOJA

WAGENI wa Taifa Stars, New Zealand wametaka mechi baina ya timu hizo irushwe hewani laivu kati ya saa 12 jioni au 1.00 usiku kwa lengo la kuitangaza Tanzania nje ukiwamo pia Uwanja wa Taifa nchini kwao.
Wakati hilo lilifanyika, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio katika mchezo huo kuwa ni Sh40,000 kwa kiwango cha juu na cha chini kikiwa Sh 3,000.
Viingilio vingine, kulingana na TFF ni Sh 5,000 kwa mzunguko rangi ya bluu, Sh10,000 kwa jukwaa la rangi ya machungwa nyuma ya magoli na Sh15,000, rangi ya machungwa mkabala na jukwaa kuu wakati VIP C Sh20,000 na VIP B itakuwa Sh 30,000.
Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa wamekuwa wakiwasiliana na timu hiyo itakayotua nchini ikiwa njiani kwenda Afrika Kusini kushiriki michuano ya Kombe la Mabingwa wa Mabara.
"Kwa kuona umuhimu wa ombi hilo la New Zealand, tumeamua mechi hiyo ichezwe jioni na tayari tumeshaitaarifu serikali kuomba tutumie uwanja huo usiku.
"Pia, tumeona itakuwa ni vizuri kucheza usiku kwa vile itakuwa siku ya kazi na kuwapa nafasi watu wote hata walioko kazini kuishuhudia mechi hiyo," alisema.
Aliongeza kuwa kikosi hicho cha New Zealand kitatua nchini Juni Mosi kikiwa na wachezaji 23 na viongozi 11 na tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa Jumatatu katika vituo vyote vilivyozoeleka.
"Mechi hiyo ni kubwa kwao na tena ni kama changamoto kwetu TFF, kuandaa mechi kubwa kama hiyo, hivyo tutahakikisha tunawapa maandalizi mazuri ili wawe ni mabalozi wakuu katika kuitangaza nchi yetu kiutalii na kupata timu mbalimbali za nje ambazo zitacheza mechi nyingi nchini," aliongeza.
Alisema timu hiyo inayokuja ni mabingwa wa Oceania na wanajiandaa kushiriki Kombe la Mabara yatakayofanyika Juni 14 - 28 nchini Afrika Kusini.
Alisema mchezo huo ni muhimu kwa Stars kwa kuwa ni fursa kwa timu hiyo kujipima vilivyo dhidi ya timu hiyo kubwa inayowakilisha bara na kuwaonyesha wapenzi wa mchezo huo nchini kuwa yale yaliyotokea katika mechezo iliyopita yalikuwa ni matokeo ya soka, hivyo imejipanga kuwapa raha.
Aliongeza kuwa kabla ya mechi hiyo ambayo itakuwa usiku , pia kutakuwa na wasanii mbalimbali ambao watakaokuwa wanatumbuiza ili kuleta hamasa katika mechi hiyo.
Taifa Stars inaingia kambini leo ikiwa na wachezaji 27 tayari kwa maandalizi ya mechi hiyo ya kirafiki.
-------------------------------------------------------------------------------------------------