WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Wednesday 20 May 2009

STARS KUKIPIGA USIKU DHIDI YA NEW ZEALAND

Mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na ile ya New Zealand uliopangwa kufanyika Juni 3 mwaka huu Dar es Salaam, utachezwa usiku kutokana na ombi la wageni hao.Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema Dar es Salaam jana kuwa, New Zealand wameomba mchezo huo ufanyike kuanzia saa moja usiku kutokana na sababu ya hali ya hewa, kwani muda wa alasiri ambao mchezo huo ulipangwa kufanyika jua linakuwa bado kali. Lakini pia alisema licha ya hali ya hewa, TFF iliona muda huo utakuwa mwafaka kwani mechi hiyo itachezwa katikati ya wiki, ambayo ni siku ya kazi, hivyo kama ukichezwa usiku mashabiki wengi watajitokeza baada ya kutoka katika shughuli zao. Kwa mujibu wa Mwakalebela msafara wa New Zealand utakuwa na watu 34 kati yao 23 wakiwa ni wachezaji na mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. “ New Zealand ambao wanakuja nchini wakiwa njiani kwenda Afrika Kusini kushiriki michuano ya Kombe la Mabara (Confederations Cup) yatakayoanza kutimua vumbi Juni 14-28 wanakuja na wachezaji wao mahiri, akiwemo nahodha wao Ryan Nelsen anayechezea timu ya Blackburn Rovers inayoshiriki Ligi Kuu ya England na wachezaji wengine, ambao wako kwenye ligi za Scotland, Marekani na Australia, ” alisema Mwakalebela. Mwakalebela alisema mchezo huo wa Stars na New Zealand ni muhimu kwa Tanzania kwani ni fursa nyingine kwa Stars kujipima uwezo dhidi ya timu kubwa na pia kutangaza uwanja huo wa mpya wa Taifa kwa ajili ya kuuza nje, ili uweze kupata timu za kufanyia mazoezi, wakati wa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini mwakani. “ Tumejipanga kutumia mchezo huo na New Zealand vizuri, ili nchi hiyo iweze kutuuza kwa mataifa mengine kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa katika mchezo huo, ambao wageni wetu wanatarajia kurusha mchezo huo kwenye televisheni moja kwa moja kwao,” alisema Mwakalebela. TFF imesema maandalizi ya mechi yameshaanza na viingilio katika mchezo huo vitakuwa Sh 3,000, Sh 5,000, Sh 10,000, Sh 15,000, Sh 20,000, Sh 30,000, Sh 40,000.
-------------------------------------------------------------------------------------------------