WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 19 July 2009

ORANJE FOOTBALL ACADEMY YATOA PONGEZI KWA MABINGWA WA COPA COCA COLA

-------------------------------------------------------------------------------------------------
------------------------------------------------------------------------------------------------- Kwaniaba ya viongozi,wachezaji,na wapenzi wote wa ORANJE FOOTBALL ACADEMY wanatoa pongezi kwa timu ya mkoa ya mjini magharibi kwa kutwaa ubingwa wa copa coca cola kwa vijana wenye umri wa miaka 17, Oranje Football Academy ni moja ya timu za vijana ambao wanaiwakilisha mkoa huo wa mjini magharibi ambapo wachezaji wake wawili wapo katika kikosi hicho cha mabingwa hao wapya wa copa coca cola,
akiongea na mtandao unaomilikiwa na academy hio katibu mkuu wa O.F.A Hussien alisema" Academy ya O.F.A inawapongeza vijana hao kwa kutwaa ubingwa huo msimu huu na kuonyesha soka ya kuvutia ambapo vijana hao walionyesha vipaji vyao ambavyo ni hazina kubwa kwa taifa siku za baadae" aidha aliipongeza "timu ya mkoa wa Tabora kwa kuwa ni timu iliyoonyesha kiwango kizuri cha soka katika mashindano hayo",aliongeza kwa kuzipongeza timu zote za vijana zilizoshiriki katika mashindano hayo ambayo yameonyesha Tanzania kuwa na hazina kubwa ya vijana wenye vipaji nchini,na kupoteza kwa mikoa mingine kufikia fainali ni moja ya mchezo wa soka ambapo ni timu mbili tu ndizo zinahitajika kuingia fainali lakini kwa ujumla timu zote zilikuwa nzuri sana na vijana wanahitaji kutunzwa na kuendelezwa kwa juhudi zote kwa manufaa ya taifa hapo baadae, aliongeza katibu huyo kwa kusema" wakati umefika kwa makampuni mingine kuiga mfano wa kampuni ya coca cola kwa kuweza kuwasaidia vijana hapa nchini kwa lengo la kuipandisha nchi yetu katika ramani ya soka duniani"
-------------------------------------------------------------------------------------------------
COPA COCA COLA 2009 YAONYESHA TAIFA KUWA NA VIJANA NYOTA WA SOKA:
Michuano ya copa Coca cola ikiwa imemalizika na timu ya mjini magharibi ikiwa imetwaa ufalme mwaka huu 2009,ambapo vipaji mbali mbali vilijitokeza na kuonyesha uwezo wa hali ya juu kwenye michuano hio,kutokana na mashindano hayo Tanzania imefanikiwa kupata mwanga kwa wachezaji chipukizi wenye uwezo na ndio wenye nafasi ya kuunda kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania.
Timu ya mjini magharibi kutwaa ubingwa huo ilikuwa ni matarajio makubwa kutoka kwa wapenzi wote wa soka kulingana na kiwango cha hali ya juu kilichoonyeshwa na chipukizi hao kuanzia hatua ya makundi hadi ya mtoano,
ikiwa ni Timu pekee kutoka kisiwani Zanzibar iliyofanikiwa kuingia robo fainali ya michuano hio,ilifanikiwa kuzifunga karibu timu zote ilizokutana nazo na kufikisha idadi ya magoli 27.
Katika michuano hio Lindi ni timu pekee ambayo ilishindwa kuifunga au kutoka sare na timu zote ilizokutana nazo na kuondoka bila ya kuwa na pointi yoyote katika mchuano hio,
Timu zote zilionyesha kiwango kizuri katika mashindano hayo ambacho hakikutarajiwa na viongozi wa soka nchini pamoja na watazamaji wote kwa ujumla waliokuwa wakifatilia michuano hio,
pamoja na viwango vizuri ,vijana walionekana kuwa na maumbile makubwa yenye kuvutia ambayo ndiyo yanayotakiwa kwa wachezaji ambao hasa katika soka ya kulipwa kama wakiendelezwa vizuri na kutunzwa.
Hali ilijionyesha kuwa Tanzania ina hazina kubwa ya vijana wenye uwezo wa hali ya juu katika soka,sawa na mataifa mengine ,kama brasil,na west africa kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuwaweka chipukizi hao kama wanavyofanya wenzetu walioendelea kisoka,na hii itaweza kutoa nyota wengi kwenda kucheza soka ya kulipwa nje na kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zitakazotisha kisoka sio tu ukanda wa Africa bali duniani kwa ujumla.
Katika michuano hio jumla ya magoli 343 yalipachikwa wavuni na vijana hao tokea kuanza hadi kumalizika kwa michuano hio,kati ya magoli hayo vijana 7 walifanikiwa kupachika jumla ya magoli 3 kila mmoja kwa mchezo mmoja, hii ni moja ya kitu cha kujivunia kwa taifa kuwa na washambuliji vijana kama hao wenye uwezo na uchu wa kupachika mabao kimiani.
Mgeni rasmi wa kufunga michuano hio ya mwaka huu 2009 waziri wa habari,utamaduni na michezo George mkuchika aliiomba Serikali, Tff na kampuni hio ya coca cola kuongeza mkataba mwingine kwaajili ya kuendleza michuano hio kwa vijana ambao ni manufaa ya Taifa.
Nchi za Africa ya kusini,Zimbabwe,Msumbiji,Ethiopia,Kenya,Zambia,Uganda,na angola zimefaidika kwa kuuza wachezaji nje kutokana na michuano kama hio ambapo nchi kama brasil,argentine ikiwa ndio vinara wa kutoa wachezaji katika michuano kama hio kwa vijana wao kuonekanwa na vilabu mbali mbali, nyota wa zamani wa Argentine Diego Maradonna alianza kuingárisha nyota yake katika michuano kama hio ya coca cola cup na kumfikisha kuwa nyota ya dunia wakati wake.
Naye kocha wa mjini magharibi Juma Abdulrabi alisema"Kikosi hicho kimejengeka kulingana na juhudi ambazo zilionyeshwa na uongozi mzima wa mkoa huo hasa kwa kuwajali vijana kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwaajili ya kukamilsha azma yao ya ubingwa na kilikaa kambini kwa muda wa miezi wiwili tu."
Michuano ya mwaka huu ya copa coca cola ilianza juni 28 na kumalizika fainali julai 18,ambapo Rais wa Jakaya Kikwete alihudhuria fainali hio alitaka vile vile michuano hio kuendelezwa kwaajili ya manufaa ya taifa hapo baadae.
Leo O.F.A wanacheza mechi ya kirafiki na viongozi wa O.f.A.
-------------------------------------------------------------------------------------------------