
Mchezaji Chipukizi wa Oranje Football academy seif Abdalla(jezi kijani) amechaguliwa katika timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania U-17 inayokwenda Khartoum-Sudan katika michuano ya Challenge Cup u-17, kijana huyo mwenye uwezo mkubwa wa kusakata soka amechaguliwa katika mchujo wa mwisho ambapo ametangazwa kuwa katika kikosi cha nyota 20 wanaounda kikosi hicho cha U-17, kwa niaba ya O.F.A inamtakia mafanikio mazuri akiwa huko Sudan ambapo mbali na kuwa ni jukumu kwa Taifa bali pia atakuwa ni Balozi mzuri wa O.F.A





