WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 31 January 2010

RIVALDINHO AENDELEA KUNYANYASA MABEKI

Nyota wa Kimataifa Rivaldo anaendelea kutingisa nyavu za timu pinzani pamoja na kunyanyasa mabeki wa timu hizo anazokutana nazo kila wanapocheza.
Nyota huyo ambae amepatiwa nafasi hiyo na Oranje Football Academy amezoa umaarufu mkubwa katika mji wa Belfast nchini Nothern Ireland kutokana na staili zake za kuwachomoka mabeki wa timu pinzani kirahisi jinsi anavyotaka kutokana na mbinu zake za hali ya juu za kumili na kuusanifu mpira hasa kwa mguu wake wa kushoto ambao ndio zaidi anaotumia katika kuwanyanyasa mabeki hao.
Kutokana na uwezo wake mkubwa na uzuri wa mabao yake ambapo mara nyingi huwatoka mabeki kwa stail za aina yake ikiwemo mikwaju ya mbali inayomfanya kuwafunga makipa mbalimbali imemzolea sifa nyingi katika mji huo wa Belfast.
Baada ya kiongozi wetu wa Oranje Football Academy kumtembelea mwezi uliopita mjini Beelfast alijionea jinsi watu mbalimbali wanavyompa heshima Rivaldo popote anapopita pamoja na kumsifia sana kwa usanifu wake wa mpira kiwanjani.
Kutokana na uchezaji wake wa stail ya aina yake na ufungaji wake tayari vilabu mbalimbali vinapigana vikumbo kumwania nyota huyo kujiunga na timu zao,ambapo hadi havi sasa kuna malumbano makubwa kati ya timu ya Rivaldo ya Bangor F.C na klabu ya Lisbun ya primier league ya Nothern Ireland ambao wamemshawishi Rivaldo kujiunga na timu yao kosa ambalo limepelekea uhasama mkubwa kati ya vilabu hivyo viwili.
Klabu ya Bangor tayari imedai kulipwa faini na timu ya Lisbun ambao wamemshawishi Rivaldo bila ya kupitia katika sheria za kukutana na viongozi wa Bangor pamoja na Agent wake.
katika siku mbili zijazo viongozi wa Oranje Football Academy ambao ndio wasimamizi wa Rivaldo watakutana na viongozi wa Bangor pamoja na viongozi wa Lisbun ili kuweza kupata usuluhishi wa nyota huyo.
Katika maongezi hayo ni pamoja na kuitaka klabu ya Bagor kumruhusu Rivaldo kujiunga na Lisbun ambapo nafasi yake itazibwa na nyota chipukizi wa timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania ambae jina lake litajwa hapo baadae mara baada ya kila kitu kukamilika.
.........................................................................................................................................................................