Katika uchaguzi ambao huamuliwa kwa kura kutoka kwa makocha Mkuu au Wakurugenzi wa Vyama vya Ufundi ya Taifa inayoongozwa na CAF. Toure alisema"Nina furaha sana kushinda tuzo. Najisikia fahari ya siku hii maalum. Naishukuru familia yangu, mke na watoto kwa msaada wao.Pia namshukuru ndugu yangu (Kolo Toure), wachezaji wenzangu wa (Club na timu ya taifa) na Shirikisho la Soka la Ivory Coast kwa mchango wao ,alisema Toure mwenye umri wa miaka 28 akiwa na baadhi ya marafiki na familia wanaoonekana kuwa na furaha kubwa kwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora katika bara la Africa katikati ya nyota wengine wengi.
Toure aliongeza kwa kusema"Ilikuwa si rahisi kushinda tuzo hii. Hii ni hatua ya kwanza katika kazi yangu. Ni tuzo muhimu sana kwa ajili yangu na shukurani kubwa kwa wafanyakazi wenzangu. Kwangu mimi hii ni tuzo ya juu katika kazi yangu".