WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Tuesday, 10 January 2012

IVORY COAST "TEMBO" YATANGAZA KIKOSI KIZITO

Ivory Coast imetangaza kikosi kizito ambacho tayari kimeanza kambi rasmi nchini Abu Dhabi ambapo itakuwepo kuko kwa siku 14 kabla ya kuelekea katika michuano ya Caf Orange Nations Cup.
wakiwa nchini Abu Dhabi "Elephant" watacheza mechi mbili za kirafiki kujiandaa na michuano hio mikubwa ya barani Africa ambapo watacheza dhidi ya Lebanon na Tunisia.

Kikosi hicho cha Ivory Coast safari hii kitakuwa na nyota ambae yuko katika "form" Wilfried Boni (Vitesse Arnhem, Netherlands), ambae ataonekana kwa mara ya kwanza kwa wapenzi wa soka katika kikosi hicho.Boni kwa sasa ni mshambuliaji bora wa kati sio tu kwa timu yake ya Vitesse-Arnhem bali ni mshambuliaji bora kwa timu zote za holland nchi inayosifika kwa kutoa nyota ambao hungára baadae katika nchi mbalimbali duniani wakiwemo nyota kama,romario na ronaldo ambao walianzia PSV-Eindhoven,Ibrahimovic-Ajax-Amsterdam,Larson-Feyanoord-Rotterdam,Nwanko Kanu-Ajax,Finidi George-Vitesse-Arnhem,Tijani Babangida-Ajax.Gudjenson-Feyanoord na wengine wengi.

kutokana na uwezo mkumbwa Wilfred Boni wa kumiliki mpira,skills,technics,na ufungaji bora na utoaji wa pasi safi za kumalizia kwa wenzake nyota huyo mpya Boni ambae ametokea nchini Russia alikokuwa akicheza soka ya kulipwa na kujiunga na timu hio ya Arnhem ambayo imenunuliwa na kumilikiwa na millionea kutoka Russia Jordanio na tayari makocha na wataalamu wa soka kutoka nchini holland wamemfananisha na kummwagia sifa Boni kuwa uwezo wake kisoka ni mkubwa sana na ana uwezo wa kuchezea timu yoyote duniani kama mshambuliaji wa kati ambapo wamemfananisha uwezo wake na ule wa Romario wa Brasil alipoanza kuichezea timu ya PSV-Eindhoven.

Millionea huyo wa Vitesse-Arhem Jordanio ambae ni rafiki mkubwa wa mmiliki wa Chelsea ya England Roman Abramovic tayari ana kikosi ambacho kimesheheni nyota wa kimataifa wenye umri kati ya miaka 18 hadi 22 ambao wanachezea timu za taifa mbalimbali duniani kati yao wapo mapacha wawili kutoka Brasil kutoka klabu ya Flamingo wanaochezea pia timu ya ya taifa ya U18 ya Brasil,ambapo pia yupo kiungo mkali kutoka Ghana Anthony Annan Koffi ambae aliichezea timu hio ya taifa katika mashindano ya kombe la Dunia nchini South Africa 2010.

Pia kutokana na maelezo ya kiongozi wetu wa O.F.A anaeishi mji wa Arnhem amemtaja Boni kuwa ni mshambuliaji wa kati mwenye akili na uwezo mkubwa wa kumiliki mipira na uwezo mkubwa wa kufunga na kutoa pasi uwezo ambao wachezaji wengi wa kati duniani kwa sasa ni adimu kupatiaka"kwani wengi wao wanakuwa na woga wakiwa na mpira katia maeneo ya hatari tofauti na boni anazidi kuwa mtulivu anapokuwa katika maeneo hayo na kutumia mahesabu kama mchezaji wa drafti-dama".
aliongeza kwa kusema Wilfred Boni ni mchezaji ambae mabeki kama watakuwa na papara ya kunyangánya mpira inakuwa ni vigumu sana kwani yeye mara zote anakuwa na akili na ujanja wa hali ya juu na nafasi ya beki kuuchukua mpira katika miliki ya Boni "ni sawa na nafasi ndogo ya kuupanda mbuyu kwa kutumia kifua inakuwa ni vigumu sana"
huku akimlinganisha na marehemu majidi musisi wa Uganda Cranes katika kudhibiti na kuficha mipira katika himaya yake.
kutoka na uwezo wa Boni ambae amesajiliwa summer msimu huu na katika kipindi cha miezi 6 aliyochezea tayari vilabu vikubwa kadhaa barani ulaya vinapigana vikumbo kumnyakua nyota huyo ambapo moja ya klabu kubwa imetangaza kumtaka nyota huyo kwa jumla ya euros mil 25 huku klabu yake ambayo kutokana na kumilikiwa na tajiri huyo kutoka russia klabu tajiri kwa sasa nchini Holland ikitangaza kuwa mchezaji huyo hauzwi na anabakia kuwa mali ya Vitesse-Arnhem.

Mbali na Boni pia kuna nyota Didier Ya Konan (Hannover, Germany), mchezaji mwenye uwezo mkubwa kumiliki mpira na kugawa pasi pamoja na upachikaji mabao,ni mchezaji mwenye quality kama Diego wa Brasil na nyota wa zamani wa Weder Brehmen ya Germany ni mmoja kati ya nyota watakaotoa burudani kubwa katika mashindano hayo ya Africa Cup 2012.

Kikosi kamili cha Ivory Coast ni:

Goalkeepers:
Barry Boubacar (Lokeren, Belgium), Gerrard Gnanahouan (Avranches, France), Daniel Yeboah (Dijon, France)

Defenders:
Siake Tiene (Paris St Germain, France), Arthur Boka (Stuttgart, Germany), Benjamin Angoua Brou (Valenciennes, France), Igor Lolo (FC Kuban Krasnodar, Russia), Didier Zokora (Trabzonspor, Turkey), Emmanuel Eboue (Galatasaray, Turkey), Kolo Toure (Manchester City, England), Souleymane Bamba (Leicester City, England)

Midfielders:
Kafoumba Coulibaly (Nice, France), Jean-Jacques Gosso Gosso (Orduspor, Turkey), Didier Ya Konan (Hannover, Germany), Cheick Tiote (Newcastle United, England), Max Gradel (St Etienne, France), Yaya Toure (Manchester City, England)

Forwards:
Gervinho (Arsenal, England), Seydou Doumbia (CSKA Moscow, Russia), Didier Drogba (Chelsea, England), Salomon Kalou (Chelsea, England), Wilfried Boni (Vitesse Arnhem, Netherlands), Abdul Kader Keita (Al Sadd, Qatar)