WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday 9 January 2012

LIONS OF ATLAS YATANGAZA KIKOSI CHA MWISHO

Kocha wa timu ya Taifa ya Morocco "LIONS OF ATLAS" Eric Gerets ametangaza kikosi chake cha mwisho kitakachoweka kambi ya siku 10 katika mji wa Marbella nchini Spain kambi ambayo inaanza leo tarehe 09-01-2012 kujiandaa na mashindano ya soka ya Caf Nations Cup 2012,wakiwa nchini Spain "Lions of Atlas" watacheza mechi moja ya kirafiki dhidi Grasshoppers kutoka nchini Switzaland kabla ya kuwasili nchini Gabon siku ya tarehe 21-01-2012 ambapo siku mbili baadae tarehe 23-01-2012 itajitupa uwanjani katika pambano lake la mwanzo dhidi ya Tunisia katika michuano hio ya Caf Nations Cup 2012.
kikosi kamili cha "LIONS OF ATLAS"ni kama ifuatavyo:

Goalkeepers: Nadir Lmyaghri (WAC), Essam Bada (FUS Rabat), Mohamed Amcife (Augsburg, Germany).

Defenders: Jamal Elioui (El Khriteyat, Qatar), Mikael Bassir (Bursaspor, Turkey), Mehdi Benattia (Udinese, Italy), Abdul Fatah Boukhrise (FUS Rabat), Bader Qadouri (Celtic, Scotland), Abdul Hamid Kawthary (Monpellier, France), Ahmed Qantary (Stade Brest, France), Mustafa Mrani (MAS Fez).

Midfielders: Noureddine Mrabet (Kaisaryspor, Turkey), Younis Belhanda (Monpellier, France), Mubarak Bousouffa (Anzhi, Russia), Karim Ahmadi (Feyenoord, Netherlands), Adel Hermache (Al Hilal, Saudi Arabia), Hucine Kharja (Fiorentina, Italy).

Forwards: Oussama Saidi (Heerenveen, Netherlands), Mehdi Carcela (Anzhi, Russia), Marouane Chamakh (Arsenal,England), Youssef Arabi (Al Hilal, Saudi Arabia), Youssef Hadji (Stade Rennes, France), Adel Taarabt (Queens Park Rangers, England).

Wakati huohuo kiongozi wa O.F.A alikuwepo nchini Morocco kuangalia baadhi ya shughuli za Academy ya FUS-RABAT ambao ni mabingwa wa Caf Confederations Cup 2010-2011,
Kiongozi wetu wa O.F.A ambae alipata kujionea jinsi ya uendeleshaji wa shughuli mbalimbali za soka za Miamba hao wa soka barani Africa ambapo aliweza kutembelea kiwanja chao cha soka cha kisasa pamoja na ofisi mbalimbali na michezo mingine inayomilikiwa na miamba hao wa North Africa.
mbali na kutembelea kiwanja hicho cha kisasa pia alitembelea kiwanja chao cha zamani kilichopo katika mji wa HAY RIAD katikati ya jiji la Rabat kiwanja ambacho kwasasa kinatumika kama kiwanja cha mazoezi cha miamba hio pamoja na mazoezi ya timu zake za youth ambapo wana vijana wenye viwango vya hali ya juu kutoka nchini humo pamoja nchi kadhaa za north na west africa ambapo nyota hao ndio watakao wawakilisha miamba hio siku zijazo na pia kupunguza gharama za kununua wachezaji wa nje kwa gharama kubwa na badala yake wamekeza katika soka ya vijana ambao wanacheza soka na mbinu sawa na kaka zao wa timu kubwa huku wakiwa na walimu wenye viwango vya kimataifa katika ufundishaji na ndio wanaoleta maendeleo na mafanikio ya klabu hio kubwa kiuchumi na ndio moja ya mbinu kubwa ambayo timu hio imeweza kupata mafanikio mengi katika soka barani africa ambao hivi sasa ndio wanaoongoza ligi nchini morocco kwa kucheza mechi 15 huku walikwa na point 33 wakifuatiwa na Raja Casablanca pia iliyocheza mechi 15 na kuwa na piont 27 katika ligi hio ngumu yenye timu zilizosheheni wachezaji nyote wa barani africa na ambazo zinaendeshwa kisasa.
mbali na kiongozi wetu ambae alitembelea shughuli za klabu hio pia aliweza kwenda kuangalia pambano kali la wapinzani wa jadi wa jiji la Casablanca miamba Wyday Casablanca vs Raja Casablanca pambano ambalo lilichezwa katika uwanja wa Wydad Casablanca uwanja wa Stade Mohamed V jijini casablanca ambapo matokeo yalikuwa ni 0-0.