WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday 16 February 2012

MILAN YAIPONDA ARSENAL:BENFICA NDANI YA FRIZA LA ZENET

A.c Milan imeikandamiza Arsenal jumla ya mabao 4-0 katika michuano ya Eufa Champions League katika pambano lililofanyika katika uwanja wa San Siro mjini Milan.
Mabao ya Milan yalifungwa na Boateng katika dakika ya 15,Robinho 38,49 na Ibrahimovic katika dakika ya 79 kwa njia ya penalti.
Zlatan Ibrahimovic alishangilia bao la nne kwa nguvu kama vile amefunga bao la kwanza la Milan akimpa machungu Arsen Wenger ambae alikataa kumsajili akitokea Sweden kuanza kutaka kutangaza kipaji chake na hivyo Ibrahimovic kuanza safari yake ya kuwa mshambuliaji wa kutisha barani ulaya kwa kujiunga na timu ya Ajax Amsterdam ya ambapo mshambuliaji huyo wa Milan ni mchezaji pekee barani ulaya katika kipindi cha miaka 6 kutwaa ubingwa mara tano na timu 5 tofauti,
Baada ya kutwaaa ubingwa na Ajax Amsterdam katika msimu wake wa mwisho katika misimu aliyochezea alichukuliwa na Juventus ambapo msimu ule ule Juve walitwaa ubingwa wa Italia,
kutokana na uchunguzi uliofanywa na Chama cha soka cha Italia iligundua Juventus walikuwa wakinunua matokea kwa miaka kadha nyuma hivyo kuipiga faini timu hio pamoja na kuishusha daraja la pili ambapo Ibrahimovic alihamia katika klabu ya Inter Milan,
kutokana na uwezo wake mkubwa wa katika safu ya ufungaji Inter Milan ambayo ilitwaa ubingwa wa Italia mara 2 huku Ibrahimovic alikuwa kinara wa ufungaji katika timu hio pamoja na ligi ya Italia. Msimu uliofata alisajiliwa na Barçelona ambapo alitwaa na Ubingwa wa Spain na msimu uliopita alijiunga na Ac Milan ambapo ghafla baada ya ubingwa kutawaliwa na Inter Milan miaka iliyopita mfululizo Zlatan aliweza kuitwalisha ubingwa Ac Milan hivyo kumfanya kuwa mchezaji mwenye mataji mingi mfulululizo katika nchi tofauti alizochezea.
Nahodha wa Holland Mark Vam Bommel ambae alitwaa ubingwa na PSV Eindhoven ya holland kwa mara ya mwisho kabla ya kujiunga na Barçelona na kutwaa nao ubingwa wa Spain kabla ya kuihama timu hio na kujiunga na Bayern München ambapo kutwaa nao ubingwa kama nahodha msimu wake wa pili kabla ya msimu uliopita kujiunga na Ac Milan na kutwaa pia ubingwa wa kwanza akiwa na Zlatan.
Katika pambano jingine la Eufa Champions League Zenet st Petersburg ya Russia dhidi ya Benfica ya Ureno.
Katika pambano hilo lililochezwa katika uwanja wa nyumbani wa Zenet wa Ptrovskiy uliokuwa na baridi kali digrizi -15 chini ya zero ikiwa ni sawa na ndani ya friza la kugandishia barafu matokeo Zanet ilishinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Benfica.
Mabao ya Zenet zalipachikwa na Shirokov aliecheza soka safi na kupachika mabao 2 katika dakika za 27 na 88, na Semak katika dakika ya 71 wakati yale ya Benfica Lisbon yalifungwa na Pereira katika dakika ya 20 na Oscar Cardozo dakika ya 87.