WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday, 16 February 2012

MAN UNITED YAWACHAPA YOSSO WA AJAX:KINDA KUTOKA AJAX CAPETOWN APIGA DHIDI YA MAN U.

Yosso Lukoki akiwa katika moja ya mapambano ya Ajax Amsterdam
.........................................................................................................................

Kinda Lukoki katika moja ya mechi za Champions League dhidi ya Olym Lyon

..................................................................................................................................Kinda kutoka Ajax Capetown ya South Africa Lukoki aliesajiliwa msimu huu na kaka zao emeendelea kucheza mechi kubwa sio tu ligi kuu ya Holland,bali pia Chapions league na leo Europer League dhidi ya Manchester United katika pambano lililochezwa katika uwanja wa Ajax Amsterdam ArenA nchini Holland.

Manchester United wameshinda mabao 2-0 dhidi ya Yosso hao wa Ajax ambao ni chuo kikuu cha soka barani ulaya wakianza na generation mpya baada ya ile ya akina Sneijder,Van Der Vart,Stephen Piener,Ibrahimovic,Babel na kikosi kizima kuchukuliwa katika nchi mbalimbali na barani ulaya hivyo kutobakiwa hata mchezaji mmoja hivyo kupandisha kikosi kipya ambapo pia mbali ya shule za klabu hio pia ni wamiliki wa Ajax Capetown ya South Africa.

Kabla ya hapo generation ya akina Sneijder kuchukua nafasi ya kaka zao akina Van Der Sar,Seedorf,Frank na Ronald de Boer,Denis Bergkamp ambae sasa ni kocha msaidizi,Nwanko Kanu,Tijani Babangida na wengine wengi wakali akina Patrick Kluivert,Edgar Davids

Ajax Amsterdam kila msimu huchukua wachezaji kutoka katika Ajax Capetown na kuwaweka katika timu ya wakubwa walio na maskani yao mjini Amsterdam,msimu mitatu iliyopita ilikuwa ni zamu ya Eyang Enouh wa Cameroon kutoka Ajax Cape Town ambapo pia kuna yosso wengine wanapikwa ili kupandishwa katika timu kubwa Ajax ambayo inatengeneza Mamilioni ya Fedha kuwauza nyota wake mara baada ya kupata Dau la nguvu kutoka vilabu vingine vya barani ulaya.

Mchezaji wa kwanza kutoka Ajax Cape Town kuchukuliwa Ajax Amsterdam alikuwa ni Benny McCarthy mshambuliaji wa zamani wa Bafana Bafana huo ulikuwa ni mwanzo wa Ajax ya Holland kuanza safari yake ya kuchukua nyota pia kutoka South Africa ambao nao pia huchukua wachezaji vijana nyota kutoka bara zima la africa safari ambayo itaendelea kuwa ya miaka mingi kutokana na kuwa na walimu wenye utaalamu kutoka Holland ambao wanasimamia vijana wa kila umri ya timu hio kutoka jiji la Cape Town,

Mabao ya Manchester United yaliyofungwa na Ashley Young katika dakika ya 59 na Hernández Chicharito katika dakika ya 85.

Kabla kuanza kwa pambano hilo mashabiki wa Ajax Amsterdam leo mchana walichapana na mashakiki wa Manchester United hali iliyopekea mashabiki 23 wa pande zote mbili kushikiliwa na Polisi wa Amsterdam kutokana na ugomvi huo.

Hata Hivyo Polisi walifanikiwa kuingilia kati na kuwatenganisha mashabiki hao.

Katika pambano jingine lililofanyika katika mji wa Alkmar timu ya AZ ya mji huo nchini Holland imeifunga Andelecht ya Belgium kwa bao 1-0 kwa bao lililopachikwa na Yosso Adam Maher mwenye asili ya Morocco huku akiwa amezaliwa nchini Holland ambapo jana ameitwa rasmi kwa mara ya kwanza kujiunga na timu ya Taifa ya Holland siku ya tarehe 23-02-2012 kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya England itayochezwa nchini Holland siku ya tarehe 29-02-2012.


Matokeo mengine ya Europer League


Lazio 1-3 Atletico Madrid

Viktoria Plzen 1-1 Schalke04

Red bull Sulzburg 0-4 Metalist Kharkiv

Lokomotiv Moscow 2-1 Athletic Bilbao

Legia Warszawa 2-2 Sporting Lisbon

F.c Porto 1-2 Manchester City (wafungaji Valera kwa upande wa Porto,Pereira goli la kujifunga na Aguero kwa upande wa The Citizens)

Stoke City 0-1 Valencia

Steaua Bucharest 0-1 F.c Twente

Udinese 0-0 Paok

Wisla Kraków 1-1 Standard Liége

TrabzonSpor 1-2 Psv Eindhoven

Hannover96 2-1 Club Brugge