WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday, 23 February 2012

MSUMBIJI WAINGIWA NA HOFU KUIKABILI STARS

Wapinzani wa Taifa Stars katika kuwania nafasi ya kucheza Africa Cup Of Nations 2013 Msumbiji "Mambas"wameingiwa na hofu kuikabili Taifa Stars wiki ijayo jijini Dar Es Salaam baada ya jana kufungwa na Namibia jumla ya mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki iliyofanyika mjini Windhouk.
Katika pambano hilo la kirafiki kujiandaa kuikabili Taifa Stars nchi hio haikucheza vizuri kiasi cha kuanza kuleta hofu kubwa kwa kocha wao kutoka nchini Ujerumani kwa mujibu wa gazeti la kila siku la nchi hio la Jornal Notícias.Hata hivyo nchi hio ilicheza bila wachezaji wao wanaochezea timu ya Liga Muçulmana baada ya kupewa mapumziko kidogo kutokana na safari yao ya Zanzibar walikocheza pambano la Orange Champions League dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.
Msumbiji itacheza mechi ya mwisho ya kirafiki dhidi ya Malawi mjini Blantire siku ya jumamosi kabla ya kuikabili Stars wiki ijayo.

Wakati huohuo timu ya Taifa ya Vijana ya Msumbiji U17 jumatatu ya wiki hii ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Ujerumani U17 katika pambano lililofanyika katika Complex iliyojengwa na Fifa ya Mário Esteves Coluna Namaacha nje kidogo ya jiji la Maputo.
Timu hizo za vijana za nchi hizo zimekuwa zikikutana kila mwaka mwaka mara mbili nyumbani na egenini kwa timu moja kuanza kwenda ugenini na baadae kumalizia nyumbani katika mpango maalum wa urafiki ulioandaliwa na nchi hizo mbili.
Timu hio ya vijana iko katika maandalizi ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Can yatakayofanyika baadae mwaka huu vilevile katika michuano ya CPLP (Communidade dos Países de Lingua Portugues)nchi zinazozungumza lugha ya kireno ambayo yatafanyika nchini Portugal mwezi julai mwaka huu.
Michuano hio hufanyika kwa zamu kila nchi kuandaa michuano hio kwa wakati wanaopangiwa kuandaa ambapo huwashirikisha vijana wa timu za Taifa za nchi hizo U17 ambao ndio nyota wa baadae wa nchi zao kwa kizishirikisha nchi za Portugal,Brasil,Angola,Msumbiji,Guinea,Cape Verde,Sao Tomé and Princeple na East Timor.