MWANDISHI WETU
KOCHA Mkuu wa Chelsea ya England, Andre Villas-Boas, amesema kiungo kinda wa Tanzania anayechezea timu ya vijana ya Chelsea, Adam Nditi, ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaotarajiwa kupandishwa timu ya kwanza siku za usoni.
Villa-Boas, maarufu kama AVB, amenukuliwa na gazeti la Teleghraph la Uingereza la Januari 20, 2012 akisema makinda Nathan Ake, Adam Nditi na Mbrazili Lucas Piazon, ambao wote si wazawa wa England, ndio wanaokaribia kuingia katika timu ya wakubwa ya Chelsea.
Ake, ambaye ni kiungo mahiri kutoka Uholanzi, alisajiliwa na Chelsea mwaka 2010, akiwa na miaka 16, hali iliyozusha utata na timu yake ya zamani Feyenoord.
Nditi, 17, kiungo mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto, alisajiliwa miaka minne iliyopita akitokea Tanzania.
Piazon alisajiliwa hivi karibuni kutoka Sao Paulo ya Brazil akitajwa kuwa mmoja kati ya vipaji adimu kutoka Amerika Kusini na hivi karibuni alitimiza umri wa miaka 18.
Wana vipaji vya hali ya juu na itakuwa jambo zuri kama wakienda timu ya wakubwa moja kwa moja. Ni kweli wanaweza? Hilo ni juu yao zaidi, alisema AVB.
Kama atapandishwa, Nditi ambaye ni mtoto wa kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Zanzibar, Eric Nditi, huenda akachukua nafasi ya beki wa kushoto wa Chelsea, Ashley Cole ambaye kwa siku za karibuni amejikuta katika wakati mgumu na kocha AVB.
Adam Nditi ni nyota aliekulia pamoja na baadhi ya nyota wa Oranje Football Academy iliyo na makao makuu yake mtaa wa Kikwajuni ambapo pia Adam alipata mafunzo kutoka kwa makocha walewale walio walea akina Nadir Haroub (Canavaro wa Yanga)na Abdi Kassim (babi wa Azam)wakati na umri kama huo hivyo nyota huyo aliondoka akiwa na mafunzo tosha kama wanayopata nyota wa O.F.A hivyo Kinda huyo alijijengea msingi msingi mzuri wakati akitua hapo Chelsea kutokea Zanzibar-Tanzania.
Adam Nditi ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa timu kikwajuni na timu ya Taifa ya Zanzibar Eric Nditi.
................................................

(KWA MAELEZO ZAIDI BONYEZA HAPA ---> http://www.chelseafc.com/page/AcademyProfiles/0,,10268~1333485,00.html )
Adam Nditi
Born 18/9/94 in Zanzibar, Tanzania.Adam arrived at Chelsea as an Under 13 and can play either left-back or left-wing.
Very quick, he bases his game on Ashley Cole, and enjoys taking players on.
Prior to signing as a first-year scholar, he had already amassed 27 youth team appearances, and featured regularly during the 2011 FA Youth Cup run.
..........................................................