WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 24 March 2012

CHANGAMKIENI REAL MADRID FOUNDATION KWA VIJANA WENU NCHINI

Balozi wa Spain nchini Msumbiji D. Eduardo López Busquet akikabidhi kikombe kama ishara ya ufunguzi wa mradi huo wa Real Madrid Foundatin wa kusaidia watoto nchini humo.
................................................................................................
Real Madrid Foundation ni mradi maalum unaodhaminiwa na timu hio kubwa kutoka nchini Spain kwaajili ya kusaidia vijana wa Kiume na Kike duniani kato.
Timu hio imekuwa ikisaidia kwa vijana wa umri mbalimbali kuanzia miaka 8 hadi 17 ili vijana hao waweze kujijengea mazingira mazuri ya vipaji vyao ambapo vitawasaidia katika ajira zao hapo baada na kuweza kuwasaidia vijana hao kuweza kukuza vipato vyao kutokana na michezo hio.
Miamba hio ya soka barani Ulaya mwezi uliopita walifungua rasmi mradi huo nchini Msumbiji chini ya usimamizi wa mwanasoka wa kimataifa wa zamani wa nchi hio ambae hivi sasa ni kocha wa timu ya Ferroveario ya nchi hio Chiquinho Konde ambae miezi michache aliyopita alikuwepo mjini Madrid kusaini mradi huo ambapo utaweza kuwajumuisha vijana wa kiume na kike 300 ambapo unagharamiwa na Miamba hio kutoka nchini Spain.
Timu hio imekuwa sio ikisaidia kundi kubwa la vijana kuweza kufanikiwa katika maisha yao bali pia inatoa mafunzo kwa makocha mbalimbali ili mafunzo hayo yaweze kuwasaidia kuwaendeleza vizuri nyota hao wadogo katika michezo na kufikia malengo yao ya kupata mafanikio mazuri hapo baadae.
Mbali na soka pia wanatoa michango kwa michezo ya Basketball na mingineyo ambapo nadhani Tanzania tayari imejenga uhusiano wa mwanzo na Miamba hio.
Suala ni je lini wataweza kufuatilia suala hili ili kuweza kuleta maendeleo kwa vijana suala ambalo halipewi umuhimu wowote kuwasaidia nchini sio kwa serikali tu bali hata kwa wadau na vyama vinavyosimamia masuala ya mchezo?
Hii hapa ni njia moja ya mkato ya kuweza kuwaleta watu ambao wataweza kuwasaidia vijana nchini na kuleta mapinduzi ya michezo ,na pengine huenda ikawa ndio mwanzo mzuri kwa kuijenga upya nchi katika michezo ya kimataifa kutokana na kupata msingi mzuri kwa vijana wake.
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Msumbiji Toci Tico ambae ni mmoja wa wasimamiaji wa mradi huo akitoa shukurani zake kwa ufunguzi wa vituo hivyo vya kuwasaidia kuendeleza maendeleo ya watoto nchini humo.
Watoto kutoka katika mitaa ya Xipamanine na mitaa mingine wakijipatia mlo katika sherehe za ufunguzi wa Real Madrid Foundation hivi karibuni.
Watoto wa Buyenzi nchini Burundi wakisherehekea ufunguzi wa Real Madrid Foundation nchini Burundi.
Real Madrid Foundation nchini Benin ambacho kina wanandinga 200 wa kiume na kike wenye umri mbalimbali
School ya michezo ya Real Madrid Foundation nchini Equador yenye vijana 700 wenye umri kati ya miaka 6 hadi 17.
Kituo cha Real Madrid Foundation nchini Fillipines chenye vijana 70 umri kati ya miaka 6 na 17 pia kikiwa na makocha 21 wanaofadhiliwa  na miamba hio kutoka Madrid.
Real Madrid Foundation nchini Honduras kituo kikiwa na nyota yosso 200 wenye umri kati ya miaka 6 na 17 pia kikiwa na makocha 25.
Vijana wanaonufaika na Real Madrid Foundation nchini Hungary shool ambayo ina nyota wa baadae 112 wa kiume na kike.
Moja vituo vya soka nchini Panama vinavyofadhiliwa na Real Madrid tayari wameanza kujikusanyia makombe katika mashindano yaliyofanyika kwa vijana chini ya umri wa miaka 7 na 11.
Kituo cha Real Madrid Foundation nchini Fillipines chenye vijana 70 umri kati ya miaka 6 na 17 pia kikiwa na makocha 21 wanaofadhiliwa  na miamba hio kutoka Madrid.
Ndugu zake Edebayor nchini Togo wakinufaika na Real Madrid Foundation kituo chenye vijana 100 wote wakiwa ni wa kiume.
Makocha 78 wakifaidika na mafunzo kutoka kwa mkufunzi wa kimataifa kutoka katika klabu ya Real Madrid mafunzo yaliyozishirikisha nchi za RD Congo,Rwanda na Burundi,
makocha 48 walitokea katika privince ya south Kivu ili kuweza kuwapatia taaluma watu wa maeneo hayo ili kuweza kwenda sambamba na makocha wa miji mingine katika taaluma hio na kuweza kuwasaidi kuwaongoza nyota chipukizi wa maeneo hayo na kuweza kuleta mafanikio ya mikoa hio.
Makocha 23 walitoka katika nchi za Burundi na Rwanda wakati waliosalia kujumuisha idadi hio walitokea katika miji ya Bukavu nchini Congo.
Makocha 26 wakipata mafunzo kutoka kwa makocha wataalamu kutoka klabu ya Real Madrid mafunzo yaliyowashirikisha makocha 10 kutoka nchi Ghana na 16 kutoka nchini Sierra Leone.
Makocha waliowawakilisha makocha wenzao katika picha hii ambayo inafanya jumla ya makocha 60 wanaodhaminiwa na Real Madrid Foundation nchini Poland wanaowafundisha nyota wadogo wenye umri wa miaka 13 na 16.
Makocha 28 kutoka nchini Venezuela wakipewa mafunzo kutoka kwa wataalamu kutoka kwa miamba ya soka barani ulaya Real Madrid.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Shati number 9 ya mwanandinga nyota wa klabu Real Madrid.suala je kuna mpango wowote uhusiano wa Real Madrid na Serikali ya Tanzania kuweza kuleta mafanikio yoyote kwa vijana nyota wadogo nchini ???????? 
Rais Jakaya Kikwete Akipokea t-shirt ya Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabéu na kuanzisha uhusiano kati ya Serikali ya Tanzania na Miamba hio.
Je Uhusiano huu ulikuwa iliishia hapa tu katika picha? Au kuna mpango wa kuweza kuwasaidi vijana wetu nchini na kuweza kulisaidia taifa leyu hapo baadae ????????
Nadhani hili linahitaji kufatiliwa ili vijana wetu nchini waweze kunufaika kama wenzetu wa Msumbiji pamoja na nchi nyingine kama ambavyo tumeona hapo katika picha zilizopita juu.