WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday 26 March 2012

SIMBA YAWARARUA WAARABU

SIMBA SC  imeifunga ES Setif kutoka Algeria 2-0 katika mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho (CAF) uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na Emmanuel Okwi na Haruna Moshi na yote yalipatikana katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Hudu Munyemana kutoka Rwanda ulianza kwa kasi na Simba ndiyo timu iliyotawala pambano hilo kwa kiasi kikubwa na kama washambuliaji wake wangekuwa makini, ingeweza kuibuka na ushindi mkubwa.
Katika kipindi cha kwanza pekee, Simba ilipoteza nafasi takribani nne za wazi zilizopotezwa na washambuliaji wake Okwi na Felix Sunzu.
Hata hivyo, katika dakika ya 73, Okwi aliwainua vitini washabiki wa Simba baada ya kufunga bao kwa shuti la mbali na kuyafanya matokeo kuwa 1-0.
Bao la pili lilifungwa dakika nane baadaye mfungaji akiwa Boban ambaye aliunganisha moja kwa moja mpira uliopanguliwa na mlinda wa Setif kutokana na faulo iliyopigwa na Machaku Salum.
Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, alifanya mabadiliko katika kikosi chake ambapo Machaku alianza huku Mafisango na Mwinyi Kazimoto wakiwa katikati.
Mabadiliko hayo ya Cirkovic yalikuwa mazuri kwani Simba ilitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa, huku Kazimoto na Mafisango wakidhibiti eneo la kiungo.
Mchezo wa marudiano utafanyika wiki mbili zijazo katika mji wa Setif na iwapo Simba itafuzu, itacheza na mshindi wa mechi kati ya Ferroviario ya Msumbiji na Shanks ya Sudan.
Katika mchezo huo Simba iliwakilishwa na Kaseja, Kapombe, Maftah, Nyoso, Yondani, Mafisango, Machaku, Kazimoto, Sunzu, Boban na Okwi.

MATOKEO KAMILI YA MICHUANO YA CAF ORANGE CONFEDERATION CUP
Simba (TAN) 2-0 Entente Sétif (ALG)
St George (ETH) 1-1 Club Africain (TUN)
Lydia Academic (BDI) 1-1 ENPPI (EGY)
Black Leopards (RSA) 4-2 St Eloi Lupopo (COD)
Séquence FC (GUI) 0-2 CO Meknès (MAR)
US Haut Nkam (CMR) 0-0 Heartland (NGR)
Royal Leopards (SWZ) 1-1 US Tshinkunku (COD)
Etoile Filante (BUR) 2-2 ASEC Mimosas (CIV)
Ferroviario (MOZ) 0-1 Al Ahly Shandy (SUD)
Invincible XI (LBR) 0-2 Wydad Casablanca (MAR)
Gamtel (GAM) - Real Bamako (MLI)
TANA Formation (MAD) 2-0 InterClube (ANG)
Hwange (ZIM) 1-1 Al Amal (SUD)
Renaissance (CHA) 3-2 CO Bamako (MLI)
Kallon FC (SLE) 0-0 Warri Wolves (NGR)
AC Léopards (CGO) 1-2 CS Sfaxien (TUN)