WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 11 March 2012

HUU HAPA MPANGO WA KUFUFUA KIWANGO CHA SOKA KATIKA FIFA

Haiti ipo katika nafasi ya 72 kwa kiwango bora duniani wakiwa na point 469.
Ukizungumzia kama Tanzania haiwezi kuwa timu nzuri kutokana na uchumi wake nadhani Tanzania ina uchumi mkubwa sana kulinganisha na Haiti.

Isitoshe kama nchi hio ina kiwango kikubwa kama hicho cha soka ambacho Tanzania haijawahi kukifikia ina maana nchi hio ina nyota wenye viwango vikubwa sana katika soka.

Kutokana na viwango vizuri vya nyota wao inaonyesha wana mpango mzuri tokea timu zao ndogo wanazozisimamia mpaka kuweza kufikia kiwango hicho cha soka duniani.

Haiti ni nchi ndogo lakini kiwango kikubwa inaonyesha sio siri wana wachezaji wakali sana hasa ukilinganishwa wamezongwa na mataifa yenye viwango vikubwa katika ukanda wake.

Nadhani hapa itakuwa ni jambo la busara kialika Haiti kuja nchini kucheza na Stars ili tuweze kurejesha kiwango chetu cha soka kwa timu ya Taifa kwa mchupo mkubwa sana kutokana na kama tukishinda tutakuwa tumeishinda timu yenye kiwango cha juu.

Hapo timu za vilabu nchini pia vitanufaika kutwaa nyota katika vilabu vyao ambao watakuwa na viwango sawa na timu za Afrika ya magharibi au Kaskazini hivyo kutoa ushindani sio kwa taifa tu bali itakuwa pia ni faida kwa vilabu nchini.
Soka ya nchi kwa vilabu ni hapa nchini tu,tukitoka nchini hata vilabu vetu vipo katika kiwango chini na kibovu sana nje hivyo tunahitaji kujitwalia wachezaji kutoka mataifa kama haya masikini ya Haiti wenye viwango vya uhakika kulinganisha na sisi kwani wanasoma mengi kutoka south amerika.

Hii ndio iliyoisaidia sana Sao Tome and Principle Islands kuchupa nafasi 53 juu katika kiwango cha Fifa baada ya kuifunga Sierra Leone ambao walikuwa na kiwango kikubwa sana kulinganisha na wao.

Aidha tucheze michezo mitatu ambayo lengo lake ni kuipandisha nchi katika kiwango kikubwa kabla ya kuanza kucheza mechi za kawaida kudhibiti nafasi yetu isianguke chini kwa mpango mzuri wa timu ya Taifa.
Nadhani tuliwahi kucheza na Cape Varde Islands na kuifunga hapo taifa,baada ya kutufunga kwao bao 2-1 kama sikosei.
Wenzetu hawa ambao tuliwafunga hapo nyumbani wao wamezidi kupaa juu kwa kuwa katika kiwango cha 62 kwa ubora duniani.kisiwa kidogo na Tanzania ina uchumi mara nyingi sana ukilinganisha na visiwa hivyo.

nadhani kama TFf watafuatilia kucheza nao katika mechi ya kirafiki kama Stars ikishinda itakuwa imechupa
tena juu kwa hatua kubwa sana kulinganisha na nchi hio kuwa katika kiwango cha juu sana mara mbili na robo kuliko sisi tulipo hivi sasa.

Mechi ya tatu au inaweza kuwekwa kuwa ndio mechi ya kwanza kwa Stars iwe dhidi ya Sao Tome and Principle Islands. hawa wapo katika nafasi ya 115 kwa ubora wa soka duniani ambapo wamekuwa ni wapandaji bora wa kiwango mwezi huu baada ya kupanda juu kwa mara 53 baada ya kuifunga Sierra Leone.
Hizi mechi tatu zinatosha kuiweka Tanzania katika nafasi ya 71 hadi 75 kwa kiwango duniani ambapo hapo ni kufanya mkakati wa kushikilia nafasi hizo kwa kucheza na timu zilizopo juu kidogo na kuzidi kujijengea uzoefu kwa walioko juu yetu.
TUKUMBUKE HATA WAKATI WA MAXIMO TULIKUWA HATUKO KATIKA KIWANGO CHA KUTISHA KATIKA FIFA.
ILIKUWA NI MWENDO WA KINYONGA NAFASI 2 HADI 3 KUPANDA JUU.TULIWEZA KUPANDA NAFASI 12 JUU BAADA YA KUIFUNGA NEW ZEALAND KATIKA MECHI YA KIRAFIKI NA KUFIKIA NAFASI ZA 98.

Wakati New Zealand haikuwa na kiwango kikubwa cha soka wakati ule kama ambavyo Haiti ipo sasa au Cape Verde Islands.

Tusicheze mpira katika magazeti tu tufanye vitendo.Huu ni mpango bora kulikoni kuialika Brasil au kutaka kuileta nchini Real Madrid mpango ambao ni kuharibu mali bila ya manufaa yoyote.
Ukimualika Rais na kiongozi mwingine wa Real Madrid ni sawa na kuialika klabu nzima na ujumbe wako au lengo lako utafika/litafika  klabu kwa viongozi waliobakia wa klabu.
Hii nadhani ni nafasi nzuri kwa Taifa kufanya mpango mzuri wa kuviandikia maombi ya mechi za kirafiki nchi hizo katika tarehe zilizoko katika Fifa na ile tabia ya kukaa bila mechi za kirafiki katika tarehe ya Fifa nadhani kwa kiwango cha sasa,kama itaendelea basi tusibiri kufikia kiwango cha 200 kwa ubora wa fifa duniani.