WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday, 5 March 2012

MAMELODI SUNDOWNS YAFANYA MAANGAMIZI

Timu ya Mamelody Sondowns ya Afrika Kusini imefanya mauaji makali baada ya kuicharaza bila hurumu timu ya Powerlines Fc inayocheza ligi daraja la nne kwa kuikandamiza jumla ya mabao 24-0 katika mechi ya kuwania kombe la Africa kusini  linaloshirikisha timu za primier league hadi timu za daraja la nne.
Kwa ushindi huo Sundowns wameandika rekodi mpya kwa ushindi mkubwa katika mechi moja baada ya kuipita ile ile rekodi ya mwaka 1976 na 1986 rekodi zote ziliwekwa na AmaZulu ya mji wa Durban katika michuano kama hio.
Hadi kufikia mapumziko Sundowns walikuwa mbele kwa jumla ya mabao 10-0.
Powerlines F.C ambao walikuwa wakichezea uwanja wa nyumbani walijikuta wakibeba kapu hilo la mabao kutoka kwa wafungaji.
Goalscorers: Hlompho Kekana 7, 15, 31, 50, 61, 78, 80, Richard Henyekane 12, 20, 56, 72, 74, Nyasha Mushekwi 24, 41, 43, 45+1, 45+2, 52, Samuel Julies 54, 76, Elias Pelembe 65, 70, Lebohang Mokoena 71, 90+1
Hata hivyo pamoja na ushindi huo haukuweza kuvuuka rekodi ya mabao mengi katika pambano moja kwani hadi sasa rekodi inashikiliwa na klabu Malagasy AS Adema ya Madagasca iliyonyongwa jumla ya mabao 149-0 dhidi ya Stade Olympique Emyrne pia ya nchi hio.
Katika pambano hilo bao la mwisho kabla ya kumalizika mchezo  ilikuwa ni bao la kujifunga mwenyewe kutokana na hasira za mmoja wa mchezaji wa Malasasy A.S Adema kuukwamisha mpira langoni mwake huku akipinga uamuzi m'bovu wa refaree wa pambano hilo ambapo hilo lilikuwa ndio bao la kufunga kitabu cha pambano hilo.