WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday 30 April 2012

SIMBA YAENDELEZA UBABE KWA WAPINZANI CAF

SIMBA kama kawaida yao katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwaka huu,imeendeleza kutoa dozi kwa wapinzani wake katika michuano hio baada ya jana kuizamisha Al Ahly Shandy ya Sudan kwa mabao 3-0.

Mchezo huo wa kwanza raundi ya pili ulifanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kuiweka kwenye mazingira mazuri Simba ya kufuzu hatua ya raundi ya tatu ambapo itasubiri kupangiwa timu zitakazokuwa zimetolewa raundi ya tatu ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kama Simba itashinda hatua hiyo inayofuata itakuwa imeingia hatua ya makundi hivyo kuzidi kuitangaza nchi katika michuano ya kimataifa mwaka huu.

Ushindi wa jana umeifanya Simba kuendelea kutoa dozi kwa timu za ukanda wa Kiarabu baada ya hatua iliyopita kuitupa nje ya mashindano ES Setif ya Algeria, ambapo zilipokutana Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda mabao 2-0 na ziliporudiana nchini Algeria Simba ilifungwa mabao 3-1, lakini ikasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.

Simba imethibitisha nguvu yake ya kuzitambia hapa nyumbani timu za Uarabuni, ambapo baadhi ya mechi hizo ni mwaka 1974 ilipoifunga Mehlala ya Misri bao 1-0. Timu nyingine zilizowahi kufungwa na Simba ni JET ya Algeria, Zamalek ya Misri ambayo ilivuliwa ubingwa wa Afrika mwaka 2003. Ilifungwa Dar es Salaam bao 1-0 nayo ikaenda kushinda Cairo, Misri bao 1-0, zikapigiana penalti Simba ikashinda 3-2.

Waarabu wengine waliowahi kuonja kipigo cha Simba ni Al Ahly ya Misri, ambayo ilifungwa mabao 2-1 Tanzania na ikashinda mabao 2-0 kwao mwaka 1985 na wengine ni Al Mokaoulun ya Misi ilifungwa Dar es Salaam mabao 3-1 ikashinda kwao mabao 2-0.

Katika mchezo wa jana, mabao ya Simba yalifungwa na Haruna Moshi dakika ya 68 na Patrick Mafisango dakika 76 kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi kufunga bao la tatu dakika ya 90 , hivyo Simba sasa inahitaji sare katika mchezo wa marudiano au isifungwe zaidi ya mabao 2-0 ili isonge mbele.

Al Ahly Shandy iliyoingia hatua hiyo kwa kuitoa timu ya Ferroviario ya Msumbiji ilionekana kucheza kwa kuonana sana na kuilazimisha Simba kucheza kwenye lango lao muda mwingi wa kipindi cha kwanza.

Ilikaribia mara kadhaa kufunga lakini washambuliaji wa timu hiyo Faris Abdalla, Hamoud Bashir na Eltaueb hawakuwa makini kwani mashuti yao mengi waliyopiga aidha yalipaa juu ya lango au kuokolewa na kipa Juma Kaseja.

Dakika ya 25 mshambuliaji Felix Sunzu aliwazunguka mabeki wa Shandy ndani ya eneo la penalti, lakini mpira hafifu aliopiga haukuweza kulenga goli.Dakika mbili baadaye Shandy walijibu mapigo kwa mshambuliaji wake Fareed Mohamedi kupiga shuti kali akiwa nje ya 18 na kupaa juu ya lango la Simba.

Simba walipata penalti dakika ya 38 baada ya mshambuliaji Okwi aliyekuwa anakwenda kufunga kukwatuliwa na kipa wa Shandy Abdelrahman Ali na mwamuzi Nhleko Simanga kutoka Swaziland kutoa penalti, lakini kiungo Patrick Mafisango alikosa kwa mpira aliopiga kudakwa na kipa huyo.

MATOKEO KAMILI YA MICHUANO HIO NI KAMA HIVI:

04-27-2012   Enppi  3 - 1 C.O. Bamako
   
 04-28-2012   ASEC Abidjan  1 - 1 CO Meknes
     
 04-28-2012   Royal Leopards FC  0 - 1 Club Africain 
  
 04-29-2012   Warri Wolves FC  3 - 1 Black Leopards 
   
 04-29-2012   Heartland FC  3 - 2 AC Leopards   

 04-29-2012   Interclube  4 - 1 El Amal    

 04-29-2012   Wydad Casablanca  3-0 AS Real de Bamako