WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 28 April 2012

TBL KUDHAMINI LIGI KUU ZANZIBAR

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) imejitosa kudhamini Ligi Kuu Zanzibar msimu ujao 2012/2013 kwa kiasi cha Sh milioni 140.

TBL imetangaza kudhamini ligi hiyo kwa kutumia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malt.

Meneja Masoko wa kinywaji hicho, Fimbo Butallah alisema jana mjini hapa wakati wa makabidhiano ya mkataba wa udhamini huo uliofanyika kwenye hoteli ya Bwawani.

Alisema wamesaini mkataba wa miaka mitatu kudhamini ligi hiyo na kwamba utagharimu Sh milioni 140 ambazo zitatumika katika mahitaji muhimu kwa timu shiriki yakiwemo usafiri, chakula na malazi, vifaa vya michezo na zawadi kwa washindi.

“Kwa mwaka huu wa kwanza, Grand Malt itatoa shilingi milioni 140,” alisema Meneja huyo na kuongeza kuwa kampuni yao itashirikiana na Serikali, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na klabu bega kwa bega kuinua soka la Zanzibar.

“Tumepokea mzigo huu na tutashirikiana na wengine ambao watajitolea kudhamini ili kuleta mapinduzi makubwa katika soka la Zanzibar,” alisema.

Naye Makamu wa Rais wa ZFA Pemba, Ali Mohammed alisema wamefanikiwa kupata udhamini huo kutokana na mchakato mzima uliongozwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo na uongozi wa ZFA ambao ulitoa fursa kwa kinywaji hicho kudhamini ligi hiyo.

“Fursa hii inatokana na ukweli kwamba wenzetu wana uzoefu mkubwa katika kuendeleza michezo mbalimbali,” alisema Mohammed na kusema kuwa ana imani kubwa kuwa ushirikiano huo wanaouanza utaleta ufanisi mkubwa katika ligi yao na kuahidi kuwa atazingatia masharti yote na matakwa ya mkataba na kutoa ushirikiano wa kweli katika kuendeleza michezo hapa Zanzibar.

Ligi kuu ya Zanzibar kwa sasa inashirikisha timu 12 ambazo ni Miembeni United, Miembeni SC, Kikwajuni, Mafunzo, Polisi, KMKM, Zimamoto, Mundu, Chuoni, Jamhuri, Chipukizi na Super Falcon.