WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 7 April 2012

SIMBA YAPETA CAF


EMMANUEL Arnold Okwi jana aliifungia Simba bao katika dakika ya 90 ya mchezo kati ya Wekundu wa Msimbazi na Setif ya Algeria, lililoivusha timu yake katika hatua nyingine ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF).
Okwi alifunga bao hilo baada ya kuachia shuti kali lililokwenda wavuni moja kwa moja licha ya juhudi za kipa wa ES Setif, Mehdi Benhamoud, kulifuata na kuzima nderemo za washabiki wa klabu mwenyeji waliojazana kwenye Uwanja wa Stade 8 Mai 45 lilikochezwa pambano hilo.
Katika mchezo huo, Simba ilifungwa mabao 3-1 lakini inapita kwenda hatua nyingine kwa sababu ya faida ya bao la ugenini. Katika mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, Wekundu wa Msimbazi waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Pambano hilo lilianza kwa kasi huku wenyeji wakionyesha uchu wa kusaka mabao lakini lilivurugika katika dakika ya 12 ya mchezo baada ya mlinzi tegemeo wa Simba, Juma Said Nyoso, kulimwa kadi nyekundu kwa madai ya kumpiga mchezaji wa Setif bila ya mpira.
Mabadiliko hayo yalimfanya Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, kufanya mabadiliko ya kiuchezaji ambapo alimhamisha Patrick Mafisango kutoka kuwa kiungo wa ulinzi na kurudi nyuma kucheza kama mlinzi wa kati kuziba pengo la Nyoso.
Mabadiliko hayo yaliifanya Setif kutawala mchezo huo na dakika 20 baadaye, mshambuliaji hatari wa timu hiyo, Akram Djanit, akapachika bao la kwanza kwa timu yake.
Bao hilo lilitokana na mpira wa krosi uliopigwa kutoka winga ya kulia ya Setif na Djanit ambaye hakucheza mechi ya kwanza jijini Dar kwa sababu ya maumivu, akaunganisha mpira huo wavuni kwa mguu wa kulia.
Hadi timu zinakwenda mapumziko, matokeo yalikuwa 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na iliwachukua dakika mbili tu Setif kuandika bao la pili kupitia kwa Djanit ambaye alivunja mtego wa kuotea wa walinzi wa Simba na kupachika bao kiufundi.
Hata hivyo, wakati akielekea kufunga bao hilo, Djanit aligongana na Juma Kaseja na kupoteza fahamu, jambo lililosababisha atolewe na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine.
Dakika nne baadaye, Setif waliandika bao la tatu kupitia kwa Adel Benmousa, ambaye alimalizia muvi nzuri iliyotokana na makosa ya mabeki wa Simba.
Kuona hivyo Milovan alifanya mabadiliko ya kuwatoa Salum Machaku na Amir Maftah na nafasi zao kuchukuliwa na Nassor Said Masoud na Victor Costa, mabadiliko ambayo yaliifanya ngome ya Simba kutulia zaidi.
Wakati watu wakidhani kwamba mpira utamalizika kwa matokeo hayo ya 3-0, Okwi alifunga bao kutoka umbali wa mita 25 kutoka golini.
Baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe, Okwi aliwapita walinzi wawili wa Setif na baada ya Felix Sunzu kukimbia kutoka alikokuwa, walinzi wa Setif waliacha nafasi na ndipo Okwi alipofumua shuti hilo kali lililokwenda wavuni.
Simba sasa inasubiri matokeo ya mechi kati ya Ferroviarro de Maputo ya Msumbiji na Al Ahly Shandy ya Sudan ambayo mshindi wake ndiyo atacheza naye baadaye mwezi huu.
Simba iliwakilishwa na Kaseja, Kapombe, Maftah (Chollo), Nyoso, Yondani, Mafisango, Machaku (Costa), Kazimoto, Sunzu, Okwi na Boban.

KITENDO cha timu ya Simba kuifunga ES Setif ya Algeria kimevunja rekodi kadhaa za miaka ya nyuma na kudhihirisha ile dhana kwamba yenyewe ndiyo vinara wa Tanzania linapokuja suala la mechi za kimataifa.
Kwa kuanzia, imekuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kuitoa timu kutoka Afrika Kaskazini tangu yenyewe ilipofanya hivyo kwa Zamalek ya Misri mwaka 2002.
Pia, imekuwa klabu ya kwanza ya Tanzania kuitoa klabu kutoka Algeria katika michuano ya Afrika tangu miaka 20 iliyopita wakati yenyewe tena ilipofanya hivyo kwa kuitoa USM AL Harrach.
Simba pia imekuwa timu ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kufika katika raundi ya tatu ya Kombe la Shirikisho au michuano mingine yoyote mikubwa ya Afrika katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

MATOKEO MENGINE YA MICHUANO HIO NI

Warri Wolves (NGR) 2  FC Kallon (SLE) 0

St Eloi Lupopo (COD) 2  Black Leopards (RSA) 2

 ASEC Mimosas (CIV) 2  Etoile Filante (BUR) 0