WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Friday, 6 April 2012

FUFUENI SOKA YA ZANZIBAR 2

Katika mahojiano mengine kati ya wadau wa nje na Blog ya Oranje Football Academy kuhusu  changamoto za kufufua soka Zanzibar wiki hii inaendea kwa mdau kutoka Duisburg nchini Holland.
Haya hapa ni maelezo yake kuhusu kupata maendeleo:

1)kwanza kabisa napenda kutoa shukurani kwa blog hii kunipatia nafasi ya kuzungumza machache ambayo labda yanaweza kutoa msaada kwa ndugu zetu kuweza kufufua soka nchini kutokana na Serikali kuonekana suala hili sasa wameamua kulitaka kwa madhumuni ya maendeleo ya nchi.

Kwa ufupi soka ni mbali na kuwa ni starehe kama inavyozoeleka kujulikana na wengi bali ni uhusiano na urafiki kati ya mtu na mtu au watu wa kikundi na kikundi nchi na nchi au bara na bara hadi kufikia dunia nzima kujuana kutokana na soka.

Watu wengi hupata ajira sio tu kwa wachezaji bali hata kwa viongozi wa vikundi hivyo au vyama vinavyosimamia michezo hio na hata kupata mawaziri na wasimamiaji wakubwa kutoka serikalini kutokana na michezo huku soka ikibakia kuwa ni mchezo mkubwa unaobeba michezo yetu ndani ya nchi.

Kama kutakuwa kuna waziri au raisi wa michezo katika nchi na hakuna hata mchezo mmoja unaoleta manufaa yoyote kutokana na viongozi hao kutojua au kutojali kuwa "mkate wao wa kila siku" unatokana na michezo,nadhani hakuna faida kuwa na wizara za michezo na kulipa mishahara ya bure kwa wizara nzima pamoja na viongozi wanaosimamia  ngazi za michezo katika nchi.

Serikali imekuwa ikilipa mishahara wizara za michezo kwa miaka mingi sasa,lakini suala ni mchezo gani?
hakuna hata mara moja Serikali ilitaka kujua maendeleo ya kile inacholipia kila mwezi kwa watendaji kazi hao wakati hakuna hata mchezo mmoja ambao wizara hizo inafatilia au kutaka kujua maendeleo ya kazi zao zilizowaweka wizarani mwao.

Nadhani hivi sasa imefika wakati wahusika wote wakuu wa michezo nchini kufatilia kwa makini michezo yote ambayo ndio sababu za kuundwa kwa wizara na vyama hivyo kushirikiana kwa karibu na walengwa wanamichezo nchini ili kuweza kuleta mafanikio makubwa huku soka ikiwa ndio mchezo wa kwanza unaounganisha na kuwakilisha wanamichezo wengine kote duniani.

2) ili kuweza kuleta mafanikio ya soka nchini tuanze pia kuangalia tokea huko chini kwa timu zetu za watoto hadi kwa timu kubwa,
Kumekuwa na kawaida kwa miaka mingi kule nyumbani kuwa na usemi huu "uwanja wa jeshi,uwanja wa ujamaa,uwanja wa chipukizi,uwanja wa nyuki."

Hivi viwanja vyote vya mji mzima ni viwanja vya "BARAZA LA MJI WA ZANZIBAR" lakini kutoka na kuzoeleka kama ni uwanja wa timu fulani unazifanya timu hizo kuonekana kama kwamba kweli ni viwanja vyao walivyonunua na wanavimiliki kama ni wenye mali hizo,hivyo kuzinyima vilabu vingine kuvitumia kwani kuwa wachache huwa wanafikiria kuwa wana haki zote na wengine hawawezi kuvitumia viwanja hivyo.

"NADHANI HAKUNA HATA KLABU MOJA INAYOWEZAKUJENGA UKUTA AU KUCHIMBA HATA SHIMO DOGO NDANI YA ENEO LOLOTE AU KARIBU YA VIWANJA HIVYO". hapo ndio utakuwa uhusiano wao na Manispaa ya mji wa Zanzibar utafikia mwisho kati ya pande hizo mbili.
Tumeona hata maeneo mengine yanatumika kwa baraza la mji kuendesha shughuli nyingine zisizokuwa za soka kama siku kuu ,au mambo mengineo bila ya kujali klabu hio au hizo zipo katika ligi au hapana.

Hivi sasa kumekuwa na mafuriko ya timu za soka za watoto nchini Zanzibar kitu ambacho ni mawazo mazuri sana katika nchi kuwa na vijana wenye wenye lengo zuri la kutaka hapo baadae kuchezea vilabu vikubwa au kuliwakilisha taifa lao.

vijana hao wamekuwa hawapewi kipau mbele na wizara au vyama vinavyosimamia michezo nchini,lakini vijana hao wanapoamua kuwachana na michezo na kuanza kukaa mitaani kufanya mambo maovu,hapo ndio serikali huanza kuwashutumu vijana hao aidha kutumia madawa,au mengineyo lakini walikuwa ni vijana hao wako safi viwanjani hawakupewa umuhimu wowote kabla ya kuamua kufata njia mbaya sio takiwa.

Nadhani hivi sasa wakati umefika kwa wizara na vyama vinavyosimamia michezo nchini kuwasimamia na kuwaendelea vijana kabla ya Taifa kuingia katika hasara kwa vijana hao kuingia mitaani na kuanza uharibu kwa Taifa badala ya kulisaidia taifa.

Kwa hizi timu za vijana zinazoanzishwa kila mwezi pia sio sahihi kutokana na kuwa kila mwezi inabidi timu zinavunjwa ili kuanzisha timu nyingine, kuanzisha timu sio lengo la maendeleo bali lengo ni kuziendeleza timu zilizopo nchini ili ziweze kufikia katika hatua inayohitajika kitaifa na kimataifa.

Kutokana na mafuriko ya timu mpya kila siku hii inarejesha nyuma sana maendeleo ya soka nchini kwani kila siku inabidi kuanza tena upya badala ya kuendelea na ile iliyovunjwa kufikia katika kiwango kikubwa zaidi,
hii inatokana na kutokuwa na uongozi bora unaowasaidia vijana hao ili kuweza kufikia viwango vikubwa vinavyo takiwa kwa taifa letu.

Kutokana na wachezaji na viongozi wa timu hizo za vijana kuwa na wakati mgumu kwa kila upande kuanzia msaada kutoka wizara/vyama vya michezo na kutokuwa na wafadhili wa timu zao ndogo pamoja na timu kubwa kujichukulia wachezaji kutoka katika timu hizo bure na kutojali kuwa timu hizo hazina mapato wala mfadhili dhio hupelekea timu hizo kuvunjwa na hivyo ndio soka inavyodidimia kwenda chini.

Kutokana na kutowekwa sheria yoyote kwa timu kubwa ya daraja la juu inayochukua mchezaji aliechezea klabu yoyote ya watoto kwa mwaka mmoja,au zaidi ya mwaka mmoja inabidi ilipe kiasi fulani cha fedha kwa timu hizo za vijana kutoka na kutumia muda wao na gharama zao mifukoni mwao bila mfadhili au msaada wa serikali hivyo huwafanya viongozi wa timu za vijana kuchoshwa na masuala hayo kutoa wachezaji wao bure huku wao wakiwa wanajitolea tu kwa taifa katika kumjengea kijana kuwa msingi wa mwazo wa soka yake ambao ndio muhimu sana kwa kila mchezaji au elimu yoyote duniani.

Timu zote nchini zinashindwa kuanzisha timu za watoto kutokana na kuwa na gharama kubwa bila ya kuingiza kwa muda wao wote wanapokuwa na umri mdogo,
Suala ni je "mbona timu hizo hazioni kuwa wale wenye timu ndogo pia wanakabiliwa na yale ambayo wao hawawezi kuyafanya ya kuanzisha timu za watoto na hawaingizi kitu bali wanapoteza muda mwingi na gharama zao kuzalisha nyota ambao ndio wanazozitumikia timu zao tokea kuanzishwa kwa soka nchini"? .

Nadhani imefikia wakati sasa Serikali/vyama vya soka husika na kuanzisha sherika kwa mchezaji yoyote mwenye umri fulani kutoka timu fulani ya watoto alipiwe ada fulani kutokana na ada ya gharama za mafundisho kwa mchezaji huyo kwa miaka aliyokuwepo katika timu hio ndogo pia walipe ada ya uhamisho kwa klabu hio ndogo hii itawiana kidogo na kuwapa moyo wafundisha wa vilabu vya watoto kuweza kupata gharama za vilabu vyao kwa wachezaji wao na kuzitumia gharama hizo kwa kuwatengeneza vijana wengine.

Kama vilabu vikubwa vina uwezo kuchukua wachezaji kutoka nje ya nchi kwa beo ambayo wanapangiwa na ile timu anayotoka mchezaji,pamoja na gharama za mchezaji ,je inakuwaje kusiwe na ada za kumlipia mchezaji mdogo gharama zake za mafunzo alizokuwepo katika klabu ya watoto kwa miaka fulani aliyofundishwa na kugharimu sio tu posho ndogo ndogo pia gharama za chakula wakati wa mechi au kambi zao,usafiri,vifaa wanavyopewa kwa mazoezi na mechi,ni gharama ambazo inabidi zirejeshwe kwa vilabu husika ili kuweza kuwapa nguvu viongozi wao waweze kulisaidia taifa.

3) katika hatua nyingine ukiondoa hii ya vijana kwa upande wa vilabu vikubwa inabidi kila klabu ilazimishwe kuwa na timu za watoto 4 hadi 5 wenye umri mbali mbali,na vilabu hivi timu zao hizo ndogo zitachuana katika ligi kama vile timu zao kubwa zinavyocheza ligi. Aidha kila klabu itanufaika na kupata wachezaji wake kutoka katika klabu zao hizo ndogo hivyo kuepuka gharama za kununua wachezaji kutoka sehemu nyingine suala ambalo ni gumu kwa timu za Zanzibar kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na wafadhili,hivyo njia hii ya kuwa na timu zao wenyewe wataweza kuziba lile pengo la kununulia wachezaji na kuwalipa mishahara mikubwa kama vile wakiwa na wachezaji wenyewe wa timu zao ndogo.

Aidha Serikali/vyama vya soka husika vitoe sheria kwa kila timu itakayo sajiliwa katika daraja la 1,2,na 3 ni lazima wawe na timu 4 au 5 za watoto, hivyo moja kwa moja vile vilabu vya watoto vitajikuta vyote vimegawanyika katika mfumo wa timu hizo nchini,hivyo hakutokuwa na timu iliyozidi kuwa haina timu kubwa,timu kama hio ya watoto isiokuwa na timu kubwa ya kuiwakilisha na kuwafanya wachezaji wake kwenda moja kwa moja kuichezea timu hio inabidi wapeleke jina la na barua yenye sahihi ya mfadhili wao ambae ataweza kuifanya timu hio kuendelea kwa miaka fulani hadi kujitegemea wenyewe kuwa moja ya timu za madaraja ya juu ili kuepusha timu yoyote ya vijana kuvunjwa vunjwa ovyo kama ilivyo sasa hivi.


Kuwekwe sheria kutoka Wizara ya michezo/vyama vya soka husika kila timu inayomiliki uwanja ( uwanja wa ??????) ambzo timu hizo zipo katika madaraja matatu ya juu kabisa katika soka nchini inabidi uwanja huo utumike sambamba na timu zake ndogo ambapo kila timu inachagua ni timu ipi ya watoto kati ya zilizopo huko chini watazichukua kuwa timu zao,

Karibuni viwanja vya timu hizo vinatumiwa pia na timu za watoto hivyo wanaweza kukubadiliana kuwa moja kwa moja kuwa ni timu zao ndog, kwa timu za central na junior pamoja na juvenile baadhi yao zinaweza kuungana kuwa mfumo wa timu moja za madaraja hayo kujiunga na timu kubwa yenye uwanja wake hivyo kuzifanya timu hizo zote moja kwa moja kuwa wawakilishi wa timu yao kubwa.

Pamoja na manufaa ya kupunguza gharama kwa timu kubwa vilevile itavisaidia vilabu vya Zanzibar kuwa na mfumo mmoja sambamba na vilabu vya nchi zilizoendelea kisoka na hii ndio itakuwa mkombozi wa soka nchini. kwa mchezaji ambae atakuwa chini ya timu kubwa inayoiwakilisha timu zake za watoto kama akichukuliwa na timu nyingine akiwa na umri mgodo kabla ya kuiwakilisha timu kubwa kuwekwe ada ya malipo kwa timu hizo kubwa ili kuweza kufanya uhamisho kwa Scouting zao ziwe katika ubora ili kuondoa utata kuwa mchezaji huyo ni mdogo hivyo anaweza kwenda kiholela timu nyingine.

Kwa maana hio vilabu vikubwa vitanufaika na kuwatumia kuwatumia wachezaji wake wote wa timu ndogo katika ligi kama wakihitajia kufanya hivyo wachezaji hao wadogo  ambao usajili wake utakwenda sambamba na timu kubwa itaweza kutoa muundo mmoja wa mzuri wa hali ya juu kwa timu kubwa kuwatumia wachezaji wadogo,na wachezaji hao wadogo watapata nafasi ya ushindani wa kujiweka katika hatua bora sana katika soka hivyo kuinua na kutaifanya soka yetu nchini kuwa katika hali ya juu muda mfupi.

Kila mchezaji wa daraja la chini wa klabu anaruhusiwa kuchezea daraja la juu yake wakati wowote,kwa vile wote wamesajiliwa na timu ya klabu moja.

Kuwa na michuano ya timu za watoto za vilabu kutatoa sio tu msisimko wa mashindano hayo kwa vijana,bali kutaanza kuwajenga vijana huko chini mfumo wa ushindani kama walivyo wakubwa zao katika madaraja ya Primier League na madaraja mawili chini yake.

Nadhani kuna timu nyingi za vijana ambao wanajiendesha wenyewe,haitokuwa kazi kubwa kwao kujiunga na timu kubwa hivyo kuwa na uhakika wachezaji wao watakuwa wakipanda ngazi kutoka timu zao ndogo hadi kufikia daraja kubwa,isipokuwa viongozi wa timu hizo ndogo watahitajia nguvu za pamoja na wenzao wa timu kubwa ili kuweza kuunda nguvu moja ya uhakika ya kuweza kuleta mapinduzi ya soka kwa kila timu kujijengea kiwanda chake wenyewe cha wachezaji ambapo pia wataweza kuwauza kwa timu nyingine za nje ya nchi na kujitengenezea zaidi kipato katika vilabu vyao.

Nadhani hakuna klabu kubwa yoyote ambayo itakataa baada ya wachezaji wake wa kawaida iliowasajili kwa msimu kuweza kuwatumia wachezaji wake chipukizi wa timu zake ndogo katika ligi au mashindano mengine yoyote ya klabu hio kama sheria itaamua kfanya hivyo, timu za mataifa yaliyoendelea zinafanya hivyo na sisi pia hilo sio suala kubwa kama hatuwezi kulifanya, tumeona timu kubwa baadhi ya nchi kila mechi wanatia yosso mpya au hata nusu ya timu kuwachezesha wachezaji wadogo ili kuwapumzisha nyota wao wakubwa kutokana na aidha kukabiliwa na pambano kubwa mbele.

Mwisho kwa sasa vilabu vya watoto ambavyo viko katika hali nzuri ya kisoka inabidi kwa viongozi wahusika kuvichagua vile vinavyoanzishwa sasa na vile vilivyokuwa na viwango vizuri kutokuwa katika daraja moja ili kuokoa soka isiporomoke,
kama ni juvenile A ins timu kali,zile timu zilizo chini ya viwango ziwe Juvenile B,na zile zile zinazoanzishwa sasa zianzie kwa Juvenile C.

kwa mfano mshindi wa kwa kwanza wa Juvenile C atakwenda moja kwa moja Juvenile A kutokana na timu hii iliyoanzishwa kuonekena ni kali kulingana na uwezo itakaoonyesha tokea kuanzishwa kwake.
Washindi wa pili na watatu wa Juvenile C wakutane na washindi wa pili na wa tatu wa Juvenile B ili kuweza kuona kama kuna timu mbili zaidi kali zitakazo jumuisha kuongeza idadi ya timu za Juvenile A kuongeza timu kuwa na ushindani zaidi wa daraja hilo,

Bila ya hivyo timu zile kali za daraja hilo ukiziweka pamoja na timu inayoanzishwa group mitaani na kusajiliwa bila hata ya kuwa na uongozi,na pengine hakuna wafauatiliaji uongozi wa soka wa vyama madaraja ya chini unaopitia viwanjani kuangalia maendeleo ya vilabu hivyo kunaifanya timu hizo pengine kabla ya msimu kumalizika kuwa tayari zimezeeka na pengine msimu unaofata kutoonekana tena kiwanjani hivyo kuzaliwa tena timu mpya na hivyo kunapunguza nguvu na uwezo sawa na zile timu nzuri na kali za madaraja hayo hivyo kuzorotesha maendeleo ya soka nchini. hivyo ni kwa madaraja yote kutoka Juvenile,Junior na Central League.

Alimalizia mdau huyo kwa kusema, WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,UTALII, NA MICHEZO vitengo vyote hivyo vipo katika Wizara Moja na waziri mmoja na watendaji wake wote.
Lakini zinaonekana kama hazina uhusiano wa karibu katika utekelezaji au utendaji wao,inaonekana kila wizara inakuwa na kazi zake bila ya kushirikisha wizara nyingine.

Sidhani kama kuna uhusiano wowote kati ya Michezo au utamaduni na Utalii?wakati zote ni wizara moja,kwanini michezo kama karata,gololi,keram,dama hazipatiwi wasimamizi wao zikawa katika sura ya kiushindani ligi yao kama michezo ya soka na netiboli na kupatiwa sheria zao na kumbi zao na kuwavutia watalii kushiriki au kulipia nauli za viingilio kuona michezo ya utamaduni wetu?

Mchezo wa Gololi mbona ni sawa na mchezo wa CURLING unaoshirikisha mataifa ya duniani kama kombe la dunia na Olympic aliongeza mdau huyo,dhumna ni mchezo wa kuwashirikisha wachezaji kama  ligi huku wachezaji wao wakivaa jezi na makocha wao kumpata bingwa wa nchi,mchezo wa ngómbe ni mchezo maarufu kwa watalii kama wataweza kuupatia kiwanja chao na kuvutia watalii kuingia kwa viingilio na ni burudani tosha kwa watalii hao pia kutoa wachezaji wa timu ya taifa ya ngómbe ya Zanzibar kama michezo mingine ilivyo na kuwa na ligi yao sawa na ligi ya mchezo wa Kiumbizi na kadhalika.

Narejea kwa kusema inaonyesha wizara ya michezo,utamaduni,utalii na habari hazifanyi kazi moja kwani lengo letu kubwa ni vyombo hivyo kushirikia kama wizara ya habari kuandaa kipindi maalumu kwa ajili ya kuonyesha matukio ya soka kwa kila wiki yanayoshirikisha timu za watoto nchini,pia kutoa habari zao kila siku katika magazeti nchini hivyo kuipa sura wizara ya habari kuwa ipo pamoja na michezo kiutendaji.

Wizara ya Utalii kwanini kama Serikali imeamua kutaka Kufufua soka nchini wizra hio isibuni mbinu kama kuongeza dola moja kwa kila mtalii anapoingia nchi au anapotoka au kuongeza nusu dola kwa kila mtalii anapopangisha malazi yake katika hoteli za Zanzibar na Fedha hizo kutumika kwa michezo ya Zanzibar pamoja na utamaduni kwani sehemu hizo zinaonekana kutokuwa na kipato kutokana na kukosa wawekezaji?

Nadhani wizara ya Utalii haionekani kama inafanya kazi na wizara ya michezo au utamaduni,hivyo wizara kama hizo zinakuwa zipo kivuli tu na sio kiutendaji. kama kutakuweo mpango mzuri wa kupada ada kidogo kutoka utalii na kuwekeza katika soka ya Zanzibar basi ni wakati mzuri hivi sasa kufufua timu zote za taifa za vijana za Zanzibar kuanzia Juvenille hadi U20,

Aidha kunaweza kuwa na mpango maalum wa matembezi kwaajili ya kuchangia soka ya Zanzibar matembezi ambayo yawashirikishe viongozi na raia wa nchi pamoja na kuwaalika watalii wote waliopo nchini kushiriki matembezi hayo marefu pengine kutoka wilaya ya mjini magharibi hadi makunduchi yakiwa matembezi yenye sura ya kimataifa,viongozi wanaweza kupokezana baadhi ya kilomita na siku ya pili anaweza kuja kiongozi mwingine kumpokea na kuendelea na matembezi hayo na kama hivyo hadi kufikia mwisho wa matembezi ambapo atafutwe mdhamini wa kutoa zawadi kwa washindi 10 wa mwanzo wa jumla wa mashindano hayo watakaoshinda kila jua linapotua kwa muda wa siku 4 au 5.

Mpango kama huu nchi njingi zinafanya na kupata fedha nyingi na pia kufanya biashara nyingi katika vituo wanavyosimama  kwa mapumziko jioni ile hivyo pia kuvinufaisha vijiji vinavyopangwa washiriki kupumzikia,
mpango kama huo unaweza kuanza kwa watalii waliokuwepo nchini na kila mwaka utazidi kukua na mwisho kuwaalika washiriki kutoka pande zote duniani huku Zanzibar ikitangaza utalii wake kwa kutumia matembezi hayo marefu nchini yatakayokuwa na sura ya kimataifa na yakuvutia na kuweza kupata fedha kwaajili ya michezo na utamaduni nchini na hii itakuwa ni kama miundo mbinu ya kusaidia michezo Zanzibar.

timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 13 itawashirikisha wale wachezaji wenye vipaji vikubwa katika madaraja hayo kwa mikoa yote ya unguja na pemba,na wachezaji hao ndio watakao kuwa wakitunzwa kwa lengo la kuwa ndio watakaokuwa wachezaji wa taifa wa U14 mwakani,na wale wa U14 watakwenda juu kwa mpango huo hadi U15 na wale wa daraja hilo watachupa juu hadi U16  mpaka kufikia U19 ambapo hapo tayari watakuwa ni wachezaji wa kutumikia timu ya Taifa ya vijana wa Zanzibar na timu kubwa ya Taifa.

Tmu hizo za Taifa za vijana ziwe zinapatiwa mechi kila mwisho wa mwezi na timu zilizo katika form nzuri katika madaraja yao,au kupambana na timu zilizowazidi daraja ili kutoa na kuwajenga kiupinzani,sambamba na kucheza mechi za kirafiki kila katika kalenda ya fifa ya mechi za timu za taifa hivyo itaanza kuwajenga wachezaji tokea umri mdogo kalenda hizo na kuanza kujipanga kimaendeleo kama wachezaji wadogo wa kimataifa wa baadae,pia kuwaombea mialiko ya timu za watoto kutoka nje kuja nchini au vijana wetu kwenda nje.ikiwezeka kuwe na mazungumzo kuwa na mpango wa kuanzisha mashindano ya timu za taifa za vijana kwa nchi za visiwa vinavyoizunguka bara la Afrika kwaajili ya kuwawezesha na kuwakuwa vijana wa visiwa hivyo sambamba na kushirikia kiutalii kati ya visiwa vya nchi hizo.
Lakini mpango huo utakuwa pale wizara ya utalii na habari zitakaposhirikiana kuweza kuwatangaza na pia kuandaa mpango wa kuipati kipato cha kuendelea wizara ya michezo ili iweze kusimamia mpango huu,
pamoja na hayo wadau wafanya biashara wajitokeze ili kuweza kuanza mpango huo wa vijana mara moja ili Zanzibar iweze kwenda sambamba na soka kwa nchi zilizoendelea duniani,na kwa mpango huo wachezaji wengi wataweza kuuzwa nje na nchi itanufaika na mapato ya wachezaji hao pamoja na maendeleo ya soka nchini.

Wafanya biashara wajitokeze kutangaza biashara zao kwa kuwatumia vijana wenye vipaji katika nembo zao za biashara ili vijana hao wanufaike na kuzidisha uwezo wao zaidi kwaajili ya kulisaidia taifa hapo baadae,

Alimalizia mdau huyo kwa kutoa maelekezo yake kwaajili ya kufufua na kuimarisha soka Zanzibar
Nashukuru sana kwa mchango huo nadhani unaweza labda kutoa picha fulani ambayo labda kule nyumbani wanaweza kuyafanyia kazi na kufufua soka nchini kama ambavyo viongozi wanataka kila Raia wake ahusike katika mchango wake wa kuleta maendeleo ya kufufua soka nchini.