WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 5 May 2012

SIMBA MABINGWA WA SOKA 2011/2012

Simba imetwaa ubingwa wa soka wa Vodacom Primier League Tanzania Bara 2011/2012  hata kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizika, baada ya jana Mtibwa Sugar kuifunga Azam mabao 2-1 mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa jana ulifanyika kutokana na uamuzi wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuamua urudiwe baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Jumatatu wiki iliyopita Uwanza wa Chamazi kuvunjika katika mazingira ya utata kutokana na Mtibwa kugomea penalti ya dakika za majeruhi.

Kamati ya Ligi ya TFF iliipa ushindi wa mabao 3 na pointi tatu Azam kwa vile Mtibwa iligomea mchezo, lakini timu ya African Lyon ambayo pia inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ilikata rufani kwa Kamati ya Nidhamu ikitaka Mtibwa ishushwe daraja kwani kanuni zinataka timu inayogomea mchezo ishushwe daraja, lakini Kamati ya Nidhamu iliagiza mchezo huo urudiwe, ndipo ukapangwa jana.

Kutokana na kipigo hicho cha jana, Azam imebaki na pointi zake 53 kwa michezo 25 iliyocheza ikiendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi nyuma ya Simba inayoongoza ligi ikiwa na pointi 59.

Hata kama Azam itashinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar kesho ihaitaweza kufikia pointi za Simba, hivyo kwa kufungwa kwake jana kumeipa Simba ubingwa katika mazingira rahisi. Simba imebakisha mchezo mmoja dhidi ya Yanga kesho, ambao hata kama itafungwa haitaathiri ubingwa wake.

Katika mchezo wa jana, Mtibwa walianza kuhesabu bao lao la kwanza dakika ya 21 lililofungwa na Awadhi Issa kwa shuti baada ya kugongeana vyema eneo la hatari.

Kuingia kwa bao hilo, kuliifanya Mtibwa kuzidisha mashambulizi langoni mwa Azam, lakini washambuliaji wake Vicent Brnabas na Thomas Maurice walishindwa kutumia nafasi walizozipata.

Juma Abdu aliifungia Mtibwa bao la pili dakika ya 60 kwa shuti kali la mpira wa adhabu, baada ya kudondoshwa eneo la hatari wakati akielekea langoni.

Azam walijitutumua na kupata bao la kufutia macho lililofungwa na John Bocco kwa mkwaju wa adhabu ndogo dakika ya 69 baada ya Bolou Kipre kudondoshwa eneo la hatari.

Katika dakika za majeruhi mchezo huo ulilazimika kusimama kwa dakika kadhaa baaada ya golikipa wa Mtibwa, Deogratius Munishi kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano iliyozaa nyekundu.

Munishi alipewa kadi hiyo baada ya kukaa kwenye nyavu za goli huku akichelewasha muda wa kupiga mpira na hivyo mwamuzi akamzawadia kadi hiyo.

Hilo ni taji la 18 kwa Simba kulitwaa katika ligi hiyo tangu ianze mwaka 1965, lakini baada ya ligi hiyo kufanyiwa marekebisho mwaka 1982 ikichezwa kama Ligi Daraja la Kwanza na baadaye kujulikana kama Ligi Kuu Tanzania Bara ni taji lake la kumi.

Watani wa jadi wa Simba timu ya Yanga yenyewe imeshachukua taji hilo mara 23 tangu michuano ianze mwaka 1965, lakini imechukua mara 15 tangu mfumo ubadilishwe kuanzia mwaka 1982.