WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday, 26 August 2012

Kisc Academy kufanya kazi pamoja na Orange Football Academy

 
KATIBU Mkuu wa timu ya Kisc Academy Hashim Ali Ahmada (Kibabu), amejivua uenyekiti wa Real Shangani pamoja na pia uongozi wa timu ya New Academy.

Kibabu amechukua hatua hiyo ili aweze kushika wadhifa wa kuiongoza timu ya Kisc Academy, ambayo msimu huu wa ligi, imeomba kutumia jina la Orange Academy.

Tayari Kibabu ameshawasilisha barua Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Wilaya ya Mjini, akieleza kuwa, kushika uongozi katika sehemu nyingi, ndio mwanzo wa migogoro inayochangia kurejesha nyuma maendeleo ya michezo.

“Vilevile, napenda kujiondoa katika nafasi zote za uongozi, upambe na ushawishi kwa timu ya New Academy na Real Shangani. Maamuzi haya ni hiyari yangu na kwa moyo safi napenda ieleweke na itambulike hivyo”, alisema Kibabu kupitia barua yake aliyoituma kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Central Wilaya ya Mjini.

Wakati huohuo, wachezaji wa Orange Academy wameanza rasmi mazoezini jana Agosti 25/08/2012 saa 10:00 jioni katika uwanja wa Mao Dzedong kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa mwaka 2012/13..