WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday, 24 November 2012

AZAM F.C YAMNASA NYOTA WA O.F.A SEIF ABDALLA "KARIHE".

Azam yasajili watatu wapya, yarudisha wawili

(aliekuwa kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Stewart Hall akiwana na wachezaji wa timu hii Seif Abdalla "karihe"wa O.F.A katikati jezi nyeupe akiwa katika kikosi hicho kwa mara ya kwanza hapo akiwa na umri wa miaka 17 akitokea katika kikosi cha O.F.A).

Baada ya kushindwa kupata haki zake na makubaliano kutoka kwa klabu ya Ruvu Shooting Star klabu ambayo imemsajili nyota wa kimataifa kinda wa Oranje Football Academy ta Zanzibar bila ya uhamisho wowote  unaotakiwa kwa mujibu wa sheria za soka nchini na zile sheria za Caf pamoja na Fifa.

Kwa mujibu wa uongozi wa kituo hicho cha kukuza soka nchini kinaamua sasa kiweka hadharani habari hii kabla ya kuanza kuipeleka klabu hio ya ligi kuu ya nchini katika vyombo vya sheria ili kuweza kupata haki zake kwa mujibu wa sheria.

Oranje football academy inavyo vielelezo vyote vya njota wake huyo Seif Abdalla "karihe"(kumbukumbu pitia katika tovuli yetu hii)ambapo imemlea na kumfikisha hadi kuchaguliwa kuwa mchezaji wa kwanza wa kituo hicho kuchaguliwa kuchezea timu kubwa ya taifa ya Zanzibar pamoja na ile ya vijana wa Tanzani wenye umri wa miaka 17.

kutokana na gharama nyingi kituo chetu ilizozitumia kumlea kinda huyo kama ambavyo inafanya kwa wengine nilazima kituo hicho kipate malipo yote kutoka kwa timu hio ya Ruvu Shooting Star kwa miaka miwili iliyomchukua nyota huyo bila ya malipo huku mchezaji huyo akiwa katika usajili pia katika blabu ya O.F.A katika msimu wake wa kwanza hivyo kufanya usumbufu mkubwa kwa kituo hicho katika usajili wake.

Baada ya kuwatafuta mara kadha viongozi wa timu hio ya Ruvu inaonekana uongozi huo umeamua soka kuigeuza katika sheria za kijeshi hivyo mchezaji huyo wakidhani ni mali yao bila ya kuwa na timu aliyotokea ambapo umri wake wote amekuwa akilelewa katika kituo hicho.

Kutokana na habari tulizozipata kutoka katika gazeti la mwananchi (nakala ip hapo chini) imeonyesha kuwa aliekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar Stewart Hall ameamua kumtwa mshambuliaji wake huyo nyota ambae hadi sasa amepachika mabao 5 katika ligi kuu ya bara ili kujiunga na Azam f.c

Kutokana na kuwa nyota huyo hadi leo hakufanyiwa uhamisho wowote kutoka kwa Oranje Football Academy uongozi wa kituo hicho utaishitaki klabu hio ya Ruvu Shooting Stars kwanza kumtumia mchezaji hiyo bila uhamisho na klabu yake ya zamani, pili kujaribu kumuuza nyota huyo wa kimataifa kwa udanganyifu kama ni mchezaji wao halali huku wakijua mpaka sasa ni mali ya Oranje Football Academy.

Wakiongea na Tovuli ya kituo hichi kinachimilikiwa na O.F.A viongozi wa Academy hii changa amabyo imejipanga kuleta maendeleo nchini na kuwa haina mradi wowote inaoingiza mapato kama vilabu vya madaraja ya juu ambapo uongozi umekuwa ukitumia muda wake na kupoteza gharama nyingi za kuwalea vijana hao ili kuleta maendeleo nchini na leo vilabu vikubwa vinakuja kuchukua wachezaji bure.

Hili halitowezekana hata siku moja,mpira una sheria zake za uhamisho, hivyo Azam F.c katika uhamisho wake itahitajika ilipe uhamisho wake wote kwa Oranje Football Academy  itakaokubaliana na Ruvu Shooting Stars kumuhamishia nyota huyo ambae sio mali mchezaji wao halali hadi sasa hivi.

Waliendelea viongozi hao kwakusema Ruvu waache waonyeshe mchezaji huyu "karihe" amemchukua kutoka klabu gani? na uhamisho wake? kwani mchezaji huyo hakuwa huru kama pengine walidanganya kwa TFF, tunao usajili wa miaka yote ya karihe katika academy yetu sambamba na msimu uliopita ambapo mara tuliona pia amesajiliwa ruvu na tukadhani wenzetu wagelipenda mazungumzo na sisi ili tuyamalize,

sasa leo hii wanataka kumuuza mchezaji chipukizi tena wa kimataifa ili faida iwe yao, kwanini wasitengeneza timu zao za watoto za kuwalea na baadae kuwauza kama ni rahisi kwa vilabu vikubwa kufanya hivyo,walimalizia viongozi hao kwa hasira.

Lengo ni kumjenga nyota wetu na uongozi pia unatoa onyo kali ambapo tayari baadhi ya vilabu vikubwa nchini pia ina nyota wake ambapo hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa na uongozi wake,hivyo kama sio rahisi vilabu kuweka timu zao za watoto,
kwanini wasifanye haki kwa wale walioamua kuwalelea nyota hao kitu ambacho kinawashinda timu kubwa zenye uwezo nchini?

nakala hapo chini kwa hisani ya tovuli ya mwananchi.
......................


AZAM FC ipo kwenye mpango wakuchukua straika mwingine kutoka Ivory Coast lakini tayari imemnasa beki kisiki wa Prisons, David Mwatika na washambuliaji, Seif Abdallah wa Ruvu Shooting na Uhuru Suleiman wa Simba.
Pia imewarudisha kundini nyota wake wa zamani, Malika Ndeule aliyekuwa ametolewa kwa mkopo kwenda Mtibwa Sugar na Omari Mtaki aliyekuwa African Lyon. Pia Azam inaendelea na mazungumzo na wachezaji wawili wa Sofapaka ambao ikishamalizana nao itakaa chini kuamua wapi pa kupangua.

Usajili huu ni mapema kabisa kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao kitakachowakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho mapema mwakani pamoja na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Kiongozi wa juu wa klabu ya Azam amesema: "Tayari tumemalizana na wachezaji hao watatu, Mwatika, Seif na Uhuru kwa ajili ya kuboresha kikosi chetu kwenye mzunguko wa pili wa ligi na michuano ya kimataifa.
"Tunaendelea kufanya mazungumzo na mshambuliaji kutoka Ivory Coast kwa ajili ya kuboresha safu ya ushambuliaji. Kipre Tchetche ndiye anafanya mpango kwa maana ndiye anamfahamu vizuri," alisema kiongozi huyo.
"Pia tumewarudisha, Malika na Mtaki ambao awali tulikuwa tumewatoa kwa mkopo klabu za Mtibwa Sugar na African Lyon."

Kiongozi huyo alidokeza kuwa, klabu hiyo inamtolea udenda, Emmanuel Okwi wa Simba hata hivyo hawana uhakika wa kumnasa ndiyo maana wameanza mazungumzo na Muivorycoast huyo.

(Seif Abdalla "karihe" watatu kushoto katikati akiwa na kikosi cha Tanzania U17 kilichoshiriki michuano ya Challenge cup nchini Sudan).
Mwanaspoti ilizungumza na Seif ambaye yumo katika kikosi cha Zanzibar Heroes kilichotarajiwa kwenda Uganda juzi Alhamisi usiku na hakutaka kufunguka moja kwa moja ila alisema:
"Ni mapema mno kuzungumzia usajili, mambo yakiwa tayari nitakufahamisha."

(Seif Abdalla "karihe" wa kwanza kulia akiwa na kikosi cha O.F.A katika mazoezi uwanja wa mao tse tung).