WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday, 3 December 2012

AZAM YATINGA RUVU KUINASA SAINI YA SEIF ABDALLA WA O.F.A


 

Kutokana na kitendo cha makusudi kinachofanywa na Uongozi wa Ruvu Shooting Star ya kutaka kumuuza mchezaji Seif Abdalla wa Orange football academy ya Zanzibar iliyomlea mpaka kufikia kiwango alichonacho sasa uongozi wa kituo cha O.F.A inatarajia hivi karibuni kuifikisha klabu ya Ruvu Shooting Stars TAKUKURU kwa kumsajili mchezaji wake bila uhamisho wowote kwa muda wa misimu miwili sasa na harakati zao wanazozifanya za kutaka kumuuza kwa Azam F.c.
tunaushauri uongozi wa Azam kuongea na uongozi wa O.F.A ili kumtwaa nyota huyo chipukizi baada ya kwenda kwa Ruvu ambapo Rungu la adhabu litawaangukia hivi karibuni kwa aidha kumsajili nyota huyo wa kimataifa bila ya uhamisho wowote kutoka kwa O.F.A, (kumbukumbu za nyota huyo fatilia zaidi kupitia katika blog yetu hii)baadae waombeni Ruvu watoe kumbukumbu zao mchezaji huyo wametwaa kutoka timu gani?kwa uhamisho gani? au ametokea katika timu zao za watoto wa Ruvu? nadhani hawatopata jibu lolote la kujibu.
Hivyo uongozi wa O.F.A hautotaka mazungumzo yoyote na Ruvu Shooting ambayo walikuwa wakikwepa kuzungumza na uongozi wetu kwa muda wa misimu miwili sasa tunawaomba viongozi wa Ruvu Shooting Stars wajipange vizuri kuzungumza na TAKUKURU kwani hakuna kiongozi hata mmoja wa O.F.A atakaekuwa tayari kuzungumza nao.

hatilia zaidi nakala ya habari kutoka kwa gazeti la mwanchi la tarehe 03-12-2012 hapo chini.
..........................................................................................................................................

AZAM FC imeanza kumsaka mshambuliaji chipukizi wa Zanzibar na Ruvu Shooting,
Self Abdallah ili kuipata saini yake.


Mshambuliaji huyo katika mzunguko wa kwanza alifanikiwa kuzifungwa Yanga, Simba na Azam kila alipokutana nazo.

Meneja wa Azam, Patrick Kahemela alisema kuwa tayari wamekwishawasilisha ofa yao kwa uongozi wa Ruvu na wamesema wapo tayari kuongeza dau ili kumpata mshambuliaji huyo.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alithibitisha kupokea barua ya Azam ya kumtaka mshambuliaji huyo.

Alisema watatoa jibu baada ya mazungumzo yao na uongozi wa benchi la ufundi chini ya kocha Charles Mkwasa kuhusiana na suala hilo.

Alisema kama kocha ataridhia Abdallah aondoka katika kikosi chake kwa sasa basi wao hawatakuwa na pingamizi.
Kama Abdallah atafanikiwa kutua Azam atakuwa ni mchezaji wa pili baada ya Uhuru aliyechukuliwa kutoka Simba kwa kubadilishana na beki George Owino.

(Mshambuliaji hatari wa O.F.A  Seif Abdalla "karihe" akiwa katika mazoezi uwanja wa mao tse tung nje)

 (Seif Abdalla akimiliki mpira moja katika mazoezi ya o.f.a)


pichani Nyota wa timu ya taifa ya Tanzania u17 akifanya mazoezi ya viungo na o.f.a.


Seif Abdalla nyota wa o.f.a wa kwanza kulia akimsikiza maelekezo ya mwalimu katika uwanja wa mao tse tung.

Nyota wa kimataifa wa O.F.A Seif Abdalla akiwa katika mapumzika ya timu yake ya O.F.A.

Aliekuwa kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Stewart Hall akiwapa maelezo wachezaji wa timu hio Seif abdalla mbele yake jezi nyeupe akiwa katika kikosi hicho kwa mara ya kwanza baada ya kocha hicho kuvumbua kipaji cha Seif kutoka Orange Football Academy.

Seif abdalla akiwa katika mazoezi na timu ya taifa ya Zanzibar katika uwanja wa aman baada ya  kuitwa kwa mara ya kwanza na Stewart Hall ambae hivi sasa ameonekana kutaka kumpeleka nyota wake hio kipaji alichokivumbua kutoa O.F.A kujiunga  Azam F.C.

Nyota wa Oranje Football Academy katika picha ya pamoja na kocha Bo Nilson kutoka Sweden mara baada ya kumalizika kwa mazoezi maalum (nyota Seif Abdalla wa sita kutoka kushoto/kulia walio simama)
 
Seif Abdalla wa pili kushoto mbele waliopiga magoti katika moja ya ubigwa waliotwaa na O.F.A

Nyota wa kimataifa ya Tanzania Nizar Khalfan akiwa na nyota chipukizi wa Tanzania Seif Abdalla mara baada ya mazoezi ambapo Nizar alikitembelea kituo chetu hicho cha O.F.A kabla ya mechi ya kirafiki dhidi ya Brasil 2010.


 Seif Abadalla akibadilishana mawazo na Nizar Khalfan mara baada ya mazoezi.
.....................................
Kituo cha Oranje Football Academy kinawaomba uongozi wa Ruvu Shooting Stars kujitayarisha na vielelezo vyao ikiwemo mikanda ya Video itakayowasaidia katika ofisi za TAKUKURU pamoja na MAHAKAMANI ili waweze kushinda vita hii ambayo inaonekana itakomesha vitendo vya baadhi ya vilabu vikubwa kuvikandamiza vilabu vidogo vinavyopoteza jasho lao kuwalea vijana na baadae kuwatwaa bila uhamisho wakitumia ubabe usiokuwa na maana yoyote badala ya kuhamisha vijana katika vilabu vyao kihalali.

TUNATARAJIA HILI ITAKUWA NI SOMO KALI SIO TU KWA RUVU SHOOTING BALI KWA VILABU VYOTE VIKUBWA VINAVYOVINYANYASA VILABU VIDOGO, KWANI BILA VILABU VIGODO HAKUNA VILABU VIKUBWA VINGEISHI NCHINI.