WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Sunday 2 December 2012

Tanzania Bara yaiangamiza Somalia 7-0

Mabao matano yaliyofungwa na mshambuliaji, Mrisho Ngassa na mawili kutoka kwa John Bocco. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao ulishuhudia, Tanzania Bara ikiizamisha, Somalia kwa mabao 7-0, kocha msaidizi wa timu hiyo, Slivester Marsh amesema wamefurahishwa na matokeo hayo japo wengi walikata tamaa ya kuona timu hiyo ikitinga hatua ya robo fainali. ” Ilikuwa ni mechi ngumu kwa upande wetu, tulionekana kama tusingefuzu kwa hatua ya robo fainali. Tunashukuru Mungu na tuna imani tunaweza kufanya vizuri zaidi” alisema, Marsh.


Ngassa, alitumia dakika 90 mchana wa leo kufunga bao lake la kwanza katika michuano, na kufunga mengine manne na kuwa kinara wa mabao katika michuano hiyo. Alifunga mara tano, uku mshambuliaji ‘ patna’ wake, Bocco, akifunga mabao mengine mawili na kufikisha mabao manne katika michuano inayoendelea ya Tusker Challenge Cup, uko, Uganda. Wawili hao, Ngassa na Bocco wamekuwa na wakati mzuri katika michuano hiyo na sasa wapo juu katika orodha ya wafungaji bora. Ngassa ana matano n ndiye anayeongoza, uku Bocco, akifuatia na mabao yake manne.

Katika mchezo wa leo, wachezaji, Edward Christopher, Athuman Idd ” Chuji” na Ramadhani Singano, walipata nafasi ya kucheza mchezo wao wa kwanza. Watatu hao waliingia kwa wakati tofauti katika kipindi cha pili, Edo, alimpokea, Bocco, kisha, Chuji akaingia mahali kwa Frank Domayo na Singano, mahali kwenye nafasi ya Salum Abubakary. Katika mchezo mwingine, timu ya Taifa ya Burundi, iliifunga, Sudan Kaskazini, bao 1-0, na kuwa vinara wa kundi kwa kufikisha pointi tisa, tatu juu ya zile za Stars.