WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 22 December 2012

Wekezeni soka kwa vijana-Kikwete



NCHI nyingi zilizopiga hatua katika medani ya mchezo wa soka na michezo mingine, kiini chake ni uwekezaji katika kutafuta, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wadogo.


Leo hii tuna mifano mingi ya nchi hizo zinazothibitisha ukweli wa kauli hii. Mafanikio yao katika michezo yamekuwa maradufu, wanakula faida ya uwezekaji kwa vijana.

Tumewahi kusema mara nyingi, na leo tunakumbusha tena kama alivyokumbusha Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki hii wakati alipofanya mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam na mmiliki wa klabu ya Sunderland.

Viongozi wa klabu ya Sunderland, miongoni mwa timu kongwe zinazocheza Ligi Kuu England, wamekuja nchi kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii na michezo, hususan soka.

Katika kuonyesha kuchoshwa na kudorora kwa michezo nchini, Kikwete alisema sababu kubwa ni ukosefu ubunifu na udhaifu katika kupanga na kutekeleza mikakati ya uwekezaji kwenye soka la vijana.

Alisema, uwekezaji kwa vijana ndiyo chimbuko la mafanikio katika michezo, lakini ameshangazwa na jinsi viongozi wa michezo nchini wanavyoshindwa kutilia mkazo suala hilo.

Rais Kikwete alisema, tatizo kubwa la kushindwa kupiga hatua soka la Tanzania, ni uwezo mdogo wa uongozi kuanzia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mpaka klabu.


Uwezo huo mdogo wa viongozi wa michezo, Rais Kikwete ameutafsiri kama kitovu cha kukosa mwamko wa kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana, na badala yake hoja za msingi zisizo na tija ndizo zilizowekwa mbele.

Alishangazwa namna viongozi wa michezo nchini wanavyotumia muda mwingi kunyang'anyana wachezaji, ambao huja kuwatumia muda mfupi kabla ya kuwabwaga, wakati muda huo wangeweza kuutumia kuwajenga vijana kimichezo.

Pia, mkuu huyo wa nchi alikumbushia jinsi Serikali yake ilivyojitahidi kuleta makocha wa kigeni na yeye mwenyewe kuwalipa, lakini hatimaye ameangushwa na utendaji wa TFF.

Kama tulivyosema awali, tunatumia fursa hii tena kuunga mkono kauli ya Kikwete ya kutaka viongozi wa michezo nchini kuamka na kuanza mikakati ya kuwekeza kwenye soka la vijana.

Alichosema Rais Kikwete ni sahihi, na ndiyo maana siku zote wadau wamekuwa wakipiga kelele namna ya kuwa na mipango mizuri ya kuwaendeleza vijana wenye vipaji kwa faida ya nchi baadaye.

Tunaamini, kama wanavyoamini wengine kuwa, msingi wa mafanikio katika michezo, lazima uwe na mwanzo wa uwekezaji kwa vijana wadogo ambao baadaye huja kuwa lulu kwa taifa.

Haipo sababu tena ya kuendelea kugombea wachezaji ambao huja kutumika muda mfupi wakati kuna fursa ya kuwaandaa wachezaji vijana watakaokuja kutumika muda mrefu kwa maendeleo ya nchi.

TFF inapata msaada wa kifedha kila mwaka kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf), na sehemu ya fedha hizo hutumika katika programu ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana wadogo.

Pamoja na mikakati na nia nzuri ya kukuza vipaji kwa vijana wadogo inayofanywa na TFF, bado hatuoni kama juhudi hizo zinaweza kuelekezeka mbele ya wadau na wapenzi wa michezo na ndiyo maana hata Rais Kikwete aliamua kuzilizungumzia suala hilo.

Tungependa kuishauri TFF, vyama vya michezo na wadau wote kuanzisha mjadala wa kitaifa kuhusu uwekezaji katika soka la vijana, ili kila atakayeguswa achangie kwa uwezo wake.

TFF kama taasisi yenye mamlaka ya kusimamia na kuratibu mchezo wa soka nchini, haiwezi kufanya kazi hiyo peke yake hivyo itahitaji nguvu ya wadau wengine ili kuweza kuitekeleza kirahisi kauli ya Rais Kikwete.

Kama wengi wanavyosema, mbizo zenye baraka huanzia nyumbani, basi kwa maana hiyo, mwanzo wa changamoto hii ya kuwekeza kwenye soka la vijana ianzie kwa wasimamizi wa soka, ambao ni TFF.

Tunatambua kazi hii siyo rahisi kuitimiza, inahitaji fedha, muda na michango ya wadau na wapenda michezo. Tunaamini kama kutakuwa na mjadala wa kitaifa wa kuhamasisha uwekezaji soka la vijana mafanikio yanaweza kupatikana