WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Thursday 30 May 2013

Raza:Nakuja kuifutia Zanzibar aibu kisoka

Ataka ZFA iache sumu ya kubaguana kimaeneo

Na Salum Vuai, Maelezo

Mara baada ya kuchukua fomu za kutaka kugombea nafasi ya urais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ibrahim Dharamsi Raza, amesema dhamira yake kuu ni kuiondeshea Zanzibar aibu inayotokana na kushuka hadhi kisoka.Raza aliyechukua fomu hiyo jana katika ofisi za Kamati ya Uchaguzi ya ZFA iliyoko uwanja wa Amaan, alisema hafurahishwi na kuzorota kwa mchezo huo, hali inayowakimbiza mashabiki viwanjani.Akijibu masuala ya waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hiyo, Raza aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa mamlaka za michezo ikiwemo Makamu Mwenyekiti wa ZFA (1995-2000), alisema soka la Zanzibar limekosa uongozi makini na wenye uchungu wa kuliokoa."Inasikitisha kuona ni watu wachache sana wanaokwenda kuangalia mechi za ligi siku hizi, tafauti na zamani ambapo viwanja vya Amaan na Mao vilikuwa vikijaa na watu wakifurahika", alisema Raza.


Alisema iwapo atafanikiwa kushinda katika kinyang'anyiro hicho, anakusudia kushirikiana na viongozi wenzake na wadau wote wa soka nchini, kupanga mikakati madhubuti ili wanamichezo warejeshe imani kwa ZFA ambayo imepotea kutokana na uongozi usiojali maslahi ya umma na kuweka mbele ubinafsi. Aidha, alisema lengo jengine ni kuhakikisha ZFA inaimarisha uhusiano wake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na hivyo kudai mgao na haki zake zinazotokana na misaada ya FIFA kupitia mgongo wa TFF.Mgombea huyo alisema, uongozi wake utakuwa wa pamoja kati ya Unguja na Pemba, akieleza kuwa bila ushirikiano kati ya pande hizo maendeleo yatakuwa ndoto.Uchaguzi mdogo wa ZFA kujaza nafasi ya urais iliyoachwa wazi na Amani Ibrahim Makungu aliyejiuzulu mwishoni mwa mwezi Januari, unatarajiwa kufanyika Juni 8, mwaka huu katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani.