WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Monday 27 May 2013

MUDATHIR YAHYA WA O.F.A ATINGA SUTI NZITO NA KUPAA KUELEKEA ADDIS ABABA


KIUNGO MKALI WA ORANGE FOOTBALL ACADEMY MUDATHIR YAHYA YUPO JIJINI ADDIS ABABA KWA KAMBI NGODO YA TIMU YA TAIFA STARS AMBAYO HAPO TAREHE 02-06-2013 ITACHUANA NA SUDAN KATIKA PAMBANO LA KIRAFIKI.

SIKU INAYOFUATA STARS ITAELEKEA KATIKA MJI WA MARRAKESH,MOROCCO TAYARI KWA PAMBANO LA KUTAFUTA TICKET YA KUFUZA KATIKA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA YATAKAYOFANYIKA NCHINI BRASIL MWAKA KESHO.
KIUNGO HUYO MKALI AMBAYE KWA SASA YUPO AZAM F.C YA JIJINI MPAKA SASA NI MALI YA KITUO CHA KUKUZA SOKA KWA VIJANA NCHINI CHA ORANGE FOOTBALL ACADEMY SAWA NA SEIF ABDALLA "KARIHE"AMBAE AZAM IMEMSAJILI MSHAMBILIAJI HUYO KUTOKA RUVU SHOOTING (AMBAO KAMA AZAM WOTE KWA PAMOJA HAWAKUWALIPIA NYOTA HAO UHAMISHO WA AINA YOYOTE KUTAKA KWA KITUO HICHO VILEVILE UHAMISHO WOWOTE KUTOKA KWA CHAMA CHA SOKA CHA CENTRAL LEAGUE NA KILE CHA ZFA ZANZIBAR)

KUTOKANA NA SHERIA ZA FIFA MCHEZAJI YOYOTE KIJANA ANAECHUKULIWA NA KLABU YOYOTE INATAKIWA KULIPA MALIPO YA GHARAMA ZOTE ZA MALEZI NA MAFUNZO YA KINDA HUYO PAMONA NA MALIPO YA UHAMISHO,

KAMA KLABU YOYOTE ILIYOMCHUKUA KUTOKA KATIKA KLABU YAKE ILIYOMLEA ITAMUUZA KWA KLABU YOYOTE BASI NI LAZIMA HIO KLABU ILIYOMNUNUA ILIPE PERCENT % AMBAZO ZINATAMBULIWA NA FIFA ZA KINDA HUYO KWA HIO TIMU YAKE ILIYOMLEA MPAKA MWISHO WA MCHEZAJI HUYO ATAKAPOTUNDIKA VIATU KUACHA SOKA.

KUNATOA MFANO HAI HUU HAPA MAPAKA SASA AJAX AMSTERDAN INAPOKEA PERCENT % KUTOKA KWA KLABU YOYOTE INAYOMNUNUA ZLATAN IBRAHIMOVIC MPAKA NYOTA HUYO ATAKAPOTUNDIKA MADALUGA YAKE UKUTANI NA KUWACHANA NA MPIRA,KUTOKANA NA JAX AMSTERDAN NDIO ILIYOMLEA ZLATAN IBRAHIMOVIC WA PARIS SAINT GERMAIN HADI KUFIKIA UWEZO ALIOKUWA NAO LEO.

SUALA AZAM F.C HADI LEO HAIKUMCHUKUA MUDATHIR YAHYA KUTOKA KATIKA KITUO CHA ORANGE FOOTBALL ACADEMY KWA MKOPO WALA MALIPO YA AINA YOYOTE WALA KUWASILIANA NA VIONGOZI KWA MAONGEZI SASA SUALA JE "ZIPO WAPI HAPA SHERIA ZA SOKA ZA NCHI? " JE TANZANIA SIO MWANACHAMA WA FIFA?

JE TANZANIA HAIZIJUI SHERIA ZA FIFA KWA TIMU NDOGO ZINAZOLEA WACHEZAJI KWA GHARAMA ZAO WENYEWE KADI KUFIKIA VIWANGO VYA KUCHEZEA HIZO TIMU ZAO ZA SIMBA,YANGA NA AZAM?

KAMA SHERIA ZA FIFA ZITAFANTWA BASI VILABU VYOTE VIDOGO VITANUFAIKA NA JASHO LAO LA KUWAKUZA NYOTA HAO WA TAIFA,IKUMBUKWE HAKUNA MAPATO YA MILANGONI KWA VILABU HIVYO WALA WAFADHILI, LAKINI NI SHERIA GANI INATUMIKA KWA TFF KURUHUSA WACHEZAJI KUCHEZA LIGI BILA YA KUONYESHA NI KLABU GANI ANATOKEA NA JE AMELIPIWA HUKO ALIKOTOKA AU VIPI?

MBONA YANGA,SIMBA NA AZAM KILA SIKU WAO WANAKUWA WAKALI SANA WAKATI WAKICHUKULIANA WACHEZAJI WAO HALI YA KUWA WAO WANA MAPATO KILA PEMBE,NAMAANISHA WANAPOKEA KILA UPANDE " KAMA MUNGU WA BUDHAH BAGWANI MWENYE MIKONO MINGI?"

JE YALE UNAYOONA WEWE HUTENDEWI HAKI NA KUZULUMIWA JE VITIMU VIDOGO VYA KIMASIKINI UNAWAZULUMU NA VYOMBO VYA SHERIA VINAJUA HAYA NA VINAJIFANYA KUWA VIPOFU AU VIZIWI?

NADHANI SISI KAMA ORANJE FOOTBALL ACADEMY TUTAPIGANIA HAKI ZETU MPAKA DAKIKA YA MWISHO, MCHEZAJI SEIF ABDALLAH "KARIHE" HAKULIPIWA NA RUVU SHOOTING KWA MIAKA MIWILI WALIOMTUMIA,

NA PIA KUMUUZA KWA AZAM KAMA VILE MCHEZAJI HUYO NI MALI YAO,

NADHANI HATA KAMA ITACHUKUA MUDA GANI LAKINI NADHANI SISI KAMA ORANGE FOOTBALL ACADEMY NILAZIMA TUCHUKUE HATUA TUPATIWE HAKI ZETU KAMA VILE VILABU VIKUBWA VINAVYO PIGANIA HAKI ZAO MPAKA DAKIKA YA MWISHO.
NA KWA UPANDE WA MUDATHIR YAHAYA KILA MTU ANAELEWA KUWA MCHEZAJI HUYO HAKUTOKA MBINGUNI, NI LAZIMA AMETOKEA SEHEMU ALIYOKUWA ANAFUNDISHWA TOKEA UTOTO WAKE NA NDIO AZAM WAMEPATA KUTOKA HUKO.

LAKINI MBONA KAMA KUNA TIMU ILIKUWA IMEMLEA AZAM PAMOJA NA ATAJIRI WAO WANAADHIRIKA KWA KUIZULUMU TIMU NDOGO KAMA HII AMBAYO HAINA KIPATO CHA AINA YOYOTE?

TUNATARAJIA TFF ITAKUWA IKIFUATILIA KILA MCHEZAJI MPYA AMBAE NI CHIPUKIZI AMESAJILIWA NI TIMU GANI ALIKUWA ANACHEZEA MPAKA KUFIKIA HAPO KUSAJILI NA HIZO TIMU KUBWA ILI KAMA KUNA VITENGO VYA KUKUZA VIPAJI NCHINI SASA VIFANYE KAZI HIZO SAMBAMBA NA SHERIA ZA FIFA ZINAVYOSEMA ILI KULETA MAENDELEO YA SOKA NCHINI.

NADHANI TAYARI KITUO CHETU KINATAKIWA KUWA CHA MFANO HAPO NACHINI KWA KUTOA NYOTA HAO KWA MUDA MCHACHE TU ULIOPITA HUKU IKIWA NDIO KITUO HICHO HICHO KILICHOMLEA NYOTA ADAM NDITI WA CHELSEA KABLA YA KUHAMIA JIJINI LONDON WAKATI HUO KITUO CHETU KILIKUWA NA JINA LA FLAMINGO F.C KABLA YA KUANZA KAZI MPYA KWA UMAKINI KAMISA NA KUANZISHA PAMOJA NA KUBORESHA SHUGHULI ZOTE KWA JINA LA ORANGE FOOTBALL ACADEMY.

NI MAENDELEO GANI ZAIDI MUNAHITAJIA KAMA HAYA HAPA NCHINI KAMA HAMUTOYATUNZA NA KUANZA KULETA MAFANIKIO YA SOKA?

KWA NIABA YA KITUO CHA ORANJE FOOTBALL ACADEMY KINATOA PONGEZI ZA DHATI KWA MUDATHIR YAHYA KUVUKA KATIKA MCHUJO NA KUIWAKILISHA NCHI YETU KATIKA KUWANIA NAFASI YA KULIWAKILISHA TAIFA LETU KATIKA MICHUANO MIKUBWA KULIKO YOTE DUNIANI NA PIA PONGEZI ZA DHATI KWA SEIF ABDALLA "KARIHE" KWA KUFANYA VIZURI MSIMU MZIMA AKIWA NA AZAM KATIKA MASHINDANO YA NYUMBANI YA LIGI NA YALE YA KIMATAIFA.

TUNAWATAKIA VIJANA WETU KUZIDI KUWA NA KIU YA KUWA WACHEZAJI BORA KWA TAIFA LETU KWANI NDIO LENGO KUU LA KITUO CHETU CHA ORANJE FOOTBALL ACADEMY.

TUNATARAJI KWA VILE VILABU AMBAVYO VITAKUWA NA KIU ZA NYOTA WA SOKA VIJANA KITUO CHA KUKUZA SOKA KWA VIJANA NCHINI ORANGE FOOTBALL ACADEMY NI KIWANDA (CHA) AU SHAMBA (LA) SOKA NCHINI NA TUNATARAJIA VILABU VITANUFAIKA NA VIPAJI VYETU NA KUVIINGIZIA AU KUOKOA FEDHA NYINGI KUPITIA KATIKA KITUO CHETU CHA SOKA NA TUNATARAJIA VILABU VITAKUWA FAIRLY NA UHAMISHO WA NYOTA WETU KWENDA KATIKA VILABU VYAO.

..............
HABARI KAMILI YA STARS KWENDA ADDIS ABABA,ETHIOPIA WAKIWA SAFARINI KUELEKEA NCHINI MOROCCO NI KAMA IFUATAVYO.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka leo(jana) (Mei 26 mwaka huu) usiku kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka saa 5 usiku kwa ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake kipa Juma Kaseja.

Timu hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.

Mbali ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa.

Wengine ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd na Haruni Chanongo.

Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko.
Katika msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

PICHA KWA HISANI YA MICHUZI GOUP