KITUO CHA KUKUZA SOKA KWA VIJANA NCHINI ORANGE FOOTBALL ACADEMY KIMEZINDUA RASMI OFFICIAL WEBSITE YAKE www.ofaznz.net AMBAYO IKO KATIKA KIWANGO CHA HALI YA JUU TAYARI KUTOA KAZI ZAKE KWA UBORA ZAIDI NA URAHISI KWA WAPENZI WA SOKA NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA,
ORANJE FOOTBALL ACADEMY IMEKUWA IKITUMIA BLOG YA www.oranjefootballacademy.blogspot.com AMBAYO ILIKUWA NI KWAAJILI YA KUHIFADHIA KUMBKUMBU ZAKE KABLA YA WEBSITE HIO KUANZA KAZI RASMI jana tarehe 29-06--2013 AMBAYO SASA ITAKUWA IKITOA HABARI NJINGINE ZA ZIADA KWA VILABU VYOTE VIDOGO NCHINI AMBAO HABARI ZAO ZIMEKUWA ZINASHINDIKANA KUPATIKANA KUTOKANA NA KUTOKUWA NA WEBSITE AU BLOG ZAO HIVYO KUVIFANYA VILABU HIVYO VICHANGA HABARI ZAO KUPOTEA BILA YA KUWA NA KUMBUKUMBU ZOZOTE.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Website hio www.ofaznz.net uliofanyika katika ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Weless alitarajiwa kuwa ni Mheshimiwa mwakilishi wa jimbo la kikwajunu mhe Mahmoud Muhammed Mussa lakini kutokana na dharura za kikazi amewakilishwa na mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe Ali Salum mwanamichezo mahiri na mpenda michezo wa muda mrefu nchini ambae michango yake mikubwa imeonekana kwa muda mrefu.
Waalikwa wengi wamejitokeza katika uzinduzi huo wakiwemo Wachezaji wa zamani wa soka , makocha wa timu mbalimbali , waamuzi ,wazee wa wachezaji wakiongozwa na wenyeviti wa Z F A Wilaya ya Mjini na wilaya ya Magharibi ambapo pia ulihudhuriwa na mwanasheria maarufu Mh Abdalla Juma ambae pia ni mwanasheria wa Z F A na mjumbe wa kamati tendaji ya Z F A katika uzinduzi huo.
TUNAWAOMBA WADAU WOTE KUTOA USHIRIKIANO NA KITUO CHETU KATIKA KUWASAIDIA VIJANA WETU ILI KWA PAMOJA TUWEZE KUPANDISHA KIWANGO CHA SOKA NCHINI KWA KUTOA VIJANA WENYE UWEZO KULISAIDIA TAIFA LETU.
Tembelea website yetu kila siku www.ofaznz.net ambapo kutakuwa na habari za soka kwa vilabu mbalimbali nchini kwa mujibu tutakavyopata habari hizo,vilevile pata habari za soka kimataifa kupitia katika LINKS katika website yetu ambapo kuna website za kimataifa za soka zenye kuweka habari zote za soka za dunia nzima kila dakika.