WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Saturday 27 July 2013

BTMZ V/S VYAMA VYA MICHEZO

Na Mwandishi Maalum

HIVI karibuni, kulifanyika kikao kimoto kati ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, viongozi wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) na wale wa vyama vya michezo nchini.

Tunaposema kikao hicho kilikuwa kimoto hatutii chumvi, kwani viongozi wa vyama vya michezo walitoa shutuma nyingi kwa uongozi wa BTMZ na hilo lilionekana na kila aliyekuwepo katika kikao hicho.   Kwa kinywa kipana, viongozi hao walidai kupuuzwa na kutopewa uzito maombi yao ya ruzuku,
wanapohitaji kufanya shughuli mbalimbali za kimichezo zikiwemo safari za kwenda kwenye mashindano nje ya Zanzibar .
Kila kiongozi wa chama aliyesimama, alielezea asivyoridhishwa na namna wanavyotendewa na viongozi wa baraza hilo . 
Lazima tukiri kuwa, kuongoza watu kuna changamoto zake, na pale kunapotokea misuguano, ndio wakati mzuri wa kumpima kiongozi kama kweli amekomaa na anaweza kuirudisha kwenye utulivu hali ya hewa iliyochafuka.
Ni jambo jema kwamba baada ya kikao hicho, Katibu Mtendaji wa BTMZ aliamua kuweka bayana taarifa ya fedha alizoingiziwa kwa kipindi chote cha mwaka wa bajeti wa 2013/2014, ambazo zilikuwa pungufu na zile alizotarajia kupewa.Tunasema hatua hiyo ni ya busara,
lakini tunaona imechelewa kwani kutolewa kwake kulitokana na presha ya viongozi wa vyama kulisakama baraza kwamba ndilo linalokwamisha shughuli zao kwa kuvinyima vyama hivyo mafungu ya ruzuku.   Tunaamini kwamba,
viongozi wa vyama vya michezo ni watu wazima na wenye uelewa wa hali halisi ya kifedha inayoikabili serikali, kwa hivyo wasingekurupuka kutoa ya moyoni, ila kuna kasoro pahala fulani.Mara kadhaa,
viongozi hao wamesikika wakilalamika kupitia vyombo vya habari juu ya ukata unaovikabili vyama vyao, na kuwa wanapoomba fedha hawasikilizwi.
Utafiti mdogo uliofanywa na safu hii, umebaini kumbe tatizo ni usiri tu unaotawala baraza, kwani mara nyingi,vyama vinapowasilisha barua za kuomba ruzuku au msaada wa kuendeshea mambo yao ,   barua hizo hazijibiwi na zinabaki kwenye makabati ya ofisi za BTMZ.
Kumbe uongozi wa baraza ulipaswa kuwa rafiki wa karibu na vyama kwa kueleza ukweli mapema unapopokea barua za maombi ya fedha, badala ya kuzikalia na kushindwa kueleza kama hauna fedha zinazotakiwa au vyenginevyo.
Aidha, vipo vyama vya michezo midogo ambavyo vinapaswa kupewa kasma ndogo sana , kwa mfano chama cha mchezo wa karata, kilichopangiwa kijifungu cha shilingi laki moja, lakini hata hizo wanalalamika kuwa hawazipati.
Hatuoni mantiki ya kukinyima chama hicho kijifungu cha shilingi laki moja, kama baraza linaweza kukipa chama cha kunyanyua vitu vizito shilingi milioni tano.
Ni kweli baraza halioni pahala pa kunyofoa shilingi laki moja na kukipa chama cha karata haki yake hiyo?Tunadhani matatizo mengine hayapasi kukuzwa kwani yanahitaji busara kidogo na maarifa ya kiuongozi ili kuyatatua, na vyama vitafahamu kwani havipingi kwamba upatikanaji wa pesa ni mgumu,
lakini vinakosa imani na uongozi kutokana na usiri tu.
Ni vyema BTMZ ikaamua kujisogeza karibu na vyama kwani baraza hilo ndilo mlezi wao, na pia likumbuke uwazi katika uwajibikaji ndio silaha ya kuleta ufanisi popote pale.